Natania
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 262
- 217
Nimejaribu Kupiga namba zinazoonekana kwenye tangazo lao la dawati la msaada na naambiwa namba ninayopiga (ya kiganjani) haipo. Najiuliza shida ni nini hasa? Haya nikaamua kupiga namba ya simu isiyo ya kiganjani nayo haiiti wala nini. Hayo yote tisa, kumi ni jinsi hizo namba za simu zilivyoandikwa. Hivi kwa ofisi nyeti kama hiyo kwa nini watoe tangazo la muhimu kama hilo lakini namba ya kupiga iwe ni 2118531? Mtu wa Sumbawanga akiwapigia atawapata? Ama wanadhani watu wote wanaishi Kinondoni?