Utofauti wa mawazo ya masikini na tajiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utofauti wa mawazo ya masikini na tajiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by eRRy, Oct 24, 2009.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  :confused:


  Ni kweli usiopingika kuwa mawazo na fikra zako ndizo zinazokufanya uwe mtu wa aina fulani. Ukiwaza kama tajiri bila shaka na wewe utakuwa tajiri, ukiwaza kama maskinii utakuwa tu maskini na ukiwaza kama mtu wa kawaida utakuwa hivyo hivyo.

  Zifuatazo ni tofauti sita zinazoonyesha jinsi matajiri, wenye uwezo wa kati na watu maskini wanavyotofautiana kimawazo na kifikra. Ni muhimu kuzingatia kuwa baada ya kuzitambua tofauti za kimawazo, utakuwa na nafasi ya kuchagua uwe nani maishani mwako, tajiri au maskini.

  1: MATAJIRI HUWAZA NA KUFIKIRI KUWA “MAISHA YANGU YANATENGENEZWA NA MIMI MWENYEWE”
  Watu maskini huwaza na kufikiri kuwa “maisha yanatokea yenyewe tu” Kama unataka kuwa tajiri lazima ufahamu kuwa jukumu la kuyabadilisha na kuyaendesha maisha yako liko mikononi mwako wewe mwenyewe.

  Hakuna aliyeumbwa kuja kukupa maisha bora. Maisha ni yako na wewe ndiye unayeamua yaweje. Ukitaka kufanikiwa lazima utambue kuwa wewe ndiyo umeshikilia usukani, na ni wewe ndiye unayechagua uyapeleke wapi maisha yako hususan katika mafanikio na hali ya kiuchumi.

  Kama unaamini tofauti na hivi, basi una mawazo ya kimaskini na itakuwa vigumu sana kwako kufanikiwa na kuyamudu maisha yako. Badili namna unavyofikiri kuhusu maisha na bila shaka ukifikiri kama tajiri utakuwa tajiri tu.

  Watu wenye fikra za kimaskini hujikuta wakiwa wahanga wa maisha, wakiendeshwa na wengine na mwisho huendelea kuwa mafukara katika siku zote. Anza kuamini kuwa hakuna aliyezaliwa akiwa maskini wala tajiri. Ni wewe ndiye unayechagua uwe nani hapa duniani.

  2: MATAJIRI HUCHEZA MICHEZO YA PESA WAKIWA NA UHAKIKA WA KUSHINDA NA KUONGEZA KIPATO
  Watu maskini hucheza michezo ya pesa wakiwa na uhakika wa kushindwa na kufilisika

  Hebu jiulize swali hili jepesi, kama timu mbili zinacheza mpira wa miguu, halafu moja yenyewe kazi yake ni kujihami isifungwe, wakati ya pili inashambulia kwa nguvu ili ipate magoli, je ni ipi yenye nafasi kubwa ya kushinda?

  Mfano huu unawazungumzia watu wawili tofauti: matajiri hucheza mchezo wa pesa kwa kushambulia ili kupata ushindi hivyo hufanikiwa kwa urahisi, wakati maskini hucheza kwa kujihami wakiogopa hasara au kufilisika na matokeo yake inakuwa vigumu kwao kushinda.

  Mara nyingi watu maskini hujali kuendelea kuishi bila kujali ni maisha ya namna gani wanaishi na huwa waoga sana kujaribu kufanya mambo mapya maishani kwa hofu ya kuharibu mambo. Utakuta mtu ana shilingi laki mbili kwa mfano, badala ya kuzitoa na kuzifanyia biashara anazidi kuziweka kwa hofu kuwa akizitoa zitapotea. Hayo ndiyo mawazo ya masikini.

  Matajiri ni tofauti, wao hupigania kuwa na nguvu kubwa kiuchumi bila kujali vikwazo wanavyokutana navyo, huwaza kukuza kila wanachokitaka wakati maskini huwaza kupata kidogo ili walipe madeni na kuendelea kuishi kama alivyo.

  3. WATU MATAJIRI HUJITOA KWA MOYO WOTE ILI KUPATA UTAJIRI
  Watu maskini hawajitoi kuwa matajiri na wala hawaamini kuwa wanaweza kuwa hivyo.

  Watu karibu wote ulimwenguni wanatamani kuwa matajiri na kumiliki mali. Kila mmoja anapenda siku moja ayamudu maisha yake kwa kila kitu. Awe ma nyumba nzuri, gari zuri, familia bora na maisha bora kwa ujumla, lakini ni wachache sana kati yetu tunathubutu kujitoa kwa moyo mmoja kupigania kile tunachokitaka.

  Utajiri sio kituo au mahali ambapo utajikuta tu ukiwa huko. Lazima ufahamu unatakiwa kufanya nini ili ufike pale unapotaka. Lazima ujibidishe usiku na mchana kwa moyo wako wote, hapo ndipo utakapoanza kuona mafanikio. Kila mmoja ana nafasi sawa ya kuwa tajiri, ila lazima afahamu anatakiwa kufanya nini ili afike hapo anapopataka.

  Uchapa kazi, bidii, malengo na kujiamini ni miongoni mwa mambo ambayo humuongezea mtu nafasi ya kufanikiwa maishani. Sababu kubwa inayofanya watu wengi washindwe kufanikiwa maishani ni kushindwa kupanga au kuyatambua malengo yao.

  Kila mmoja kati yetu ana lengo kubwa sana ambalo ndilo lililomleta hapa duniani. Anza kujiuliza leo lengo lako ni lipi na unatakiwa kufanya nini ili ulitimize.

  Ukishajua nini unachotakiwa kufanya, kifanye kwa moyo wako wote bila kujali vikwazo unavyokumbana navyo.

  Kama kila siku unawaza kununua baiskeli, bila shaka ukijituma lazima utanunua baiskeli. Lakini pia kama unawaza kununua gari, ukijituma lazima utamudu kununua gari. Kama pia unawaza kujenga nyumba ya vyumba vitatu, ukiweka uzingativu wa kutosha lazima utafanikiwa.

  Lakini pia unaweza kuwaza kujenga nyumba ya ghorofa na ukafanikiwa. Kwanini wengine wanawaza vitu vidogo vidogo wakati wengine wanawaza mambo makubwa? Kuwaza vitu vidogo vidogo ni dalili ya kuwa na akili yenye upeo mdogo. Jifunze kuwaza mambo makubwa bila kuwa na hofu ya namna ya kuyatimiza. Anza leo kuwaza mambo makubwa na utaona mabadiliko.

  Hii inawagusa pia watu wenye vipaji mbalimbali. Kwa mfano kama wewe una kipaji cha kucheza soka, malengo yako ni yapi maishani mwako? Kuishia ligi za mchangani, kufika ligi kuu ya nchi yako au kuichezea klabu kubwa duniani kama Arsenal au Real Madrid? Kama hukuwahi kujiuliza mahali unapotaka kufika, basi anza leo na jiambie mambo makubwa na anza kutekeleza yale unaoyaona madogo kwanza kwa ufanisi, kisha hata makubwa yatawezekana tu.

  5. WATU MATAJIRI HUYARAHISISHA MATATIZO YAO HATA KAMA NI MAKUBWA
  Watu maskini huyakuza matatizo yao hata kama ni madogo.
  Kufanikiwa maishani sio jambo linalotokea kama bahati. Katika njia ya kuelekea mafanikio, kuna vikwazo vingi sana ambavyo mtu anaweza kukumbana navyo. Unapokumbana na vikwazo vingi haina maana kuwa una bahati mbaya au umerogwa.

  Baadhi ya watu wamekuwa na tabia ya kuyakuza matatizo hata kama ni madogo kiasi gani. Unakuta mtu akikumbana na kikwazo kidogo anakuwa mwepesi wa kulaumu sana, atalalamika sana akiomba msaada kwa kila mtu. Ukiona mtu yuko hivi basi ujue ana fikra za kimaskini akilini mwake.

  Matajiri wao ni tofauti, hata akipatwa na tatizo kubwa kiasi gani hulirahisisha na kutafuta suluhu iliyo bora zaidi. Jiulize wewe uko katika kundi lipi?

  Ukweli ambao wengi wanashindwa kuujua ni kwamba hakuna tatizo dogo wala kubwa,yote yako sawa ila tofauti yake ni jinsi tunavyoyatafsiri akilini mwetu. Tafsiri hii ilishajengwa akilini mwetu tangu tukiwa wadogo na ndiyo tunayoitumia kutafsiri maisha yetu ya kila siku. Kama uliaminishwa kuwa kufilisika ni janga kubwa kuliko yote,bila shaka utakapofilisika inaweza kuwa ndiyo mwisho wa maisha yako kwani utalikuza jambo hilo na kuliona ni kama laana.

  Lakini kama ulifundishwa kuwa kushindwa jambo ni nafasi ya kulifanya jambo hilo tena kwa umakini na usahihi zaidi, utakuwa na nafasi nzuri ya kukabiliana na changamoto kubwa kirahisi kuliko wengine wanavyotafsiri.
  Matatizo katika maisha hayakwepeki, yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo. Usikubali tatizo likuzidi uwezo hata kama uliambiwa ni kubwa kiasi gani. Anza leo na utaona tofauti.

  Huna haja ya kuyaogopa matatizo, yaache yaje na jiandae kukabiliana nayo kishujaa bila kuwa na hofu au wasiwasi na utaona mabadiliko maishani mwako.

  6. WATU MATAJIRI HUTAZAMA MAFANIKIO ZAIDI KULIKO MATATIZO
  Watu maskini hutazama matatizo zaidi kuliko mafanikio.
  Watu matajiri wanatazama nafasi za kufanikiwa maishani wakati maskini wanatazama nafasi za kushindwa maishani.

  Kuna msemo mmoja maarufu sana ambao hutumiwa kuelezea maada hii. Kama glass ya maji imewekwa maji nusu, ukipewa na uambiwe ueleze unachokiona, jibu lako litakuwa ni lipi kati ya haya?
  Glasi ina maji nusu, au glasi iko tupu nusu? Haya yote ni majibu sahihi yanayowakilisha pande mbili tofauti. Kama unaiona glasi iko tupu nusu, basi una mawazo ya kimaskini akilini mwako, na kama unaiona ina maji nusu basi una mawazo ya kitajiri.

  Kuona glasi iko tupu nusu maana yake ni kushindwa kutambua na kuyaona mafanikio ambayo tayari umeshayapata na badala yake kutazama matatizo yanayokukabili. Wengi wetu tuko katika kundi hili. Tunaumizwa na yale ambayo hatuna na hatuyafurahii yale ambayo tumefanikiwa kuyapata.

  Jifunze kujipongeza kwa mafanikio unayoyapata hata kama ni madogo kiasi gani na acha kuyaogopa matatizo hata kama ni makubwa kiasi gani. Yatazame mafanikio zaidi kuliko matatizo. Ukimudu kufanya hivi, basi utakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa maishani.  [​IMG]

  source:http://www.globalpublisherstz.com/2009/10/22/tofauti_ya_mawazo_ya_maskini_na_tajiri2.html
   
 2. Typical

  Typical JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 261
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  some good staff
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,027
  Trophy Points: 280
  Hahahahah! Sisi matajiri kumbe tuna mamboe?
   
 4. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  wauza unga, wameza vidonge wako kundi gani? Maana huwa wanajitoa kwa moyo wote ili kupata utajiri au wale cowards wanatumia vijana kufanya kazi zao. Hapo vipi? Maana utajiri wao haukai na si wa raha, cos the sh*t always hits the fan.
   
 5. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nimeipenda!
   
 6. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2013
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 8,623
  Likes Received: 4,773
  Trophy Points: 280
  Dah mmh
   
 7. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2013
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,633
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  nimeipenda ila ni kama unauza mchoro wa da vinci Mbagala kwa Mfuga mbwa!
   
Loading...