Utotoni nilihisi nateswa na kunyimwa haki ya Kucheza

6321

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
649
1,116
Nawasalimu kwa JMT.

Leo na share maisha yangu ya utotoni, kwa akili za utoton nilihis nateswa na wazazi lakin kuna kitu wamekipanda akilin mwangu.

Enzi za utoto nikiwa primary had High school, nyumbani sikuwah kupewa nafasi ya kucheza kama watoto wengine, route za kwenda kutembea sikuwah kupewa hiyo nafasi. Likizo kwangu ilikuwa chungu mno. Yan nilikuwa nikisikia tunafunga shule nakosa amani, huzuni ina niandama.

Maisha yalikuwa hiv; Nikitoka shule basi nitaambiwa nikakae dukani unaweza kuta nakaa dukan had saa 6 usiku, nifundishwe kufunga hesabu, yanionyweshwe madaftari yawatu wanaochukua order za bidhaa. Weekend ilikuwa mbaya zaid naenda kufungua duka saa 12 asubuh nashinda dukani had 6 usiku.

Kwa kipind kile maisha siku ya furahia, sababu sikuwa na nafasi ya kuwa huru kucheza na kuzurula. Nakumbuka kusambaza cretes za bia na pakti za sigara madukani. Unatembea jua lako mvua yako. Maisha yaliendelea hivyo had 2016 nilipoenda University kidogo majuku yakapoa. Nikawa narudi home usiku jmoc, j2 mapema tu saa 8 mchana naenda chuo nakimbia kaz za dukani.

Lakin kwenye miaka yote hiyo nilijifunza mengi, moja ya nilichojifunza kutoka kwa wazazi wangu ni usimamizi mzuri wa kile kidogo ulichonacho, Ubahiri pia nilijifunza maana kipind nasambaza bidhaa kwenye maduka ya rejareja nilikuwa nabania 100 100 au 200 200 lakin wazee walikuwa wananikaba had kunisachi mifukon.

2019 nilimaliza Degree ya kwanza, nikarudi dukani kama kawaida nilifanya kazi kama miez 3 hiv, yan fulltime nikawa incharge. 2020 kipind kama hiki maandalizi ya x-mass. Wazee wakakniita wakaniambia sasa umekua hatutaki utuombe hela, wala chakula hapa kwetu sema unataka nini?.
Mimi: Nilichowajibu biashara wanifungulie.
Mzee: Hatukufungulii tunakukopesha hela
Mimi:Kinywa
Wazee walinikopesha hela kukiwa na mashahidi, nirudishe ndani ya miaka 2, sasa hiv ndio kwa mwaka lakin mambo ni , nikamuomba nianze kumlipa akasema acha nenda kanunue kiwanja kikae hapo.

Leo hii ndio nimeamin sikuwa nateswa wala kunyimwa haki ya kucheza bali nilikuwa napikwa, na kwenye swala la ubahir na kujua pesa nimepikika kweli kweli.


Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom