Utitiri huu wa Mitumba, Watanzania tumekubali kuwa Dampo?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utitiri huu wa Mitumba, Watanzania tumekubali kuwa Dampo??

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nicky82, Sep 8, 2010.

 1. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengi watakubaliana na mimi kuwa biashara ya mavazi ni moja kati ya biashara isiyopitwa na wakatati, ni kama vile ilivyo biashara ya vyakula, kwani mtu atahitaji kula na kuvaa kila siku.
  Linalonitatiza kwa sasa ni utitiri huu wa mitumba ya nguo ulionea kila kona ya nchi hii, na utamaduni unaozidi kujengeka wa watanzania kupenda kuvaa nguo za mitumba,viatu,n.k. Kuna wakati nahisi kuwa ni kama nchi yetu imegeuzwa dampo la wenzetu kutupia vitu used. Sina lengo la kuwakejeli wale wanaovaa mavazi hayo kwani hata mimi nilivaa wakati huo.
  Swali mbalo najiuliza ni kuwa tumeshindwa kuendeleza viwanda vyetu vya ndani, au pamba haipatikani, au ni utamaduni wetu wa kupenda vya 'nje' au Watz wengi hawana uwezo wa kununua nguo mpya??

  Sijasikia kwenye kampeni vyama vikiongelea hili la kufufua/kuimarisha viwanda vya nguo vya ndani, ni kwamba tumeridhika nalo au ni yaleyale ya liache bora liende
  .

   
 2. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  soko holela mkuu! yaani hakuna kitu kama hiki kinachoniuzi kama mitumba kuwekwa kipaumbele badala vitu vyetu wenyewe. Kuna kiwanda cha nguo hapo Arusha wanazalisha nguo nyingi sana, lakini zinauzwa Marekani, Uingereza, canada nk. Hizo nguo zinaenda zinavaliwa then zinarudi bongo! what the hell are we?

  Nani wakulaumiwa? Watunga sera ndo hawana bongo sawa sawa, maana hata kama hawakusoma lakni angalau wanaenda nchi nyingi wanajionea mambo yalivyo lakini wanaishia kula, kunywa na kufanya starehe badala ya kuwa wabunifu wa mambo kwa ajili ya nchi yetu.

  Anyway, nadhani watanzania wengi wanaona hilo linarahisha maisha lakini kumbe ndo kwanza linatumaliza kila siku.
   
Loading...