Utumbuaji Kanisani: Magufuli ni mkatoliki asiyejua "Roma locuta, causa finita"!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Kwa wakatoliki wengi huu ni msemo maarufu unaojulikana kuasisiwa na Mt. Augustine karne ya tano ukiwa na maana "Roma ikisema kesi imefungwa"
Kwa kutojua hilo jana Magufuli alitoa milioni kumi kusaidia ujenzi kanisani na kuwaonya wazitumie vizuri la sivyo atawatumbua! He! rais wetu unawatisha hata viongozi wako wa dini? Hii haikubaliki hata kidogo.

Fedha alizotoa rais kwa ajili ya ujenzi kesho baba askofu anaweza kuamua zinunue vinanda vya kwaya na rais wetu hana ubavu wa kumuhoji baba askofu kwa nini amefanya hivyo. Sadaka, zaka au matoleo yoyote hayawezi kuhojiwa na muumini yoyote, labda rais akitwambia yeye ni zaidi ya muumini.

Na kama yeye ni zaidi ya muumini mbona anahudhuria, anakomunika, anatubu mbele ya hao anaopiga mkwara kuwatumbua? Rais wetu anatakiwa kujua mkwara anaupiga wapi. Ule haukuwa mkutano wa hadhara, na mbele yake hawakuwepo wakuu wa mikoa au wilaya bali viongozi wake wa kiroho.

Roma locuta, causa finita.

====================

Waziri mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga amesema Rais John Magufuli atakumbana na vikwazo na majaribu mengi katika mapambano dhidi ya ufisadi, rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, hivyo anatakiwa kumtumainia Mungu.

Chato. Waziri mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga amesema Rais John Magufuli atakumbana na vikwazo na majaribu mengi katika mapambano dhidi ya ufisadi, rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, hivyo anatakiwa kumtumainia Mungu.

Akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria mjini Chato jana, Raila ambaye pia ni kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani wa Cord, alifananisha majaribu atakayokutana nayo Rais Magufuli kuwa ni sawa na yaliyompata Yesu Kristo, ambaye licha ya kupingwa na watu wake, pia alijaribiwa mlimani na shetani.

“Unatakiwa kusimama imara na kumtumaini Mungu kwa sababu utakumbana na majaribu mengi kama aliyoyapata Yesu Kristo akiwa mlimani alipojaribiwa na shetani,” alisema Raila.

Kiongozi huyo aliyeambatana na mkewe Ida na binti yao, Winnie Odinga wako Chato tangu juzi baada ya kuwasili kwa chopa wakiwa wageni wa familia ya Rais Magufuli aliyeko mapunzikoni.

Huku akimuangalia Rais Magufuli ambaye pia alihudhuria misa hiyo pamoja na mkewe Janeth, Raila alisema: “Jambo muhimu na la msingi nakusihi usimamie ukweli na haki katika utendaji wako.”

Ushirikiano EAC na utanzania wake

Akizungumzia ushirikiano katika ukanda wa Afrika Mashariki, Raila alisema umejengwa katika misingi ya utu, undugu na historia ya mataifa hayo kabla na baada ya ukombozi, akitolea mfano wake yeye alivyotumia hati ya kusafiria ya Tanzania kwa miaka mitatu baada ya Serikali ya kikoloni kumnyima hati ya Kenya.

“Mwalimu Julius Nyerere alijitoa mhanga kupigania uhuru wa mataifa mengine ya Afrika ikiwamo Kenya, natamani kuona umoja wa Afrika Mashariki ukiimarika kutimiza ndoto ya waasisi wa nchi hizi waliopigania uhuru na kuimarisha umoja wao,” alisema Raila.

Alisema bado anakumbuka urafiki wa kweli kati ya baba yake , marehemu Mzee Oginga Odinga na Mwalimu Nyerere aliosema unamfanya kujihisi Mtanzania, licha ya kuwa raia wa Kenya.

Urafiki wake na Magufuli

Kuhusu urafiki wake na Rais Magufuli, kiongozi huyo wa upinzani nchini Kenya alisema: “Urafiki wetu ulianza tangu Mheshimiwa Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi na mimi nikiwa na wadhifa huo nchini Kenya ambapo tulibadilishana uzoefu na kushirikiana katika mipango na miradi ya ujenzi wa barabara.”

Magufuli achanga Sh10 milioni, atishia kutumbua jipu

Rais Magufuli aliwataka Watanzania wote kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Taifa lao huku wakiepuka ubaguzi wa aina yoyote miongoni mwao.

“Tuongozwe na mioyo ya mshikamano, upendo na ushirikiano huku tukimtanguliza Mungu kwenye kila jambo; tuepuke kubaguana kidini, kikabila wala kiitikadi huku tukiliombea Taifa letu liendelee kudumu kwenye amani, utulivu na mshikamano,” alisema Rais Magufuli

Rais alichangia Sh10 milioni kusaidia upanuzi wa kanisa hilo linalokaribia kusherehekea miaka 50 tangu lijengwe, huku akiutaka uongozi kutumia vema mchango huo akitishia kutumbua majipu iwapo atafuatilia na kubaini matumizi mabaya ya fedha hizo.

“Baba Paroko, nachangia Sh10 milioni kwenye ujenzi wa kanisa, lakini mzitumie vizuri nisije nikawatumbua nitakapofuatilia matumizi yake,” alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa na waumini.

Kama alivyosema Raila, Rais Magufuli alisema urafiki wao umevuka viwango vya urafiki na kufikia undugu na kubainisha siyo mara ya kwanza wao kutembeleana kifamilia.

“Hata kwenye msiba wa marehemu baba yangu, Raila alikuja na kukaa Chato siku mbili, huyu ni rafiki wa kweli na tumesaidiana katika mambo mengi, naomba wana Chato mmtambue kama mtoto wa Chato,” alisema Rais Magufuli, ambaye mwishoni mwa wiki alitangaza mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni.

Chanzo: Mwananchi
 
Bila shaka wewe ndio haufahamu utaratibu wa uendeshaji wa kanisa. Mchango unaotolewa kwa sababu fulani unaweza kuhojiwa na mtoaji wa mchango kama ulitekeleza kile alichochangia, na kimsingi kama muumini anaweza kutumbua uongozi wa kanisa kupitia Baraza na Walei parokia. Kisichoweza kuamuliwa na muumini ni sadaka anayoitoa kwa siri, tena kimsingi yeye kama Muumini ana haki ya kufahamu matumizi yake na ndio maana kuna kitu kinaitwa Baraza la Walei katika parokia zote, lengo hasa wa baraza hili ni kusimamia rasilimali za parokia kwa niaba ya waumini.
 
Kwa kutojua hilo jana Magufuli alitoa milioni kumi kusaidia ujenzi kanisani na kuwaonya wazitumie vizuri la sivyo atawatumbua! He! rais wetu unawatisha hata viongozi wako wa dini? Hii haikubaliki hata kidogo.

Kanisani kumeharibika pia ana haki ya kusema hivyo kwani aweza toa pesa hizo halafu kiongozi wa dini akaenda zitumia kwa ngono angalia kama huyu padri aliyefumaniwa unafikiri pesa aliyotumia alitoa wapi? Kama sio sadaka kama za Magufuli zilizotumika vibaya ona hapa

Padri Anatoly Salawa afumaniwa akifanya ngono ndani ya gari
 
Bila shaka wewe ndio haufahamu utaratibu wa uendeshaji wa kanisa. Mchango unaotolewa kwa sababu fulani unaweza kuhojiwa na mtoaji wa mchango kama ulitekeleza kile alichochangia, na kimsingi kama muumini anaweza kutumbua uongozi wa kanisa kupitia Baraza na Walei parokia. Kisichoweza kuamuliwa na muumini ni sadaka anayoitoa kwa siri, tena kimsingi yeye kama Muumini ana haki ya kufahamu matumizi yake na ndio maana kuna kitu kinaitwa Baraza la Walei katika parokia zote, lengo hasa wa baraza hili ni kusimamia rasilimali za parokia kwa niaba ya waumini.
Aliyowapiga mkwara siyo walei na pale wala asingejua mlei ni nani. Mbele yake alikuwepo paroko na haikuwa sahihi kumwambia kiongozi wake wa kiroho namna ile
 
Kwa wakatoriki wengi huu ni msemo maarufu unaojulikana kuasisiwa na Mt. Augustine karne ya tano ukiwa na maana "Roma ikisema kesi imefungwa"

Kwa kutojua hilo jana Magufuli alitoa milioni kumi kusaidia ujenzi kanisani na kuwaonya wazitumie vizuri la sivyo atawatumbua! He! rais wetu unawatisha hata viongozi wako wa dini? Hii haikubaliki hata kidogo.

Fedha alizotoa rais kwa ajili ya ujenzi kesho baba askofu anaweza kuamua zinunue vinanda vya kwaya na rais wetu hana ubavu wa kumuhoji baba askofu kwa nini amefanya hivyo. Sadaka, zaka au matoleo yoyote hayawezi kuhojiwa na muumini yoyote, labda rais akitwambia yeye ni zaidi ya muumini.

Na kama yeye ni zaidi ya muumini mbona anahudhuria, anakomunika, anatubu mbele ya hao anaopiga mkwara kuwatumbua? Rais wetu anatakiwa kujua mkwara anaupiga wapi. Ule haukuwa mkutano wa hadhara, na mbele yake hawakuwepo wakuu wa mikoa au wilaya bali viongozi wake wa kiroho.

Roma locuta, causa finita.
Wewe utakuwa mkatoliki wa Misri
 
Usitake kuturudisha kwenye ugomvi wa Papa Boniface wa 8 na Mfalme Philipo wa 4 mwaka 1320. Ambapo wawili hawa walisumbuana sana kila mmoja akijigamba kuwa yeye ni mkuu kuliko mwingine.
Yani kanisa na Serikali.
 
Magufuli hajui misemo mingi tu ya kikatoliki, na hajui taratibu nyingi tu za kikatoliki, ila tunamsamehe
 
Usitake kuturudisha kwenye ugomvi wa Papa Boniface wa 8 na Mfalme Philipo wa 4 mwaka 1320. Ambapo wawili hawa walisumbuana sana kila mmoja akijigamba kuwa yeye ni mkuu kuliko mwingine.
Yani kanisa na Serikali.
Ya kaisari unampa Kaisari na ya Mungu unampa Mungu. Hata Magufuli hizo mil 10 angechangia madawati lakini akazitoa sadaka
 
Kwa wakatoliki wengi huu ni msemo maarufu unaojulikana kuasisiwa na Mt. Augustine karne ya tano ukiwa na maana "Roma ikisema kesi imefungwa"

Kwa kutojua hilo jana Magufuli alitoa milioni kumi kusaidia ujenzi kanisani na kuwaonya wazitumie vizuri la sivyo atawatumbua! He! rais wetu unawatisha hata viongozi wako wa dini? Hii haikubaliki hata kidogo.

Fedha alizotoa rais kwa ajili ya ujenzi kesho baba askofu anaweza kuamua zinunue vinanda vya kwaya na rais wetu hana ubavu wa kumuhoji baba askofu kwa nini amefanya hivyo. Sadaka, zaka au matoleo yoyote hayawezi kuhojiwa na muumini yoyote, labda rais akitwambia yeye ni zaidi ya muumini.

Na kama yeye ni zaidi ya muumini mbona anahudhuria, anakomunika, anatubu mbele ya hao anaopiga mkwara kuwatumbua? Rais wetu anatakiwa kujua mkwara anaupiga wapi. Ule haukuwa mkutano wa hadhara, na mbele yake hawakuwepo wakuu wa mikoa au wilaya bali viongozi wake wa kiroho.

Roma locuta, causa finita.
Kichaa kapewa rungu
 
Bila shaka wewe ndio haufahamu utaratibu wa uendeshaji wa kanisa. Mchango unaotolewa kwa sababu fulani unaweza kuhojiwa na mtoaji wa mchango kama ulitekeleza kile alichochangia, na kimsingi kama muumini anaweza kutumbua uongozi wa kanisa kupitia Baraza na Walei parokia. Kisichoweza kuamuliwa na muumini ni sadaka anayoitoa kwa siri, tena kimsingi yeye kama Muumini ana haki ya kufahamu matumizi yake na ndio maana kuna kitu kinaitwa Baraza la Walei katika parokia zote, lengo hasa wa baraza hili ni kusimamia rasilimali za parokia kwa niaba ya waumini.

Na wewe unajua kukalili tu haujui vizuri, kwanza tambua kanisa Catholic linaongozwa kwa kauli mbiu ya UTII NA UNYENYEKEVU. Hilo ni la kwanza, pili Baraza la walei linasimamia Rasilimali kama ulivyotangulia kusema ila sio michango wala sadaka na hata zaka, kama wangekuwa wanasimamia hayo, hayo niliyoyataja wangekuwa wanayashikilia basi Magufuri angewakabidhi huo mchango, Sasa kwa taarifa yako Mabaraza au Halmashauri za walei zipo lakini kitu kinachoitwa fedha yoyote ndani ya parokia mwenye mamlaka ya mwisho ni Paroko husika hata hizo rasilimali zinazosimamiwa na Hayo mabaraza iwapo ni vitega uchumi mapato yake hutunzwa kwenye akaunti ya parokia lakini mwisho namna ya kuyatumia ni lazima paroko ajiridhishe na aidhinishe utoaji wa fedha hitajika. Hivyo pesa ya Magufuri kama kaikabidhi kwa Paroko yeye aombe paroko awe mpenda maendeleo na asiyependa kujinufaisha kwani siku hizi baadhi ya mapadre wameingia kwenye huo utume kwa maslahi yao binafsi sio kwa wito halisi.

NB: Magufuri hana wa kumuwajibisha hata hayo mabaraza na H/walei hawana uwezo wa kumuwajibisha Padre yeyote labda wasubiri akijiondoa kwenye daraja la upadre. Padre anawajibishwa na Askofu wake wa jimbo husika na Askofu anawajibishwa na Papa sio vinginevyo maybe ziwe porojo za kisiasa na ambapo hazina mashiko kwa kanisa.
 
Kwa wakatoliki wengi huu ni msemo maarufu unaojulikana kuasisiwa na Mt. Augustine karne ya tano ukiwa na maana "Roma ikisema kesi imefungwa"

Kwa kutojua hilo jana Magufuli alitoa milioni kumi kusaidia ujenzi kanisani na kuwaonya wazitumie vizuri la sivyo atawatumbua! He! rais wetu unawatisha hata viongozi wako wa dini? Hii haikubaliki hata kidogo.

Fedha alizotoa rais kwa ajili ya ujenzi kesho baba askofu anaweza kuamua zinunue vinanda vya kwaya na rais wetu hana ubavu wa kumuhoji baba askofu kwa nini amefanya hivyo. Sadaka, zaka au matoleo yoyote hayawezi kuhojiwa na muumini yoyote, labda rais akitwambia yeye ni zaidi ya muumini.

Na kama yeye ni zaidi ya muumini mbona anahudhuria, anakomunika, anatubu mbele ya hao anaopiga mkwara kuwatumbua? Rais wetu anatakiwa kujua mkwara anaupiga wapi. Ule haukuwa mkutano wa hadhara, na mbele yake hawakuwepo wakuu wa mikoa au wilaya bali viongozi wake wa kiroho.

Roma locuta, causa finita.

wewe si mkatoliki na kama mkatoliki ungejua fedha za ujenzi zinasimamiwa na kamati ya ujenzi na padri akipiga hata miamoja msala wake ni balaa. Kuna mgogolo Mkanisa mengi sana niliona kanisa la ulongoni Padri alibanwa kwa kula pesa ya Milango
 
Back
Top Bottom