Utumbuaji wa watu kama akina Mtela Mwampamba utatutokea puani siku moja

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Watu tunakumbuka sana kuwa Mtela Mwambapa na Juliana Shonza walikuwa ni WanaCHADEMA na walipohamia CCM wanajulikana kama wanasiasa na sio watendaji. Regime hii ya Magu iliwachukua wanasiasa wa aina ya Mtela Mwambapa na kuwafanya watendaji. Nafikiri mnamkumbuka Tumbili pia - Ajabu sana! na Mwenyezi Mungu anamwona sana tu JPM!

Sasa kubwa kuliko zote unaona Mtela Mwambapa anavyoingizwa kwenye utumishi wa umma kinyemela. Yaani hivi hivi na WaTanzania tunaangalia tu. JPM alitoa maelekezo kuwa Mtela Mwambapa apewe kazi ndogondogo kuliko ile ambay alikuwa akiifanya kama DAS.

Kazi ndogo ndogo kwake ama ni kuwa Afisa Tawala wa Wilaya au Afisa Tarafa. Kwa kuangalia kwa kina ina maana Mtela Mwambapa ameingia kwenye utumishi wa umma bila utaratibu unaopaswa kufuatwa. Yaani hamna usaili wala nini! Serikali ya JPM hiyo! Kazi kweli kweli.

Mtela Mwambapa anajulikana wazi wazi kuwa ni Mwanasiasa, sasa leo hii ndiyo unamkuta yupo Ofisi ya Umma - atawezaje kuwatumikia bila upendeleo wasio wanaCCM?

Ukweli haya mambo yaendelee tu kufanyika lakini mwisho wake unakaribia kufika! Akina Membe watayasema soon?
 
Kuna kazi za kisiasa na zisizo za kisiasa nakubaliana na wewe kidogo pia nitatofautiana pia kazi za kisiasa ni kama ukuu wa wilaya au mkoa lakini ukurugenzi, ukatibu tawala, makatibu wa wizara siyo kazi za kisiasa.
 
Rais Magufuli amevuruga mifumo mingi sana Nchini. Na mpaka atakapotoka madarakani, huenda akavuruga zaidi na zaidi. Sheria na kanuni nyingi zinakiukwa mchana kweupe! Hili halikubaliki.
 
kwa kweli wote tunajiuliza alipewaje cheo kama hiki ambacho 1. lazima uwe umeajiliwa serikali kwa merit 2. umepanda vyeo kufuata cadre yako mpka kuwa senior. huyu alikuwa mwanasiasa hajui hata taratibu za utumishi wa umma ndo maaan unamwona yuko easy tu na bosi wake mwegelo kitu amabcho sio sawa katika utumishi wa umma. Ila kama mlivyoonya hapo juu awamu ya 6 itapata tabu sana kurekebisha madhaifu ya awamu ya 5.
 
Watu tunakumbuka sana kuwa Mtela Mwambapa na Juliana Shonza walikuwa ni WanaCHADEMA na walipohamia CCM wanajulikana kama wanasiasa na sio watendaji. Regime hii ya Magu iliwachukua wanasiasa wa aina ya Mtela Mwambapa na kuwafanya watendaji. Nafikiri mnamkumbuka Tumbili pia - Ajabu sana! na Mwenyezi Mungu anamwona sana tu JPM!

Sasa kubwa kuliko zote unaona Mtela Mwambapa anavyoingizwa kwenye utumishi wa umma kinyemela. Yaani hivi hivi na WaTanzania tunaangalia tu. JPM alitoa maelekezo kuwa Mtela Mwambapa apewe kazi ndogondogo kuliko ile ambay alikuwa akiifanya kama DAS.

Kazi ndogo ndogo kwake ama ni kuwa Afisa Tawala wa Wilaya au Afisa Tarafa. Kwa kuangalia kwa kina ina maana Mtela Mwambapa ameingia kwenye utumishi wa umma bila utaratibu unaopaswa kufuatwa. Yaani hamna usaili wala nini! Serikali ya JPM hiyo! Kazi kweli kweli.

Mtela Mwambapa anajulikana wazi wazi kuwa ni Mwanasiasa, sasa leo hii ndiyo unamkuta yupo Ofisi ya Umma - atawezaje kuwatumikia bila upendeleo wasio wanaCCM?

Ukweli haya mambo yaendelee tu kufanyika lakini mwisho wake unakaribia kufika! Akina Membe watayasema soon?
Mkuu wa nchi ana vyombo vingi vya kumpa habari ingawa nahisi kuna wakati vinamuingiza chaka.Tukiangalia Mwigulu,Kicheere,Andenginye wa Zima moto na wengine inaelekea kuna shida mahali.Hata hivyo huyo ndiye Rais wetu na tunachoweza kfanya 'Kuguna na kuvumulia"
 
Back
Top Bottom