Utiwaji saini wa mkataba kati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kampuni ya DNATA na EGIS

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
714
463
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi amesema uamuzi wa Serikali wa kushirikiana na Kampuni za National Air Travel Agency (DNATA) pamoja na EGIS katika uendeshaji wa Huduma za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Terminal III, unalenga kuimarisha uchumi kwa mtazamo mpana ili kuvutia mashirika ya ndege zaidi kufanya safari zake hapa Zanzibar.

Dk. Mwinyi amesema hayo leo katika shughuli ya utiaji saini wa mkataba wa Mashirikiano ya Uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (terminal III), baina ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na Dubai National Air Travel Agency (DNATA), pamoja na Kamuni ya EGIS, hafla iliofanyika Ikulu Jijini Zanzibar.

Alieleza kuwa ongezeko la ndege utaongeza idadi ya watalii wanaokuja kuitembelea Zanzibar, wageni, mizigo na ukuaji wa biashara pamoja na soko la ajira.

Alisema ujio wa watalii utaambatana na ukuaji wa sekta mbali mbali muhimu katika ukuaji wa uchumi , akibainisha uamuzi huo wa Serikali umelenga kuleta manufaa mapana ya kiuchumi katika sekta zote.
 
Back
Top Bottom