Utitiri wa Div One za point 7 zinaleteleza GPA 4.5 kule SUA na UDSM. Na zamani tulikwama wapi? Tujadiliane kidogo

Ki ukweli one ya 7 sio kitu ajabu vijana wa sahivi wanawekezwa kwenye elimu wakiwa wadogo. Wanafundishwa katika mazingira bora na kila facilities za kunufaisha ubongo wao

Kwa nini wasipate one ya saba. One ni kitu rahisi sana
 
Ni wivu au ni husuda? Mafanikio ndiyo tunayoyahitaji kwa Kila mtu tena ingependeza Nchi nzima hasa shule za serikali zikafaulisha watoto wote kwa hiyo division 1 maana tunahitaji mambo mema kwa Kila mtu na siyo mabaya, tufanikiwe kwenye elimu tuondoe ujinga, tufanikiwe kwenye ustawi wa Kila mtu tuondoe umasikini na tufanikiwe kwenye malazi na miundo mbinu Bora Ili tuishi na afya njema tupate uwezo wa akili wa kufanya mambo makubwa Sasa kutaka watoto wasifaulu Ili iweje?
 
Tanzania kuna ugonjwa umeingia wa wanafunzi wa kidato cha nne kupata Division one Za point 7 nchi nzima.
Dr msonde wewe ulipata Div one ya point 7?
Je ina maana ulikuwa huna akili au ni mtindo wa sasa kupata point 7?
Mtihani ya multiple choice ina madhara makubwa.

Wewe una matatizo binafsi, wamepata wote? Hakuna waliofeli? Wewe usitake Tabu zako Za kusoma mwaka 1932 wapate wanaosoma 2012
 
Kiasi fulani paper za zamani zilikuwa za moto haswa mbali na kwamba materials upatikanaji wake ulikuwa mgumu.

Lakini siku hizi paper zimelegea na upatikanaji wa materials kwa maana ya vitabu, vitini ,past papers ni mwepesi sana.

Mwisho, Watungaji wa mitihani wanatunga mitihani ambayo angalau ni fair kwa shule za kata, sasa mitihani hiyo inapokutana na wanafunzi wa St's inakuwa Kama maji ya kunywa tu.
Acha kudharau shule za kata kule ndio kuna cream ni pesa tu hawana na wao wangeenda st. Nanii uko
 
Ni mtoto yuko private kidato cha pili 2021. Darasani hushika nafasi ya 8 au 9 kati ya 70. Hajawahi kushuka wala kupanda hapo. Kinachobadilika ni wastani. Kwenye mitihani ya shule hupata wastani 69 had 73. Juzi matokeo yanatoka ana division 1 ya pointi 7. Kwa masomo yake yote ana B moja tu . Masomo mengine yote ana A.

NILICHOJIFUNZA:
Shule za private hutunga mitihani na mazoezi magumu compared to 'shule za kata'. Watoto hawa wakiletewa mitihani ya baraza huona ni uji ndiyo maana hupata alama za juu kiasi hiki.

Hatuna baraza la mitihani. Tuna jina tu la l baraza la mitihani. Wanatunga mitihani dhaifu sana ili kuzibeba shule za serikali hususani za kata ili zionekana zimefanya vizuri.

Kwa maoni yangu shule binafsi zingepewa kazi ya kuandaa mitihani ya kitaifa. Halafu tungeona shule za serikali zinapata ufaulu gani.
Hujatumia akili hapa
 
Hapa naona wazazi wanaolipa ada za mamilioni wanaumia wakiona watoto wao wamefaulu sawa na wa kata anayelipa ada ya laki 2
 
Waacheni watoto wa watu. Kupata kwake one 7 ya saba hupati chochote wala hupungukiwi chochote .
 
1. Kuna ukweli kuwa mitihani zamani ilitungwa na walimu wakongwe, na sasa NECTA wametunga wenyewe?

2. Usahihishaji unafanyika kwa muda mfupi sana , wameongeza wasahihishaji au wasahihishaji wameongeza speed?

3. Kuna ukweli kuwa wasahihishaji wakimaliza kazi, wataalamu na standardazation huingia kazini?

4. Sifa za walimu wanaosahihisha mitihani hiyo zikoje, muda wao kazini yaani uzoefu, ufaulu wao mitihani kama hiyo wapokuwa wanafunzi?

5. Malipo ya wasahihishaji kwa siku wanalipwa kiasi gani au mtihani mmoja wanalipwa kiasi gani. Na ni malipo yanayoendana na rate za zilizopangwa na serikali kuwalipa watumishi wanapokuwa nje ya kituo au kunamanunguniko?

6. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Dr. Msonde anatoa sababu gani za ufaulu wa watoto miaka hii tangu alipoteuliwa kushika nafasi hii tofauti ya miaka ya mtangulizu wake Prof. Ndalichako? Na tunakubaliana na sababu anazozitoa.

7. Wahadhiri wa Vyuo vikuu waliofundisha muda mrefu wanasemaje wanapofanya mlinganisho wa wanafunzi wanaojiunga na Vyuo vikuu wa Dr. Msonde na wale wa zamani wa Prof. Ndalichako.

8. Tume ya ajira na waajiri wanasemaje wanapofanya mlinganisho wa vijana wa sasa wa point 7 na wale za zamani kiutendaji.

9. Maswali wanayoulizwa watoto yakoje kwa sasa, yanapima nini sasa?

10. Kwanini somo kama la hesabu watoto bado wanafeli tofauti na masomo mengine?
9. Wa miaka hio walisoma ABBOT na NELKON na maswali yalitoka humo na sasa hivi wanad
soma hizo ABBOT na maswali ni yaleyale.
Watoto wa sasa hivi wapo under intensive care na wana resource nyingi za kujifunzia ikiwepo JF.
It is very simple.
NECTA hawajawahi kuwa na maswali mapya kwa sababu mada ni zile zile hakuna mada mpya kutoka mbinguni.
 
Fikiri kidogo kabla hujasema.
Hao private tumekutana nao chuoni ni watoto sana.

Chuoni hakuna spoonfeeding kwa hiyo wanateseka sana.
Ni mtoto yuko private kidato cha pili 2021. Darasani hushika nafasi ya 8 au 9 kati ya 70. Hajawahi kushuka wala kupanda hapo. Kinachobadilika ni wastani. Kwenye mitihani ya shule hupata wastani 69 had 73. Juzi matokeo yanatoka ana division 1 ya pointi 7. Kwa masomo yake yote ana B moja tu . Masomo mengine yote ana A.

NILICHOJIFUNZA:
Shule za private hutunga mitihani na mazoezi magumu compared to 'shule za kata'. Watoto hawa wakiletewa mitihani ya baraza huona ni uji ndiyo maana hupata alama za juu kiasi hiki.

Hatuna baraza la mitihani. Tuna jina tu la l baraza la mitihani. Wanatunga mitihani dhaifu sana ili kuzibeba shule za serikali hususani za kata ili zionekana zimefanya vizuri.

Kwa maoni yangu shule binafsi zingepewa kazi ya kuandaa mitihani ya kitaifa. Halafu tungeona shule za serikali zinapata ufaulu gani.
 
Tafuta papers za miaka ya 70, both O level na A level, linganisha na ya Sasa. Utapata jibu!
Hiyo miaka walikuwa wanazidi kupenda sifa!!

Mi mwenyewe class eti walikuwa wananiona mkali wa Kemia! Basi bhana kuna siku likaletwa paper la 1978! Hakuna nilichoelewa, na hakuna aliyeelewa chochote!!

Tuka-conclude kwamba inawezekana palifanyika mabadiliko ya mtaala manake haiwezekani kila swali tunalogusa halisoviki na wala halieleweki!!

Sema papers za siku bhana zimezidi rojo rojo! Papers za kuumiza kichwa ziliishia in 1990's!

Nakumbuka wakati tupo A-Level, Tanzania mzima hapakuwa na A ya Uchumi, na kama kuna waliokuwa wamepata B, basi hawafiki 5, and I doubt kama waliwepo!! Na hiyo ilikuwa ndo trend yenyewe! Ukipata C fahamu una chance kubwa ya kuwa kwenye Top 10!

Siku hizi sasa... madogo wanasimamisha A za Economics kama hawana akili mzuri, na nilivyofuatilia nikagundua Paper II ambayo ilihitaji reasoning, na ndiyo ilikuwa inafelisha watu, hivi sasa imechakachuliwa bila kufahamu Economics inahitaji sana logical and analytical reasoning!
 
Back
Top Bottom