Utumiaji wa Alovela katika kuponya magonjwa mbalimbali ya kuku

theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,750
15,636
UTUMIAJI WA SHUBIRI MWITU KWA KUKU
zipo dawa tofauti za asili zinazopatikana kirahisi kwenye mazingira yetu ambazo zina uwezo wa kutibu magonjwa ya Kuku katika page hii tutajifunza baadhi ya hayo.

UGONJWA: VIDONDA VITOKANAVYO NA NDUI
Kuku hupata vipele vya mviringo, Kuku hupata vipele kwenye upanga wake wa kichwani, masikioni, miguuni na sehemu zisizokuwa na manyoya.

MMEA WA KUTUMIA:
LUGHA JINA LA MMEA
Kisayansi: Aloe vera
Kiswahili: Shubiri mwitu
English: Aloe
Kihehe: Litembwetembwe
Kinyaturu: Mkankiruri
Kigogo: Itembwe
Kinyiha: Ibhata
Kikaguru: Koli

KUANDAA
chuku majani ya shubiri na kuyachana
vipande vidogo vidogo.
vitwange na pumba kidogo na kuvianika.
vikiisha kauka vitwange na kuchekecha upate
unga laini.
hifadhi unga katika chombo kisafi na kikavu.

KUTUMIA
• Safisha vidonda vilivyotokana na ndui au
vidonda vyovyote vile na maji safi yaliyo na
chumvi kiasi (sio nyingi).
• Paka unga wa shubiri mwitu katika vidonda
vilivyosafishwa.
• Rudia tena baada ya siku moja. Tumia hivyo
mpk vidonda vikauke.

KUDHIBITI MAGONJWA MENGI MENGINE YA KUKU KWA KUTUMIA SHUBIRI MWITU NI KAMA IFATAVYO:
chukua jani moja la shubiri mwitu lenye
ukubwa wa kati.
likate katika vipande vidogo vidogo
loweka vipande ulivyokata katika maji kiasi
cha Lt 2( Kuku hutumia maji hayakunywa
yakiwa na vipande hivi vya shubiri mwitu hadi
unapobadilisha

KUTUMIA
-> Kuku watumie maji haya kwa kunywa siku
zote.
-> Hii inafanya kazi Kwa kuwakinga Kuku dhidi
ya magonjwa mbalimbali.
-> Badilisha maji hayo kabla hayajaanza
kuchacha na kuwatengenezea dawa nyingne.
-> Hakikisha chombo kinasafishwa vizuri kabla
ya kuweka dawa nyingne.

USHAURI WANGU, kwa wafugaji wenzangu mpande mimea ambayo itatumika kama Dawa na chakula ilikupunguza gharama ,kama hizo aloe vera ,lusina , mlongelonge, pilipili kichaa nk

Waweza share nasi dawa ya asili uliowahi kuitumia na ikatibu magonjwa mbalimbali ya kuku, ili kusaidia wafugaji wengine.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom