Utumbuaji Majipu: Inashangaza mpaka sasa alietumia document fake kuzuia uchaguzi hajasimamishwa kazi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Inashangaza sana hii serikali ambayo tunaambiwa imedhamiria kurejesha nidhamu ya watumishi wa umma mpaka sasa haijamsimamisha kazi mtumishi alietumia document isiyostahili(fake) ya Mahakama kuzuia uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar-es-salaam ili nae apishe uchunguzi kama wengine.

Wacha tusubiri lakini nimekumbuka msemo wa Kiswahili usemao: "njia ya muongo ni fupi."
 
Mimi pia nimechoka kuskia kauli za viongozi wa upinzani kila siku tumechoka ,kina Mbowe wamefanya nini juu ya upuuzi wa huyo mama ?? Wameenda mahakamani ? Kutafuta haki ??
 
Hahahahaaaa Mkuu haitawezekana kwa hilo...
Kwan mtumbuaji hauopi mikono yake kuchafuka na uchafu na jibu husika. Hata kama gloves zitavaliwa!
 
Inashangaza sana hii serikali ambayo tunaambiwa imedhamiria kurejesha nidhamu ya watumishi wa umma mpaka sasa haijamsimamisha kazi mtumishi alietumia document isiyostahili(fake) ya Mahakama kuzuia uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar-es-salaam ili nae apishe uchunguzi kama wengine.

Wacha tusubiri lakini nimekumbuka msemo wa Kiswahili usemao: "njia ya muongo ni fupi."
Mkuu naona umesahau usemi usemao kuwa kinyozi kamwe hajinyoi,au ule wa meno ya mbwa hayaumani
 
Mimi pia nimechoka kuskia kauli za viongozi wa upinzani kila siku tumechoka ,kina Mbowe wamefanya nini juu ya upuuzi wa huyo mama ?? Wameenda mahakamani ? Kutafuta haki ??
Mkuu mahakamani kwenyewe utawakuta aina ya majaji ya kina jaji lubuva,hapo ndio utaishiwa nguvu
 
Nchi hii ni Ccm tu ndio wapo juu ya sheria.
Kwanza jiulizeni huyo aliyetangaza kuharishwa kwa uchaguzi kwa kutumia hati feki ya mahakama mbona Ccm wenyewe wapo kimya hawampigii kelele kama wafanyavyo wapinzani?
 
yule mama alitumwa kufanya ule uongo lakini kuna kila dalili kwamba watamtosa , ni aibu sana ofisa wa serikali kutumia nyaraka batili .
 
Mkuu mahakamani kwenyewe utawakuta aina ya majaji ya kina jaji lubuva,hapo ndio utaishiwa nguvu
Na hata hakimu akiamua kutenda haki, anakataliwa na mtuhumiwa, anataka ahukumiwe na amtakae.
 
Back
Top Bottom