Utumikishaji Watoto Wadogo (Child Labor) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumikishaji Watoto Wadogo (Child Labor)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IshaLubuva, Jul 9, 2009.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kumekuwa na harakati mbalimbali ambazo zinaendeshwa na wadau mbalimbali za kutetea watoto wadogo dhidi ya kile kinachoitwa utumikishaji wa watoto au kwa kiingereza child labor. Lakini mara nyingi utakuta kwamba watoto wanaoangaliwa zaidi ni wale ambao wanafanya/wanafanyishwa kazi za mashambani na kwa kiasi kidogo wanaofanya kazi za majumbani.

  Hoja ninazoziweka hapa na kutaka tuijadili ni hii hapa;

  Je watoto tunaowaona wakitumika katika kuigiza (kama walivyofanya Orijino Komedi au yule yule mwanamziki wa Bongo Fleva aliyeimba Neema, n.k), kwenye filamu kwenye muziki, kutangaza vipindi vya Runinga na Redio n.k. hawa wanaangukia kwenye kundi lipi?

  AU

  wale wanaofanya kazi za mashambani wanalengwa zaidi kwa kasumba kuwa kazi hiyo ni duni (au siyo kazi).

  Je watoto wadogo wanaoshirikishwa kwenye tamthilia na filamu huku wakilazimika kushuhudia wazazi wao wa bandia wakigombana, kutukanana na kupigana wanakuwa wanafunzwa maadili gani kwa ajili ya manufaa ya maisha yao?

  Je ni watoto hao huwa wanalipwa ujira wowote/, nani ambaye hulumbana (negotiate) ujira huo na pia nani huchukua ujira wa watoto hao ambao hawajui kuwa wanashiriki katika kutengeneza kipato?

  Karibuni tujadiliane
   
Loading...