Utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, May 9, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Dr Faustine Ndungulile Mbunge wa Kigamboni (ccm)

  Utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka*mitano


  Leo asubuhi nimeshiriki kwenye semina iliyoandaliwa na wakala wa vizazi na vifo (RITA). Lengo la semina hii ilikuwa kuhamasisha wadau kuhusu zoezi la majaribio la kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kwenye kata 14 za majimbo ya Kigamboni na Temeke.

  Hivi sasa ni asilimia 14 ya watoto chini ya miaka mitano wamesajiliwa na ni asilimia 6 tu ambao wana vyeti vya kuzaliwa. Tanzania ndio nchi pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashiriki yenye idadi ndogo ya usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano.

  Nimefurahia mikakati ambayo RITA inayo ili kuondokana na tatizo hili.

  RITA imepanga kufanya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa katika mikoa mitano baada ya zoezi la majaribio katika Wilaya ya Temeke. Majaribio haya yanalenga kufanya tathmini ya makakati mbalimbali ya maboresho wanayotarajia kuyafanya.

  Ili kuondokana na ukiritimba uliopo RITA imepanga kupanua wigo wa utoaji wa huduma hii. Wanatarajia watumishi wa Afya kutoa vyeti vya kuzaliwa kwenye zahanati, vituo vya Afya na mahospitalini. Kwa watoto wanaozaliwa nje ya mfumo wa hospitali, wakunga, watendaji wa vijiji, mitaa na kata watahusika.

  Vilevile RITA ina mpango wa kufanya maboresho katika utumiaji wa teknolojia ya mtandao na simu kutoka vijijini hadi makao makuu ya RITA ili kurahisisha upatikanaji na utunzaji wa taarifa.

  Nawapongeza RITA kwa maboresho haya makubwa ambayo yanatarajia kuyafanya na ninaahidi kuwapa ushirikiano wangu ili watoto chini ya miaka mitano katika Jimbo la Kigamboni wanasajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa.
   
Loading...