Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?!

Hakuna busara kabisa aisee. Mh rais ukienda hivi hutafika popote. Toa adhabu lakimi za kibinadamu. Argument kwamba eti je, walipokuwa wanaiba walikuwa na ubinadam kwa maskini? Haina maana. Wewe kama mkuu wa nchi ni mtu mkubwa sana. Hupaswi kufanya mambo km unalipiza kisasi. Hupaswi kujishusha kwenye level ya huyo anayetuhumiwa alibehave inhumanely. Wewe unajitanabahisha km mcha Mungu, basi ujue Mungu hapendi kisasi. Mtendee mtu mbaya kwa wema ili aweze kujirudi! Ni hsyo tu Mr President.
 
Mi nnacho jua haija wahi toka mtu aka waridhisha binadam wotee, malalamiko na ukosoaji uendelee tuu ni mzuri.

Lakin pia mi nnacho msifia Rais ana malengo mema, anaweza asi tu please kila siku ila kujua kuwa rais ana ifikira nchi yake na maendeleo na kuchapa kazi ni vizuri.

Na wenye mawazo mbadala waruhusiwe, wenye kupinga waruhusiwe pia, ila nao malengo yao yawe nchi, isije kuwa hisia za kuhurumia watumbuliwaji, au kupinga tuu.

Pia uyu mama kisheria na kikatiba haja onewa kwa kuwa ni nafas ya uteuzi. Rais ana haki ya kumtoa muda wowote, infact TIC yenyewe haikuwa na jipya chini yake
 
Hakuna busara kabisa aisee. Mh rais ukienda hivi hutafika popote. Toa adhabu lakimi za kibinadamu. Argument kwamba eti je, walipokuwa wanaiba walikuwa na ubinadam kwa maskini? Haina maana. Wewe kama mkuu wa nchi ni mtu mkubwa sana. Hupaswi kufanya mambo km unalipiza kisasi. Hupaswi kujishusha kwenye level ya huyo anayetuhumiwa alibehave inhumanely. Wewe unajitanabahisha km mcha Mungu, basi ujue Mungu hapendi kisasi. Mtendee mtu mbaya kwa wema ili aweze kujirudi! Ni hsyo tu Mr President.

Wapi kuna adhabu ya kibinadamu. Ukimchapa mwanao pia atasema adhabu hiyo si ya kibinadamu. Adhabu ya kunyongwa ambayo ipo kisheria nayo ni ya kibinadamu?

Hizi busara kwenye mambo yanayohitaji maamuzi magumu ndio imetufikisha hapa tulipo. Kila mtu anafanya na kutaka kufanya vitu at will, bila kuwa na mshika kengele hatuwezi kuondoka tulipo wala kufika tunapotaka kwenda yaani kumkomboa mwananchi maskini asiye na uhakika wa mlo mmoja kwa siku na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
 
Haya mambo ni mazuri kuyasikia kwa mwenzio tu.manina yakukute wewe au mama/baba ako utatia akili.Kabwe yalimkuta akiwa kalazwa India...hadharani mbele ya mashabiki.This is inhuman.Naungana na Pasco naunga utumbuaji,lakini siungi approach yake,imekaa kishamba ni kama watu wanajipikilisha
Nyie vijana hamna msimamo, kipindi cha JK mlileta lawama sana, leo mnataka watu watumbuliwe gizani, subili na wewe huko Halimashauri huko, hakuna staha wala nini
 
Nnamuunga mkono sana rais wetu ni kwa kipindi kifupi amefanya kazi kubwa sana ila kwa ili la mkurungezi wa TIC ata mimi limenigusa ni ukweli hakutendewa haki Bibi Julliet Kairuki ana uwezo mkubwa sana kiutendaji.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Nimeshatahadharisha Mara nyingi humu. Kwa wale watendaji waliozoea ujanja ujanja. Public service is not for you kipindi hiki. Hivi kweli bila aibu unaweza kusema eti for the past three years ulikuwa kwenye negotiations za mshahara? Hivi watanzania walipa kodi mnatuonaje? Kairuki from day one alivunja mkataba wake mwenyewe kwa kukataa kupokea huo mshahara mdogo. Tufike sehemu tuheshimu ofisi za umma. Hata kama aliletwa kama diaspora....but she was subject to the laws and regulations of our country. Hizi story nyingine in za vijiweni. Kama Aliona maslahi in kidogo.......angeikataa hii kazi from day one. Hii nchi in yetu sote...kuna Watu wanaitumikia jamhuri yetu kwa ujira mdogo sana na mazingira Magumu. Here you have akina Kairuki eti wanafanya kazi bila mshahara kwa sababu in mdogo. Na wanakula millions kwenye posho .......It is an insult to our collective conscious as a nation. Watumbuliwe tuu. Hakuna namna.
 
Makongamano Na maforum mmefanya kibao wakati wa JK mmeleta tija hipi ? Wacha kwanza Magufuri asawazishe uwanja alafu haya maforum yatakuja kibao , huwa hayaishi hayo ndugu zangu hata ukienda marekani bado wanatafuta wawekezaji, uwekezaji ni kazi ya kudumu
Unafikiri nchi itapiga hatua kwa kufukuzana daily bila Sera za kuvusha nchi ni wastage of time matatizo ya haya nchi ni ccm wala sio wafanyakazi. Wanasiasa wezi ndo wametufikisha hapa sasa hasira zinahamishiwa kwa workers
 
Tuelezane ukweli , uteuzi wake tangu mwanzo ulikuwa zaidi ya ujuzi kwa aliyemteua , taasisi siyo MTU mmoja , haya mambo ya teuzi za kishikaji hayana nafasi kwa serikali ya Magufuri. Utatumbuliwa hats ukiwa unaendesha kikao ukumbini
Nyani Ngabu The Boss wakubwa kama mtakumbuka tulizungumzia sana kuhusu mfumo. Tulionekana mahayawani na punguani. Leo wanazungumzia tulichokisema bila kujua wanazungumzia mfumo

Tunapataje viongozi wa taasisi nyeti kama hii! Kiushikaji, kisifa au.

Kwanini dhamana ya masilahi ya mtu anayeongoza taasisi hii yawe mikononi mwa mtu mmoja? Kuna ushirika gani wa kikazi, kati ya bodi, wizara na Ikulu?

Nani anapanga mishahara ya watumishi wa umma? Mikataba naingiwaje na kwa njia gani?

Taratibu wataelewa tunazungumzia nini.
 
Wanabodi,

Hili ni swali, Jee, huu Utumbuaji Majipu wa Rais Dr. John Pombe Magufuli: Which is which?!
A: Is He Doing The Right Thing, at The Right Time, And Doing It Right?
B: Is He Doing , The Right Thing, at the Right Time but in a Wrong Way?.
C: Is He Doing The Right Thing, at The Wrong Time, But Does It Right?,
D: Is He Doing The Wrong Thing, at The Wrong Time, And Doing It Wrong?.

Tangu rais Magufuli aanze utumbuaji, amekuwa akishangiliwa sana na watu, kuna maeneo ambayo amefanya utumbuaji sahihi, katika muda sahihi na kwa usahihi, yaani doing the right thing, at the right time and doing it right!. Kwa utumbuaji huu, rais amefanya kitu sahihi, na anastahili pongezi!.

Lakini pia kuna utumbuaji ambao amefanya kitu sahihi, katika muda sahihi lakini alivyokifanya amekifanya vibaya!. Hii ni doing the right thing, at the right time, but in a wrong way!, yaani not doing it right, lakini pia kuna utumbuaji ambao ni right thing, at the wrong time and doing it right,
lakini pia kuna utumbuaji, amefanya a wrong thing, at the wrong time, and does it wrongly, na mfano hai wa hili ni huu utumbuaji wa leo wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ewekezaji, TIC, Bibi Julliet Kairuki, kwa mujibu wa sababu zilizotolewa, huu ni utumbuaji wa wrong thing, umefanywa at the wrong time and in a wrong way!.

Kwa mliofuatilia media jana mliona Julliet ametayarisha mikutano mikubwa miwili ya uwekezaji ambayo yote inafanyika leo. Asubuhi tulikuwa na mkutano wa uwekezaji katika Tanzania na Singapore pale Kilimanjaro Hotel, na mchana huu tuko ukumbi wa JNICC kwenye mkutano wa wawekezaji kutoka Urusi, Juliet ndiye alikuwa moderator, hivyo hata kama ilikuwa ni kumtumbua, why umtumbue leo?!, kwa nini asingesubiri angalau mikutano hii ikapita ndipo akamtumbua!, utumbuaji wa aina hii ni very unfair!.

Naunga mkono juhudi za rais Magufuli katika utumbuaji wa baadhi ya majipu, anafanya kazi nzuri, lakini siungi mkono huu utumbuaji ambao sio utumbuaji sahihi, kwa muda sahihi na bado unafanyika in a wrong way!. Japo rais wetu ni binadamu na sio malaika, hivyo anaweza kufanya makosa, lakini yeye kama mkuu wa nchi, macho yetu wote yako kwake, hivyo we have very high expectations on him to be perfect, it is not only about doing the right thing at the right time, but he got to do it right!.

Nimeguswa sana na hili!. Just imagine mko kwenye international investment forum, imechelewa kuanza kwa sababu Juliet anasubiriwa kuja ku modarate, no one tells us anything, ndipo Waziri wake kaja na kusema tuendelee tuu bila yeye!, kumbe....keshatumbuliwa!, huu ni utumbuaji gani?, kulikuwa na urgency gani?!.

Kiukweli Magufuli ni noma!, ni hatari sana!. Akiendelea hivi, hatuwezi kuwa na mwisho mzuri kutoka na pile up ya negative forces zitakazoweza kutengeneza a bad 'karma', na kiukweli 'karma' ni karma tuu, haina mswalie mtume!. Nasisitiza mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!, hata mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa, japo atanyongwa ila shurti atendewe haki!, haki sio favor ni right!.

NB. Mimi nimejibainisha wazi humu kuwa mkweli daima, nitasema kweli no matter what, sasa wasio upenda ukweli, wataona kama namkosoa sana Magufuli, ninakosoa pale ninapoona kuna makosa, lakini pia huwa ninapongeza kwenye mazuri.

Hebu msikilizeni, Mtoto wa Mkulima, anasema nini kumhusu mtu huyu?.

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize
Kauli za Vitisho na Kidikiteta za Rais Magufuli "Hana Ma
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'u

Pasco.
1461860335496.jpg
 
Sitasema tena kuhusu haya! Inaonekana rais anataka watu waseme ili aone wamesema. Mimi siyo mmoja wao!!

Nilishawahi kusema kuwa siyo lazima mtu anayetambua thamani yake kufanya kazi na.........
 
Back
Top Bottom