UTUMIAJI MADAWA,USHOGA:Vithibitisho vya unafiki na ujinga wa watanzania na viongozi wetu.

Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
2,198
3,579
Nianze kwa kutoa salamu zangu za mwaka mpya kwa wanajamvi humu ndani,poleni sana na haka kahali kalikoanza kujitokeza baada ya kufanya kufuru kubwa ya matumizi katika sherehe hizi za mwisho wa mwaka,kipindi hiki kitaisha tu

Nijikite moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu,tangu tarehe za mwisho za mwezi wa 12 mwaka 2016 kumekuwa na mijadala mipana katika mitandao ya kijamii,vyombo vya habari,vijiweni n.k kuhusu suala la matumizi ya madawa ya kulevya,mijadala ilikuwepo tangu zamani lakini imekuja kupamba moto siku za hivi karibuni baada ya kuzagaa kwa picha za chid benz ambaye hakuna asiyemfahamu,baadae picha za nando wa BBA.

Picha hizi ndio zimefanya mijadala hii kupamba moto lakini kwa mtazamo wa mimi naona ni muendelezo wa tabia za unafiki wa sisi watanzania pamoja na viongozi wenye dhamana ya kusimamia masuala haya,mijadala hii imekuwa inapamba moto kipindi ambacho madhara yanakuwa yamekwisha kujitokeza,kipindi ambacho kama ni nguvukazi basi imekwishapotea na juhudi zote hazitaweza kuubadili ukweli kuwa tumeshapoteza.

Vyombo vya habari vimekuwa vikiyachukulia haya masuala kishabiki zaidi,sometimes wanayatumia kama fursa ya wao kupata umaarufu zaidi,suala la chid benz tangu anachukuliwa kupelekwa soberhouse lilikuwa linachukuliwa kama utaniutani hivi,hivi ni lini mtu akaacha madawa kwa kulazimishwa au kushawishiwa na mtu?,then akakae soberhouse siku si zaidi ya 30 akawa kaacha madawa kabisa?!!,basi kumbe kazi hii ingekuwa rahisi sana.

Hatuna tabia ya kuzuia matatizo kipindi yanaonyesha dalili za kutokea,bali huwa tunajipanga kutatua kipindi yakitokea tena kwa mbinu za 'kijanjajanja',ishu ya madawa siyo suala la ujanjaujanja,ni suala serious na tunaona linavyosumbua dunia nzima.

Kuna hili suala lingine la ushoga ambalo kwa sasa kulitamka katika vyombo vya habari ni kama laana,lakini kiuhalisia ndio kinachoendelea sahivi mitaani,ukitaka thibitisha fuatilia huko instagram ambako siku hizi watoto wetu wadogo wako wanatumia mtandao huu maarufu,wakati tukijidanganya kwa kukaa kimya kwenye vyombo vya habari tukayajadili kwa upana watoto wetu wanapata hizi habari kwa urahisi kuliko fikra zetu,na kwakua hakuna mijadala ya kukemea hadharani maana yake hakuna cha kuwafanya waone ni jambo la ajabu ndio tunajikuta tunakuwa na watoto wa ajabuajabu mitaani&mashuleni n.k siku hizi movies kibao zina vipande vya kuchochea ushoga ila hakuna mijadala ya wazi ya kuwafanya hawa watoto wajue kuwa hivyo vitu ni haramu,masikini sijui tutakuwa na kizazi cha aina gani miaka 20 ijayo.

Siku hizi hakuna watoto wa kiume wanaolelewa kiume,wote wanavaa visuari vya kubana,mitindo hatarishi ya nywele na mapozi ya ajabu ambayo ukikaa ukajiuliza mara mbili tatu unapata hofu sana na future ya hili taifa.

Tukitaka tumalize haya ni kuruhusu tu mijadala ya wazi,hakuna namna maana hakuna cha kuficha sasa,watoto wanajua kila kitu vingine hata wazazi hatuvijui.

Unafiki wa viongozi pia ni tatizo,nakumbuka kipindi cha kwanza zamaradi kukirusha kuhusu yule kijana shoga siku ya pili kulikuwa na mjadala clouds 360 na mh mkuu wa mkoa wa dsm alipiga simu na kutoa maneno ya kumpongeza zamaradi kwa ujasiri wa kuibua mjadala ule,lakini siku chache baadae alitoa tangazo la kuwakamata mashoga wote,sasa unajiuliza je kuwakamata ndio solution ya kudumu??!!!!!

Utatuzi hapa ni kuwa na mikakati ya muda mrefu,kila muhusika acheze kwenye nafasi yake kuanzia familia hadi ngazi ya jamii.,kinyume na hapo tumekwisha.
 
Yote uliyojadili hapo juu ni maswala binafsi si mijadala, nguvu au chochote kile kitamaliza hayo mambo kabisa.

Swala kama la ushoga sio ishu kabisa bongo thus far. Ni nyie mnaoshinda Instagram ndiyo mnawajua hao mashoga na kulikuza hili swala ila huku mtaani hawapo wala hatuwaoni, katika watz 10 watu 9 hawamjui shoga yeyote katika jamii yao utasemaje hilo ni jambo linalotaka attention. Katika nchi ya watu 45mil mashoga hawafiki hata 10k bado mnataka tulipe attention? Kikwete alisema vizuri "tuna mambo mengi ya kujadili kabla ya kujadili ushoga".

Kwa upande mwingine wanasema any publicity is good publicity hivyo katika hiyo mijadala badala ya kumaliza tatizo mtajikuta mnalipa exposure zaidi na kuongeza idadi ya mashoga. Aidha mtu kuwa shoga ni uamuzi wake binafsi maisha yake chaguo lake so long as haingilii mambo yako kwanini kusumbua akili kwa kitu mtu anachofanya chumbani kwake!! Tuna mambo mengi ya kufanya
 
Back
Top Bottom