Utoroshaji mabilioni ya shilingi Uswisi Mwinyi na Mkapa watanusurika?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3][/h]

thumbnail.aspx

Kwa wanaojua jinsi marais Ali Hassan Mwinyi (mzee Ruksa) na Benjamin Mkapa (Mjasiriamali) walivyoendesha Tanzania, hana wasi wasi kuwa kati ya vigogo sita wanaodaiwa kuficha jumla ya Dola za Kimarekani, 196.8 nchini Uswisi watakuwamo. Chini ya dhana ya ruksa, Mwinyi, kwa kuwatumia baadhi ya waarabu na wahindi marafiki zake, alichota pesa nyingi ingawa huwa hatajwi. Nani mara hii kasahau kashfa kama vile IPTL iliyoingizwa nchini na mawaziri wake Profesa Kighoma Malima na Jakaya Kikwete ukiachia mbali wengine? Nani hakumbuki kashfa ya watu waliokuwa karibu na mke wa Mwinyi kupata vimemo vya kununulia madala dala na viwanja na upuuzi mwingi. Kuhusu Mkapa kila mtu anajua jinsi alivyokwapua pesa ya umma kuanzia wizi wa EPA hadi kujimilkisha machimbo ya makaa ya mawe ya Kiwira. Je kwa mtaji huu wawili hawa hata huyu aliyepo madarakani watanusurika na kashfa hii?
 
in short hawahusiki,hii thread yako imekaa kiuongo mno,haraka zako za nini wakati takukuru wameshaanza uchunguzi,be patient buana,
 
Serikali DHAIFU haiwezi kuwagusa hata kama wanahusika maana kwa wizi wa Kiwira Mkapa na madudu mengine aliyoyafanya sasa hivi alikuwa anatakiwa kuwa lupango.
 
Wanaweza kabisa wakawa wanahusika, lakini kwa serikali hii dhaifu unategemea watafanywaje kama wameshindwa kutekeleza hata azimio la bunge kuhusu Jairo? Halafu Mibunge ya CCM pamoja na kutuharibibia TV zetu kwa mimate yao siku ile inatokwa povu kuhusu Jairo, bado inathubutu kusimama na kusifu "serikali sikivu"!
 
Back
Top Bottom