DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,472
Inashangaza sana kuona mtu anakaa kudai eti Yanga imeshinda kwa ubora. Ukweli ni kwamba kuna mambo ya ndani kwa ndani huko Simba yanayopelekea kupigisha timu shoti na hata mgomo baridi wa wachezaji.
Turudi mechi ya nusu fainali dhidi ya Singida. Hivi unahitaji akili kubwa kiasi gani kujua Simba haikutaka kushinda ile mechi? Waliona chaka la uchovu lipo wakaamua kulitumia ila hiyo siyo sababu ya kweli.
Njoo mechi ya mwisho dhidi ya Kagera. Ile mechi ni bahati mbaya tu au kukosa umakini kwa wachezaji wa Kagera ila mipango ilikuwa iishe sare. Hili nalo kwa waliotazama mechi hauhitaji akili kubwa sana kulitambua.
Tuje sakata zima la derby. Ukweli ni kwamba Simba ilikimbia derby ya 08/03. Sababu kubwa ni kuogopa kufungwa kungeharibu morali ya timu katika mashindano ya CAF na Yanga angeweza kutangaza ubingwa mapema sana. Sababu hiyo ikakutana na sababu za kisiasa na pande hizi mbili zilipoungana kila mmoja akimtegemea mwenzake ndiyo kikapelekea kile kilichotokea.
Ukija mechi yenyewe ya jana. Baada ya kushindwa kupata sare katika mechi ya Kagera, jana hauhitaji akili kubwa kujua Simba hakuingia kwa hamu na shauku ya kutafuta ushindi. Tuweke mihemko pembeni, tuangalie kile kilichokuwa kinafanyika uwanjani toka kipindi cha kwanza, sub za Simba zilizofanyika, magoli yaliyofungwa, nk. utagundua mazingira yalitengenezwa na Simba wenyewe wasishinde ile mechi.
Wenyewe wanajua nini kinasababisha haya yote.