Utulivu wa Kisiasa: Mafanikio kuelekea siku 365 za Rais Samia Suluhu Hassan

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
KUELEKEA SIKU 365 ZA MHE SAMIA, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Na Elius Ndabila
0768238284

1: UTULIVU WA KISIASA
Itakumbukwa kuwa bado siku chache kwa Mhe Samia, Rais wa awamu ya sita kumaliza mwaka mmoja tangu alipoapishwa kuwa Rais. Kuelekea siku 365 nitakuletea mfululizo wa makala mbalimbali. Leo nitaanza upande wa siasa kwa ujumla. Siasa ndiyo inayobeba maisha ya watu na maendeleo ya nchi.

Itakumbukwa Rais Samia aliapishwa kuwa Rais mara baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli baada ya kufariki tarehe 17/3/2021.

Itakumbukwa kuwa baada ya Mhe Samia kuapishwa alikiri kuwa kazi yake kubwa atakayoanza nayo ni kufungua nchi. Kufungua nchi kwa mkutadha wa nadharia ya kichambuzi ina dhana pana sana. Kubwa hakumaanisha kama nchi ilikuwa imefungwa na minyororo au makufuli bali aliamini kurejesha hali ya diplomasia ya kimataifa ambayo ilikuwa imeanza kuteteleka.

Ikumbukwe kuwa huwezi kutengeneza diplomasia ya kimataifa kama ndani hujatengeneza. Lazima ndani kuwe na lugha moja ndipo unaweza kwenda kutengeneza nje. Msingi wa utawala bora wa ndani unategemea sana UTANGAMANO WA KISIASA. Siasa zilizotulia ndizo zinazoweza kuleta utengamanifu. Duniani kote, vita vya ndani ya nchi havisababishwi na serikali bali husababishwa na mfumo dhaifu wa kisiasa unaokosa masikilizano.

Rais Samia aliingia uongozini nchi ikiwa kwenye taharuki. Aliingia kipindi ambacho kama Taifa halijawahi kukipitia. Utulivu wake wa akili, ushupavu wake, Uhodari wake na Umahiri wake ndio uliweza kulivusha taifa ktka kipindi hicho kigumu.

Mhe Samia alisimama kama Mwenyekiti wa CCM na wakati huo huo alisimama kama Rais wa nchi Hivyo kazi moja kubwa aliyokuwa nayo Samia akiwa amevalia nafasi ya Uwenyekiti wa CCM ni kuteua viongozi wakuu wa Chama ambao wangemsaidia kuleta utengamanifu ndani ya chama. Hilo zoezi amefanikiwa Kwa kiasi kikubwa na Kwa ufanisi mkubwa. Hata hivyo akivalia joho la Urais kwa kipindi cha kuelekea mwaka mmoja yeye anetumika kama mfariji mkuu wa vyama vyote. Hakuna alitegemea tutavuka salama kipindi hicho.

Ili kuleta utulivu huu, Mhe Samia kwa nyakati tofauti amekutana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa. Amekutana karibu na viongozi wa vyama vyote. Tafsiri yake kukutana na viongozi wa vyama ni kuonyesha kufungua nchi ndani. Ukishafungua nchi ndani hasa kisiasa inassidia na kupunguza gharama za kuifungua nchi nje kwani kama Taifa mnakuwa na lugha moja.

Ukweli ni kwamba Tanzania tunazihitaji zaidi nchi kubwa duniani kuliko wao wanavyotuhitaji.Lakini ili uhitaji huo uwe sanifu umoja wa kitaifa ni mhimu kuliko kitu chochote. Ili kufikia maendeleo endelevu tunahitaji kujenga mahusiano makubwa na nchi kubwa. Mgogoro uliokuwepo kati ya viongozi wa CHADEMA na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ulichochea Kwa kiasi kikubwa kumomonyoa mahusiano ya Tanzania miongoni mwa nchi zingine Duniani.

Rais Samia amekuwa dakitari mkuu kutibu tofauti hizo. Katika kuelekea kuhitimisha mwaka wake WA kwanza ameshakutana na aliyekuwa mgombea Urais wa Chadema Wakili Tundu Antipas Mughwai Lisu na pia amekutana na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Aikael Mbowe. Kote huko ni kijaribu kuiunganisha nchi kisiasa na kuzifanya siasa kuwa utani wa jadi kama ilivyo Kwa mpira na si uhasama na ubabe.

Utulivu huu wa kisiasa ambao ndio tunu ya umoja na utaifa wetu umeondoa Kwa kiasi kikubwa kundi la watu wasiojikana ambao kuna wakati walishika hatamu kwenye taifa hili.

Mhe Samia kama mwenyekiti wa CCM ndani ya mwaka mmoja amefanikiwa kukituliza Chama Cha Mapinduzi. Itakumbukwa kuwa chini ya Mtendaji Mkuu wa Ndg Chongolo CCM hakijawa tena Chama Cha Matamko na kutisha bali kimekuwa chama Cham kusimamia katiba na miongozo waliyojiwekea. Chongolo amekuwa ni mfariji/comforter mkuu.

Hivyo tunapomuangazia Mhe Samia kwa kipindi chake cha kuelekea mwaka mmoja tunamtazama kama kiongozi shujaa na jasili ambaye hataki kuona kama siasa inaaeza kutugawa.

Rais Samia ni kiongozi ambaye ameonyesha kuwa siasa inaweza kuleta utani na si uhasama na Vita. Samia ukimtazama ni mtu ambaye anaamini maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wote endapo tu wataamini kuwa siasa si kufa na kupona. Mazungumzo yake na Mbowe ni dalili tosha kuwa waliafikiana mambo makubwa kwa masilahi ya Taifa.

Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema siasa safi ndiyo chachu yamaendeleo. Kwa mkutadha huo huwezi kufungua nchi kwenye nyanja ya kimataifa kama ndani kuna vita vya nafsi na kutokuelewana. Kama taifa inatakiwa kuwa na kugha moja mnapotoka nje. Huwezi kupata maendeleo kama serikali inaongea hivi na vyama vingine vinaongea tofauti unapotoka nje.

Rais Samia ameupiga mwingi kisiasa. Kuna utulivu mkubwa. Ninaamini atakapoanza mwaka wa pili ataendelea kuboresha yale ambayo bado hayajapata suluhu kwa mwaka mmoja.

Mwisho, hizi tofauti za kisiasa zinazoondolewa kwa ngazi ya kitaifa, sasa sisi wa huku chini tuna wajibu wa ku adopt. Tuendelee kutanguliza Taifa kuliko vyama vyetu vya kisiasa.
 
Hakuna Mabaya aliyofanya?

Kama mchambuzi inabidi uelezee pro and cons, (inaongeza authenticity ya uchambuzi) unless otherwise unakuwa mpiga propaganda; Kama hivyo ndivyo basi sawa.
 
Back
Top Bottom