Utumishi mjiongeze kwa hili kwa suala la usaili kufanyika Dodoma pekee

Aug 24, 2021
72
65
Habari JF,

Naomba Sekretarieti ya Utumishi waweze kusaidia wahitimu weweze kufanya mitihani ya Ajira wakiwa mikoani kwao.

Majuzi TRA wametoa nafasi 1097 za Ajira ambazo ni nyingi sana kwa kipindi hiki cha Uchumi wa Kati.

Sasa Kikwazo ni hizi interview kufanyika huko Dodoma pekee. Kuna mtu alikuwa Makete namfahamu alishindwa kwenye kwenye usaili uliopita wa TRA, kisa tu ni kumudu gharama.

Sasa inakuwa vigumu kwa mtu aliyekuwa labda Songea ukipiga hesabu za usafiri na makazi ni ngumu sana. Inatia huruma na ghadhabu.

Kumbuka hizi interview zinakuwa na michujo mpaka tatu ,Je kwa mtu asiye na ndugu wala kipato atamudu vp?

Nashauri waangalie njia mbadala ili wengine wasikose kisa tu ya kuwa na kipato.
 
Oops
 
Unauza mbuzi wanne upate laki 2 nauli,malazi nk toka Songea vijijini uende dodoma kupiga interview ya kwanza ya pili baada ya wiki unapiga hesabu usubirie au urudi Songea unaona usubirie unalala guest ya bei rahisi ya nje ya mji kuokoa Ili ubahitishe ajira.Baada ya interview ya pili mnaambiwa mkasubirie majibu unarudi kijijini,majibu hola haupo unaumia hasara umepoteza pesa mbuzi au mifugo na ajira umekosa ukienda Dodoma mara tano jumla ni mtaji tosha wa kufungua duka kubwa ukajiajiri kuliko kuuza mifugo ukabahatishe ajira ni SAwa na kubeti.Serikali ifanye jambo juu ya hili kuliko kuwazidishia umasikini wasaka ajira.
 
Aisee ni majanga sana mkuu. Mwisho unakata Tamaa unabaki mtaani na sifa unazo .
 
Habari JF,

Naomba Sekretarieti ya Utumishi waweze kusaidia wahitimu weweze kufanya mitihani ya Ajira wakiwa mikoani kwao.

Majuzi TRA wametoa nafasi 1097 za Ajira ambazo ni nyingi sana kwa kipindi hiki cha Uchumi wa Kati.

Sasa Kikwazo ni hizi interview kufanyika huko Dodoma pekee. Kuna mtu alikuwa Makete namfahamu alishindwa kwenye kwenye usaili uliopita wa TRA, kisa tu ni kumudu gharama.

Sasa inakuwa vigumu kwa mtu aliyekuwa labda Songea ukipiga hesabu za usafiri na makazi ni ngumu sana. Inatia huruma na ghadhabu.

Kumbuka hizi interview zinakuwa na michujo mpaka tatu ,Je kwa mtu asiye na ndugu wala kipato atamudu vp?

Nashauri waangalie njia mbadala ili wengine wasikose kisa tu ya kuwa na kipato.
Mimi pia yamenishinda kwenda gharama ni kubwa na risk ni kubwa ..
 
Nimeshashindwa kwenda interview nyingi hizo za Utumishi zinapoitishwa Dar es Salaam, kutokana na gharama na kiongezea na idadi ya ajira inayokuwa imetolewa na idadi ya watu mlioitwa kwenye interview hiyo.
 
Aisee ni majanga sana mkuu. Mwisho unakata Tamaa unabaki mtaani na sifa unazo .
Na pesa imeenda darasani na kwenye interview.
Huku darasa la saba ambae aliumia baada ya kushindwa kuendelea na sekondari kwa factor mbalimbali mfano uchumi,mwako, mazingira,nk yeye akiwa alishapona maumivu yake yupo anapambana na madegree ya maisha aliingia kwenye kilimo,madini,uvuvi, biashara,udereva akiwa na experience ya kutosha mtaani kuhusu maisha.Aingie wapi atokeee wapi,unamtegemea kumpiga virungu.
 
Ndio namna ya kuchuja watu. Mimi niliwahi kuomba nafasi ya kazi ya ndani ya Shirika Niko Mkoani machakani nilipewa taarifa saa 7 mchana kuwa kesho yake natakiwa kwenye Interview saa 3 Dar hata ningeondoka baada ya kukata simu nisingewahi.
 
TRA wa organize iwe inafanyika kikanda mfano kanda ya mashariki wafanyie Dar, kanda ya kati wafanyie dodoma, kanda ya ziwa wafanyie huko mwanza, hii itaounguza gharama, halafu watu waliofaulu kwenye oral Sasa watumike Skype, zoom, or Microsoft teams kuwafanyia interviews mbona mashirika makubwa people work from home hadi kufanya meeting. Hii kurundika dodoma ni gharama sana hebu wawe wabunifu
 
Back
Top Bottom