Utoto bwana,Leo nikikumbuka "najiskia tu kumuomba Mungu Anisamehe"

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,931
22,901
Hamna kitu kilichokua kikinikera kama mwalimu kuja kutuuzia vitumbua darasani au unakuta mwalimu anakuja na ubuyu wake katengeneza kwake anauza darasani nilikua sipendii tena nilikuaga mnoko nikiitwa ofisini kwa head master kuwataja walimu wauza ubuyu

LEO HII NDIO naelewa maskini mimi kumbe maisha ndio haya daaah, eeeh baba nisamehe mimi maana nilikua sijui nilitendalo...kumbe ndio yana ladha hiii eeeh aseee baba ulie juu naomba nirehemu "nisamehe mja wako" Nilikosea sana.

Kosa nililokua naona wanalifanya walimu enzi hizo nina uhakika asilimia 500 Leo hiii paaap nikiambiwa kawe mwalimu. Marufuku kufanya hivyo unavyofanya sasa hivi kukuingizia kipato, Yaani nasema hiviiiiiiiiiiiiii.....Nitakua nikienda kazini nitaenda na
  • Ndoo 1 ya karanga,
  • Ndoo 1 ya Ubuyu,
  • Ndoo 1 ya Vitumbua,
  • Ndoo 1 ya kachori na
  • Ndooo 1 ya Biskuti za sh 100

Na OLE wake niskie katoto ka mtu kameleta ule unoko niliokuaga nao enzi zangu. Hakika nita katengua shingo sio siri.... Maisha haya "ebu kila mtu atubu dhambi zake" maaana kuna wengine walisemaga. Mimi huyu mimi niuze pombe mimi!!! leo hii anauza konyagi ya kupima

Mimi huyu nichezeshe pool table mimi, nishinde kwenye Pool table he he heeeeee! leo hiii ndio kazini kwake. Mimi huyu niwe mama ntilie mimi khaaaa! leo hiii anaulizia Mtaji wa kufungua mama ntilie sh ngapi. Msicheke mjue ebu tubuni dhambi zenu,Tukubali sote tu wakosaji.

Baba wabariki walimu huko mashuleni wanafunzi wanunue vile vitumbua viishe. Baba wabariki wale walimu ubuyu wao uishe. Baba wabariki mama ntilie vyakula vyao viishe. Baba bariki kila raia anaetafuta shilingi yake BARIKI BARIKI BARIKI. Namwaga mau pakooooooooo wanafunzi nunueni ubuyuuuuuu, kuleni mandazi eeeh baba wape njaa wale watoto, wanunue zile pipi ziiishe, wape njaaa wale watoto wanunue zile kachori ziiishe...

na sote tuseme AMEEEEEEEN.
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom