Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Rais ametangaza kuwa siasa za majukwaani zitafanywa 2020, Pia taarifa ya kiusalama ya Jeshi la Polisi nikuwa hakuna mikutano ya vyama vya siasa. Vyama karibu vyote vya Upinzani vimetii maagizo hayo ya kiusalama, lakini Chama Tawala CCM inaonyesha kama chenyewe hakiishi Tanzania na wala hakihusiani na maagizo hayo ama kipo juu ya sheria.
Taarifa za kuaminika toka Dodo zikimnukuu naibu katibu mkuu wa ccm kupitia radio mmoja nchini, anasema mara baada ya kukabidhiwa kiti mwenyekiti mpya wa ccm atazunguka nchi nzima kujitambulisha kwa wananchi.
Pia mara baada ya kupewa kiti hicho tarehe 23 kuna utambulisho yani mkutano wa hadhara dodoma na kumpokea Dar.
Sasa taifa lifahamishwe kuwa mikutano ya kisiasa ruksa au ni marufuku kwa vyama vingine tu isipokuwa chama tawala.
Utii wa sheria bila shuruti unasubiriwa!!