Utitiri wa makampuni ya michezo ya bahati nasibu kwa njia za SMS umekuwa kero

The Iron

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
1,393
1,453
Kwa miaka ya karibuni kumekua na utitiri wa makampuni ya michezo ya bahati nasibu kwa njia za SMS hapa nchini.......

Makampuni haya yamekua na usumbufu uliopitiliza sana kwa tabia yao ya kutumia watu msg mara kwa mara bila kujali kwamba mtu amewahi kuwa mshiriki au la....na sijui namba za simu wanazipata kwa njia gani

Nilijaribu kupiga simu mtandao husika wakadai hawawajui badae nikapiga simu bodi ya michezo ya bahati nasibu nao wakatoa ahadi kwamba watafwatilia lakini ajabu mpaka Leo ni miezi imepita hamna kitu chochote

Jambo la kusikitisha ni kwamba wengi wa watu walio maeneo ya vijijini, kutokana na ugumu wa maisha wameathiriwa sana na hii michezo kama ilivyo kwa wale wa betting (Yani mtu akiona msg imeandika sijui "Tuma neno xxxx ushinde 100,000 sasa hivi" chap chap anatuma bila kusitasita

Mamlaka husika naomba mdhibiti hili swala
 

Attachments

  • Screenshot_20191009-225222~2.png
    Screenshot_20191009-225222~2.png
    9.5 KB · Views: 2
  • Screenshot_20191009-225157~3.png
    Screenshot_20191009-225157~3.png
    17.2 KB · Views: 2
Back
Top Bottom