Utumiaji wa Lugha Isiyofaa ya Matusi na Udhalilishaji

MABAGHEE

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
682
126
Ndugu wana jamvi, tangu Dr. Mkumbo na Mh. Zito wasimamishwe nyadhifa zao CHADEMA kumekuwa na maoni mbalimbali yanayotolewa na wadau. Wapo ambao wamekuwa wakipinga maamuzi ya kamati kuu na wengine wakiyaunga mkono. Binafsi nayaheshimu maoni ya watu wote.
Lakini nimekuwa nikisikitishwa na lugha inayotumiwa na baadhi yetu. Wengine wamekuwa wakitoa lugha ya matusi, kejeli na udhilishaji. Jamani hata wakosaji wanahaki zao. Kila mmoja wetu anaamini hawa mabwana wameifanyia CHADEMA mambo makubwa mazuri, iweje leo wadhalilishwe na kudharauliwa kiasi hicho hata kabla ya hukumu ya mwisho? Mbona utetezi wao bado na sisi tumeshatoa hukumu? Jamani hawa ni binadamu na si malaika kukosea ni sehemu yakujifunza ingawa kwa tuhuma nilizozisoma sioni kosa lao. Kwenye siasa ni lazima kuwe na kambi, si watu wote wakubaliane na utendaji wako. Sasa wale wanaokupinga usiwaone niwadhambi sana au wahaini. Nimeshangazwa watu wanafikia hatua ya kuingilia maisha binafsi ya Mkumbo na Zito. Familia zao zinakuwa zimewakosea nini? Narudia tena kuwa na mawazo tofauti ndo kunaweza kujenga chama na sivinginevyo. Dunia hii tungekuwa watu wote tunamitizamo inayofanana pengine tusingeendelea. Tukosoane na kuonyana kwa kuheshimiana, Leo kwangu kesho kwako. Sidhani kwamba matusi yatafanya watuhumiwa kujifunza lolote.Unaweza kuuona ujumbe huu kwa mtizamo tofauti, hoja yangu ni kwamba hata kama hupendi nilichokiandika, huitaji kunitukana au kunidhalilisha au kunikejeli. Haiwezekani watu wote tufikiri the same way.
 
Back
Top Bottom