Utumbuaji majipu wa Rais Magufuli wakwamisha kusafirishwa kwa mizigo bandarini kwenda ughaibuni

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,173
Kuna kontena kadhaa za mzigo fulani zimekwama haziwezi kupanda meli kwa kuwa hazina kibali cha idara fulani ya serikali ambapo inaarifiwa wahusika wa kutoa vibali hivyo huko katika idara hiyo ya serikali wametumbuliwa majipu na kwa hiyo basi ili kukipata kibali hicho ama waliotumbuliwa wakamuliwe usaha vizuri wapone warudi kazini au wabaki hukohuko waajiriwe wengine ndio hapo kibali kitatolewa.

Muwekezaji kakasirika sana kwa utaratibu huu mbovu.
 
kuna kontena kadhaa za mzigo fulani zimekwama haziwezi kupanda meli kwa kuwa hazina kibali za idara fulani ya serikali ambapo inaarifiwa wahusika wa kutoa vibali hivyo huko katika idara hiyo ya serikali wametumbuliwa majipu na kwa hiyo basi ili kukipata kibali hicho ama waliotumbuliwa wakamuliwe usaha vizuri wapone warudi kazini au wabaki hukohuko waajiriwe wengine ndo hapo kibali kitatolewa.

muwekezaji kakasirika sana kwa utaratibu huu mbovu.

Ukute muwekezaji ana order yenye time limit.
 
Habari na kuficha ficha unayoongelea au unapopaongelea, kwa kweli kama mie naona hewa tu kwa sasa.
 
kwenye containers kuna nini isije kuwa tembo na twiga wetu au mchanga toka machimboni. achelewe tuu maana hakuna namna
 
Back
Top Bottom