Tetesi: utumiaji wa oil za magari na umbali wa kutumika

Ahoks92

New Member
Sep 25, 2017
3
1
wadau naomba kueleweshwa suala zima la oil....
mfano watumia gari dogo ist...unakuta unaaambiwa weka oil flan ya km 3000 mara mwingine oil hii kma 50000 mara ooo oil hii nyepesi sana si nzuri..mara hii nzito sana si sawa!! basi sijawah kuwa na jibu sahihi ni oil gan kwa ajili ya matumizi na umbali sahihi!!!
 
Ili uweze kujua oili ipi inafaa zaidi au haifai ni vyema ukaelewa kazi ya hiyo oil katika injini ya gari. Baada ya kuelewa hili utajua utumie oili ipi kwenye gari yako. Je, oili inakazi zipi kwenye injini?
1. KUPUNGUZA MSUGUANO; Kutokana na msuguano unaotokea ndani ya injini ni lazima kuwe na oili(lubricant) ili kupunguza huo.
2. KUPOOZA INJINI; Hii ni kazi nyingine na muhimu kwa afya ya injini ya gari lako. Kutokana na msuguano mkubwa wa vyuma wakati injini imewaka, joto kubwa sana hutengenezwa na injini hivyo uhitaji kupoozwa. Hii haimaanishi hakuna mifumo mingine ya upoozaji wa joto ndani injini ya gari. Mifumo mingine ikiwemo upepo na maji husaidiana katika upoozaji wa injini ya gari yako.
3KUSAFISHA INJINI YA GARI YAKO; Nini husafishwa ndani ya injini? Kutokana na msuguano wa vyuma ni vigumu sana kwa oili kuzuia kwa asilimia mia moja vyuma ndani ya injini kulika(tear). Hivyo vipande vipande vya vyuma ambavyo ni vidogo vidogo sana(si rahisi kuviona au kuvishika) hutolewa ndani ya injini kama uchafu. Usafishaji wa moshi au majivu(soot) kwenye kuta za chumba cha uunguzaji mafuta. Hivyo oili huondoa uchafu huu.


Kwa haya machache kati ya mengi matumizi ya oili ndani ya injini kwa nionavyo mimi oili inayofaa ndani ya injini ya gari ni ile isiyokua nzito sana wala nyepesi sana. Pia oili hiyo inapaswa kua imara(stable) oili ambayo mabadiliko ya joto ndani ya injini hayawezi kubadili hali(state) yake aidha kua nyepesi sana au nzito sana. Hii ni kutokana na kazi au matumizi ya oili ndani ya injini kama yalivyoainisha hapo juu. Mfano oili inaweza kua nzuri na inauzito unaotakiwa lakini isiwe imara ikabadilika na kua nyepesi sana. Hii itasababisha oili hii kushindwa kuzuia msuguano ndani ya injini kwa ufanisi mkubwa(high efficient).
NOTE; HAYA NI MAONI YANGU BINAFSI KULINGANA NA UZOEFU NILIONAO KIDOGO NA SI MTAALAM WA MAMBO YA MAGARI. UKIONA HUJAELEWA AU UNAPATA SHAKA AU UNAPATA UKAKASI PAHALA FULANI JUU YA MAELEZO TAJWA JUU HAPO UNAWEZA KUYAPUUZA.
 
Sasa hivi miji yetu kama Dar ni vigumu sana kuhesabu KM ili kubadilisha oil, hii inasababishwa na gari kukaa kwenye foleni ikiunguruma... Hapa ni suala la kutumia akili tu na kubadilisha oil basi. Hivi kwenye jenereta tunabadili oil baada Km ngapi vile???
 
Back
Top Bottom