UTUMISHI: Kugoma kwa baadhi ya kada kwenye maombi ya ajira za TRA

Capital G

JF-Expert Member
Jul 2, 2017
3,447
5,299
Wakuu salaam,

Nina mdogo wangu kamaliza chuo mwaka 2018, ana bachelor degree ya Business Administration, kashafanya usaili wa Mamlaka ya Mapato mara mbili sasa, cha ajabu leo wakati anaomba kwenye hizi nafasi mpya zilizotangazwa anaambiwa hana "qualifications" za kuomba kada hiyo na kwenye tangazo wameandika kabisa wanahitaji mtu wa business administration.

Nashindwa namna ya kuwafikia watu wa Utumishi (Kwa maana ya mawasiliano), kama kuna mtu ana namna ya kunisaidia ili kijana aweze kuomba ajaribu bahati yake basi nitashukuru sana.

Naamini, dubwana hili ni kubwa na kuna watu wengi sana wanaoweza kuwa msaada katika hili tusaidieni ili dogo ajaribu bahati yake, nakala za kuitwa kwa nafasi hizi mara mbili zipo katika portal ni ajabu leo anakataliwa.

Wakuu, msaada wenu una umuhimu sana kwa namna yoyote ile.

Natanguliza shukrani.

N.B: Naambatanisha picha nayopata baada ya kila akijaribu ku - apply, pamoja na requirements za kada hiyo

20211025_234231.jpg

View attachment 1986876
 
Hili Ni kila mtu inasumbua hata lile kwa mwezi wa sita ilichelewa pia kukubali hvyo awe na subira kdg wanaweka mambo ssswa utaona zinakubali zenyewe kutuma ..sas HV nimetoka kutupia ila naona inagoma ..
 
Nadhani ni system haijakaa sawa maana kuna wengine wakati wa kuapply inachelewa kuload
 
Mdogo wangu kasomea record management chuo cha utumishi wa uma (TPSC) ngazi ya diploma lkn akichagua chuo kinakuja but course aliyoisoma ahionekan kwenye academic qualification

Msaada pia katika hili Jman
 
Mdogo wangu kasomea record management chuo cha utumishi wa uma (TPSC) ngazi ya diploma lkn akichagua chuo kinakuja but course aliyoisoma ahionekan kwenye academic qualification

Msaada pia katika hili Jman
Waandikie email ukiambatanisha na cheti chako ambayo program yake haionekani. Mimi nilitumia mbinu hiyo na nikafanikiwa na nikaikuta
 
Back
Top Bottom