Utu wema na upendo huanza kwa rafiki au ndugu wa karibu

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,375
12,566
Huu ni ushauri kulingana na mtazamo wangu.

Katika hili swali watu walio wengi hukosea pasipo kufahamu nini hasa hasara zake. Binadamu wengi sisi sio wakamilifu sana wala sio watenda mema sana, lakini pale tunapo guswa huwa tunajaribu kujitoa kwa hali na mali.

Utakuta mtu anawahi kushikwa na roho ya huruma kumsaidi mtu asie mfahamu kabisa endapo atadai kuwa anashida pasipo kujua mwenendo au matendo ya mtu huyo, si jambo baya ni jambo zuri kabisa.

Lakini lengo la uzi huu ni kukumbusha kua.. sisi sote sio wakamilifu tunatakiwa pia kuwa na utu wema na roho ya kujali kwa mtu unae mfahamu, bila kujali tabia zake au level yake ya maisha.

Kwani siku wew ukipatwa na shida huta chukua uamuzi wa kuwa ombaomba (begger) utamfata yule ambae unamfahamu, na pengine hata pasipo wewe kumuomba anaweza kurudisha fadhila kwa njia yoyote ile endapo uliwahi kumsaidia, kama ni jirani yako au ndugu yako.

Katika kuchunguza kwangu ninaona kwamba huko kukosea kunasababishwa naa..

Watu wengi tunaona endapo tutamsaidia mtu asie tufahamu hasa kitabia, ni kwamba unaona mtu huyo atakuvika taji la wema kwa asilimia mia moja na kukushukuru sana,

Na pengine tunadhani usie mjua ndie mala nyingi Mungu anataka umsaidie lakini hapana..
Na wengine hudiliki kumthamini mtu kutokana na Muonekano wake, ukadhani huyu nikimpa huduma vizur atanisifia na kuniona na mim niwamaana sana.

Alafu unae fahamiana nae au kulingana nae level fulani ya maisha unamuona kama msumbufu, au kaja kukuchora, pengine unamuona kwamba hato shukuru ipasavyo, lakini tusisahau ya kwamba unae mfahamu ni wamaana pia sana kwako.

Ujumbe wangu ndio huo... Anae kufahamu wakati mwingine anaweza kuona wew ni wathamani sana kwani sisi sote sio wakamilifu sana, kuliko asie kufahamu wakati mwingine hato ona maana yoyote kwako.

Anae kujua unavyo pambana, siku yeye akiwa juu, atatamani akuvute mkuno na wew ufike juu kwani anatambua kiu yako na upambanaji wako.

Sipingi wema kwa mtu usie mjua, lakin nakumbusha tuthaminiane sisi tunao fahamiana kwa kiasi zaidi hata kama rafik yako ni mmbea, au snich au pengine yeye vyakake unaona anakua mchoyo, huwezi jua leo na kesho bado wew kwake unaweza kua wa maana kwani mliishi kucheka wote na wakati mwingine kutembea pamoja.
 
Kama unatenda wema ili ufaidike kwa namna yo yote ile huo siyo wema.

Kama unasaidia ili ufaidike kwa namna yo yote ile, huo siyo msaada. Ni ego yako tu imekusukuma kufanya hivyo. Sawa na macelebrity tunaowaona wanapeleka gunia moja la mchele na debe la mafuta lakini wanakwenda na makamera yao. Wajulikane kuwa wametoa. Huo, kimsingi, siyo msaada.

Msaada halisi ni ule unaotoa bila kutegemea cho chote. Na wema halisi wa mtu hupimwa kwa jinsi anavyowatendea wale ambao hawawezi kumlipa cho chote. Ukitaka kuijua tabia halisi ya mtu, mwangalie anavyowatendea wasio na uwezo wa kumlipa cho chote.

Hata Maandiko yameweka mibaraka zaidi kwa misaada na mema tunayowatendea watu tusiotegemea cho chote kutoka kwao kuliko ndugu na marafiki. Ndiyo. Saidia ndugu na marafiki zako lakini mibaraka na furaha ya kweli hasa imejificha katika kusaidia watu wasiokufahamu na usiotegemea cho chote kutoka kwao - watoto mayatima, wagonjwa mahospitalini, omba omba mtaani na wote wenye uhitaji wa kweli.

20200618_105922.jpg

Na kwa uzoefu wangu, ndugu wengi ambao nimeshajaribu kuwasaidia, leo wamegeuka kuwa maadui wakubwa. Wao wanataka uwasaidie tena na tena na siku ukisema kuwa huwezi basi unageuka adui. Na siku wewe ukikwama na kuomba msaada kwao wengi hutawaona. Na siku hizi upendo wa wengi umepoa - hata kama ni ndugu wa tumbo moja. Ni minyukano tu kwenda mbele....
 
Mtoa mada bado hujakutana na manyanyaso ya ndugu na marafiki snitch, Saidia yeyote kwa kumuhofia Mungu maana naye atakuletea wa kukusaidia bila ya wewe kumfahamu.
 
View attachment 1482589

wewe ukiokoka, si vyema umvute kwenye wokuvu na nduguyo?
Ukimpenda ndugu yako au rafik ukiwa na Yesu, unaweza kumshawishi nae aweze kumjua Yesu.
 
Mtoa mada bado hujakutana na manyanyaso ya ndugu na marafiki snitch, Saidia yeyote kwa kumuhofia Mungu maana naye atakuletea wa kukusaidia bila ya wewe kumfahamu.
Ninae mjua lazima nimpe first priority, kuangaika na usie mjua unaweza angaikia hata jini.
 
wewe ukiokoka, si vyema umvute kwenye wokuvu na nduguyo?
Ukimpenda ndugu yako au rafik ukiwa na Yesu, unaweza kumshawishi nae aweze kumjua Yesu.
Sio kila ukisaidia unafikiria kuwa na wew uje unufaike kitu kwa huyo mtu, wengi tunatageti baraka kutoka kwa Mungu.

Lakini Kwanini mtu wa karibu akose thamani, na kumthamini usie mjua?
Nahakika ukiwa na Yesu ndani yako, rafik na ndugu utawaona wamaana sana siku zote bila kujali tabia zao.
Kumbe we umeokoka mkuu? Ningejua tangu mwanzo wala nisingehangaika kuweka comment yangu. Kwa kawaida huwa siendeshi mijadala na walokole. Huwa haifiki po pote
 
Kumbe we umeokoka mkuu? Ningejua tangu mwanzo wala nisingehangaika kuweka comment yangu. Kwa kawaida huwa siendeshi mijadala na walokole. Huwa haifiki po pote
Ni sawa.
But nimesema hayo baaada ya wew kuwa wakwanza kutumia vifungu vya biblia.
It means unaamin maandiko ya bible.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom