Ndugu wana bodi habari ya leo.
Niende kwenye mada. Malori ya mizigo yamekuwa mengi sana barabarani kuliko magari ya aina nyingine. Ukibahatika kusafiri kutoka DSM kwenda Mwanza, malori haya yamejaa. Ukisafiri kwenda Mbeya mpaka Iringa malori haya yamejaa. Ukisafiri kutoka Ruvuma kwenda Lindi au Mtwara malori yamejaa. Yaani utitiri wa haya malori ni mwingi sana.Hata Ukiwa hapa DSM, malori haya ni mengi sana.
AJALI
Ajali za malori haya zimekuwa nyingi sana na mara nyingi tunaambiwa kuwa Lori hilo limefeli breki. Je, hizo breki kila siku zitakuwa zinafeli na kuuwa abiria wasio na hatia? Huu ni uhuni na ugaidi wa kisirisiri unaofanywa na baadhi ya watu. Hata wewe unayesoma hii taarifa yangu siku moja ndugu yako au rafiki yako atagongwa na Lori na tutaambiwa kwa urahisi tu kuwa breki zimefeli. Mama Samia, kama utapata nafasi ya kusoma huu uzi Tafadhali tunaomba uchukue hatua kutusaidia sisi wananchi wako.
MATUKIO YA AJALI
Mwezi Machi Lori kubwa la mizigo liligonga basi la Ahmed lililokuwa linafanya safari za kutoka Tanga kwenda Mbeya na kuua watu 23. Mwezi Machi: Lori la mizigo liliacha njia na kwenda kugonga nyumba iliyo karibu na barabara na kuua watu watatu, Morogoro Mikumi.
Mwezi March mwishoni Profesa wa Mzumbe aliangukiwa na kontena kutoka juu ya Lori na kufariki: Mwezi wa tisa: Mkurugenzi wa Igunga akitoka Mbeya gari yao ilivamiwa na Lori, kwa madai ya kukosa breki.