Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Mfalme Daudi - umeelezea vizuri - lakini unaonaje kuhusu hii bia ya watu kupenda 0713 - haufikirii kuwa ikawa cha
ELIMU YA AFYA KUHUSU U.T.I!! NA KAMA HALI HALISI NDIYO HII BASI KUNA UWEZEKANO WANAOPATA MAJIBU SAHIHI YA UTI NI ASILIMIA NDOGO SANA!!

MAJIBU ya UTI hayatoki ndani ya muda mfupi

By Kalunde Jamal, Mwananchikjamal@mwananchi.co.tz

Hali yako kiafya siyo nzuri na unahisi una malaria kutokana na kuwa na dalili zote za ugonjwa huo.

Unaamua kwenda zahanati kupata vipimo vya afya, unakutana na foleni ya wagonjwa, hivyo unafuata utaratibu wa kwenda kumuona daktari kisha unachukuliwa vipimo na kupelekwa maabara.

Ndani ya saa moja, ukiwa umekaa kwenye benchi huku umeshika tama, anakuja muuguzi kukuita ili uende kuchukua majibu yako kwa daktari ambayo yanaonyesha una maambukizi ya njia ya mkojo (UTI).

Hakika ugonjwa huu umekuwa ‘maarufu’ siku hizi kwa kuwa wengi wanaokwenda katika baadhi za hospitali, zahanati au vituo cha afya kupata tiba huambiwa wana UTI.

Huenda hiyo ndiyo sababu ya kushamiri kwa biashara ya kuuza dawa za ugonjwa huo kwenye baadhi ya zahanati na vituo vya afya.

Utafiti uliochapishwa miaka kadhaa iliyopita na Asina Pacific Journal of Tropical Medicine, umeonyesha kuwa zahanati na vituo vya afya binafsi hulenga kuuza dawa kama chanzo cha mapato badala ya kuangalia afya ya mteja(mgonjwa).

Kwa mujibu wa utafiti huo, vituo vya afya na zahanati binafsi huongeza malipo kwa mgonjwa kwa kumuandikia sindano za ugonjwa huo.

Wagonjwa wasemaje?

Wagonjwa saba kati ya 10 waliohojiwa na gazeti hili kwenye vituo vya afya viwili na zahanati sita waliopimwa afya kutokana na kusumbuliwa na homa, waliambiwa vipimo vyao vimeonyesha wana UTI.

“Hee huu ugonjwa umening’ang’ania kila nikijisikia vibaya nikipima nakutwa na UTI na dawa ninazopewa ni hizi hizi Ciprofloxacin,”anasema Zulfa Zayd ambaye ni miongoni mwa wagonjwa waliohojiwa na gazeti hili. Nilihama zahanati na huku nako nimekutana na yale yale, kilichobadilika ni aina ya dawa huku nimepewa Ciplo, nimechoka jamani.”

Agness Shao aliyekuwa akipima afya kwenye zahanati iliyopo maeneo ya Kinondoni anasema anajua ugonjwa wake ni huo.

“Nikijisikia vibaya nakwenda kupima kwa ajili ya kujiridhisha, lakini najua kabisa huu ndiyo ugonjwa wangu kwa sababu tunatumia choo kimoja watu wengi,” anasema Shao.

Wataalamu wa afya wazungumza

Mganga mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi anasema waliopewa mamlaka ya kulinda afya za wananchi wanaonekana kulisahau jukumu lao na kwa kufanya hivyo wanahatarisha maisha ya wananchi.

“Tumekuwa tukisema mara nyingi hatua za kupima maradhi hayo, kwanza unaupima mkojo na unaweza kupata mabadiliko ya mkojo kwa kupima kipimo cha kwanza ukahisi ni UTI, ilihali kitaalamu ni lazima kujiridhisha kabla ya kutoa uamuzi wa majibu kwa mgonjwa,”anasema Profesa Kambi.

Anaongeza kuwa mkojo unapopimwa unaweza kuonyesha kuwa kuna bakteria, ili kujiridhisha kama ni wa ugonjwa huo lazima wale bakteria waoteshwe hatua hiyo kitaalamu inaitwa (culturing bacteria).

“Ili upate majibu sahihi kipimo hiki huchukua saa 48 kwa uchache hadi 72, tofauti na hapo majibu hayo si sawa. Tunakemea kila siku kumpa mtu dawa za ugonjwa asiokuwa nao... ni kumtia usugu, kwa sababu ukifanya na kipimo cha kuotesha bakteria kinakupa na mwelekeo wa dawa gani atumie, kwa kuhisi hisi lazima utampa isiyokuwa sahihi,” anasema Profesa Kambi.

Daktari Godfrey Materu wa Kituo cha Afya cha Arafa kilichopo maeneo ya Temeke Dar es Salaam, anasema kuna wagonjwa wanakwenda kupima wakiwa na majibu yao kichwani.

“Kuna wakati tunalazimika kutoa elimu, kwa sababu wagonjwa huja na majibu ya magonjwa yao kichwani, wanapoambiwa hawana homa wanakasirika na kwenda kupima mahali kwingine.

“Kuna wakati nilinusurika kufukuzwa kazi kwenye zahanati fulani baada ya kumueleza mgonjwa aliyekuwa anapata homa kuwa hana malaria, UTI wala Typhoid badala yake ana uchovu akanywe maji na apumzike muda mrefu, ”anasema Dk Materu.

Anafafanua kuwa mgonjwa alikuwa anamfahamu mwenye zahanati ndipo alikwenda kumwambia kuwa hakupimwa ipasavyo.

“Aliambiwa (na mwenye zahanati) aje siku inayofuata na asilipe; apimwe na daktari mwingine. (alipopimwa) alikutwa na UTI nyingi na malaria wadudu watano na kununua dawa pale pale na aliondoka kwa furaha,”anasema.

Kutokana na vipimo hivyo kutofautina na vyake, bosi wake alimfokea na kumuona kama mtu anayetaka kumfukuzia wateja.

“Sipingani na hilo, lakini nashauri wagonjwa wawaamini wataalamu wa afya, badala ya kuja na majibu ya homa zao kwa madai wanajijua,” anashauri Dk Materu.

Utaratibu wa vipimo vya UTI

Mkuu wa mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha KCMC, Profesa Alfred Mteta anasema ili kujua kama mtu ana UTI au la, mkojo wake unatakiwa kupita kwenye vipimo saba.

Anasema vipimo hivyo vikibainisha kuwapo kwa bakteria ndiyo wataoteshwa kupata uhakika kama ni maradhi hayo au la, na itafanyika kwa saa *48 au 72.*

“Kinachofanyika sasa ni biashara badala ya huduma, hawa wenye hizi zahanati wanalenga zaidi kuuza dawa.

“Wanasahau kuwa kazi yao ni kulinda afya za watu na siyo kuwaumiza, kumpa mtu dawa kwa ugonjwa asiokuwa nao ni kuufanya mwili uwe sugu na usikubali matibabu,”anasema.

Profesa Mteta anasema UTI inaanza na dalili kwa mgonjwa ikiwamo kuhisi maumivu au moto kwenye njia ya mkojo na kukojoa mara kwa mara.

“Baada ya dalili hizo mgonjwa akisikilizwa na kupimwa na daktari, hufanyiwa pia vipimo vya maabara. Kipimo cha kwanza na cha muhimu sana ni urinalysis ambacho pamoja na mambo mengine mkojo wa mgonjwa huzungushwa kwenye mashine maalumu (centrifuge) halafu huangaliwa kwenye darubini!,” anasema Profesa Mteta.

Akielezea zaidi anasema lengo ni kuangalia kama kweli kuna ushahidi wa UTI hasa uwapo wa white cells na red cells (Seli nyeupe na nyekundu) nyingi.

“Vilevile huangalia uwapo wa bakteria katika mkojo pamoja na aina nyingine za seli na vijidudu,” anasema.

Akizungumzia hatua ya pili, anasema ni kuufanyia ule mkojo ‘culture’ yaani kuotesha na kutambua aina ya vidudu vilivyo kwenye mkojo.

“Hii ya culture huendana na sensitivity test yaani vile vidudu vilivyoota hujaribiwa kwenye maabara ni dawa gani itafaa kuvitibu. Hatua zote hizi _zinachukua saa 48 hadi 72! Lakini_ zinampa daktari uhakika wa uwapo wa UTI na matibabu gani yatolewe yaani antibiotic gani na kwa dose gani na muda gani.

“Huo ndiyo utaratibu ambao sasa unavunjwa na baadhi ya watu wasio na weledi kwenye taaluma ya afya ambao huchukua njia ya mkato na kubambikiza wateja UTI ili kuwauzia dawa tu,” anasema Profesa Mteta. Pia, anasema wagonjwa wanaweza kuathirika na antibiotics hizo na vilevile dawa holela husababisha usugu wa vijidudu kwa antibiotics.

Sent using Jamii Forums mobile app

nzo kikubwa cha UTI - badala ya kusema wagonjwa wanakuja na majibu yao? Inawezekana wagonjwa wanajua kile walichokifnya - ndio maana wana majibu.
 
Mfalme Daudi - umeelezea vizuri - lakini unaonaje kuhusu hii bia ya watu kupenda 0713 - haufikirii kuwa ikawa cha

nzo kikubwa cha UTI - badala ya kusema wagonjwa wanakuja na majibu yao? Inawezekana wagonjwa wanajua kile walichokifnya - ndio maana wana majibu.
Duuh mkuu
 
Wazee wakazi mchumba angu anasumbuliwa sana na hii kitu naomben anaejua dawa nzur kwa uti sugu aseeh mm nimepima nikovizur sina uti ila yeye ni wimbo wa taifa yan msaaada naomben jamaan naomben sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazee wakazi mchumba angu anasumbuliwa sana na hii kitu naomben anaejua dawa nzur kwa uti sugu aseeh mm nimepima nikovizur sina uti ila yeye ni wimbo wa taifa yan msaaada naomben jamaan naomben sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ameshatumia dawa gani Kwanza mpaka ukahisi hio ni sugu? Na huo ugonjwa kwake una mda gani? Pia ukiweka umri wake itakua vizur? Ukinijibu hayo naweza alau kukushauri.
 
Nilisumbuliwa na U.T.I kwa miaka 4,nilitumia kila dawa na nilifikia hatua ya kukata tamaa.
Ila niliingia Youtube ili kuona kama naweza pata tiba mbadala,kupitia TOP TEN TV nilipata tiba ya moja kwa moja.

Chukua kijiko kimoja cha BICARBONATE OF SODA(ina boksi la blue na chapa ya simba),changanya na maji safi na salama ya kunywa yenye ujazo wa 400 mls(Nusu lita kasoro mils 100)koroga mpk B.S ichanganyike vzr,
Kunywa maji yote then usubiri kwa muda wa dk 45 ndio unywe chai.

Mchana kbl ya kula,tengeneza mchanganyiko mwngn,kunywa,subiri 45 ndio ule.

Usiku fanya hivyo hivyo,Kama U.t.I ni sugu fanya zoezi hili kwa siku 7 na kama sio sugu kwa siku 3.

Nilipona kbs U.T.I
 
Wazee wakazi mchumba angu anasumbuliwa sana na hii kitu naomben anaejua dawa nzur kwa uti sugu aseeh mm nimepima nikovizur sina uti ila yeye ni wimbo wa taifa yan msaaada naomben jamaan naomben sana

Sent using Jamii Forums mobile app
jibu hayo aliyosema mkuu apo juu, then tujue tunakusaidiaje... lakini pia tofauti na dawa anazotumia je namna yake ya kuishi huwa anabadili akishatumia dawa, maana unaweza sema ni sugu kumbe akitumia dawa anapona afu anapata maambukizi mengine... hii inaweza sababishwa na nguo za ndani anazovaa kubaki na vimelea, kama maambukizi huwa anayatoa bafuni au chooni bado anarudi kule kule na kwa style ile ile...
nashauri pia, achukue vipimo vya uhakika... some time watu wa maabara zetu huwa wanakimbilia conclusion ya uti, kumbe ni fungus ama sti....
leta maelezo ya kutosha tujue uzito wa tatizo, then tutakushauri the best way ya mpenzi wako kupona
 
Habari wataalam wa jukwaa hili,

Nimewahi kwenda hospital kupima nkaambiwa nna UTI, nkamuuliza dr kama inaambukiza akasema haiambukizi, lakini katika kuongea na watu huku mtaani pamoja na mijadala kwenye mitandao, wengine wanadai inaambukiza,

Wakuu naomba kufahamishwa zaidi kama kweli inaambukiza au haiambukizi...
 
Hello
UTI imekua tatizo sana kwa wanaume na wanawake, kuna watu imetibika wengine wanakunywa magunia ya dawa na sindano bila mafanikio, natumai unajua chanzo dalili na madhara ya ugonjwa sitayasema.

Nilikimbizana na uti kwa muda mrefu zaidi ya miez nane, kila nikibadili dawa wapi, hadi nikakata tamaa, ilianza kama utan nilianza kuwashwa na kutoka usaa kweny uume nilijua gono kumbe uti nilipoteza hela za vipimo na dawa zaidi ya laki nne, naandika Uzi huu nikiamini wengi wanapitia na watapitia, itasaidia kujua niliponaje.

Nilichofanya nilifanya utafiti wakutosha kwenye web na blog za English na kiswahili nikagundua wote wanamaelezo yale yale, nikachukua mbinu kila sehem na kuziunganisha, unapotibu ugonjwa huu ukiwa sugu inabidi iwe kazi kazi otherwise itachi kizazi na ikipanda kwenye figo ni hatari.

Kama uko busy kazini itabid uombe ruhusa kabisa kwa wiki mbili.

Nilichoma zile sindano tano, nikaunga na vidonge vya azuma packet nne, wakati natumia vidonge makali yalikua yamepungua kidogo, nilikua nakunywa maji lita tano kwa siku, kama una choo cha ndani itafaa sana, usinywe yabaridi hutaweza kunywa ya uvugu vugu taratib kikombe kwa kikombe huku unafany mambo mengine,

Niliacha kabisa sukari, ni chakula cha bacteria, iwe yenyewe au iliyo kwenye biscuit cake maandaz nk, itabid ule dona mboga majani na maharage, wengi wanakosea kwenye chakula wanawalisha wadudu, hii nikuanzia unapoanza matibabu hadi mwisho.

Nilikua natumia mchai chai nachemsha, nakunywa mara mbili kwa siku nachanganya na baking soda ukipoa, hii ilisaidia sana muwasho wote uliisha
Mchai chai ni ule ulio kama nyasi mana iko mingi.

Nilikua napiga zoez karib kila siku na niliacha kufanya mapenzi, kama una mpnz hakikisha wote mnapitia hizi hatua mana utafanya kazi bure itajirudia

Nilichogundua uti ni neno la jumla linalowakilisha mashambulizi kwenye njia ya mkojo manake hakuna bacteria mmoja madaktari hawana elim wanatoa tu dawa bacteria anazifanya msos wa jion

Ushauri wangu wa mwisho kama dawa za hospital zikigoma usiendelee nazo utasababisha matatizo mengine, dawa ni sumu fuata ushauri niliokupa ukifeli nunua dawa asilia kutoka herbs japo nigharama sana jama yang alichukua dose kwa elf tisini, lakini alipona, alifuata pia maelekezo niliyoyatoa hapo juu .
From
Paternus
 
Dalili za sukari zinafanana sana na UTI niliwahi kuhisi nina UTI baada ya vipimo sikukutwa na UTI ila sukari. Nilianza masharti ya kuacha kabisa sukari na vywakula vyenye wanga mwingi sasa hivi ni mzima kabisa
 
Baking powder ulikuwa ukiweka kiasi gani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom