SoC01 Uthubutu ni Silaha ya Mafanikio

Stories of Change - 2021 Competition

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,215
3,587
Nyanja: Maendeleo ya Jamii

th

Mark Zuckerberg mmiliki wa FB
Taswira kwa hisani ya Google​

Utangulizi
Tabia ya uthubutu haikuumbiwa waoga wala wenye soni bali wajasiri, kuna usemi kuwa wenye visu vikali ndiyo wala nyama. Kule mwituni, simba angekuwa mwoga na mwenye soni njaa ingemwondoa kwenye uso wa dunia. Uthubutu unamfanya simba amjaribu hata tembo, faru na nyati. Sisimizi licha ya udogo wao kimaumbile wanao uwezo wa kumshusha tembo chini kwa sababu wana malengo ambayo lazima yatimie hata kwa kuthubutu (Fortune favours the brave. Bahati hupendelea wajasiri) na kwenye himaya ya sisimizi tembo hakai (hajikuni kwenye mti ambao ni makazi ya sisimizi). Halikadhalika, mbwea wana uthubutu na ushirikiano, wanawinda kama timu kasoro makundi maalum kama watoto na wazee, na wanagawana mawindo kwa usawa, hii ni tofauti na jamii ya simba ambapo dume ni bazazi tu mwenye kazi moja ya kuzalisha na kulinda himaya yake asiporwe majike yake.

Ujasiri wa kutenda
Wengi chini ya jua waliofanikiwa waligundua kuwa kutenda kwa ujasiri hakukwepeki katika utendaji wenye kuona mafanikio mbeleni na kudhamiria kuyapata mafanikio hayo. Macho ya wajasiri kamwe hayaoni kufeli mbele bali yanaona mafanikio tu, na roho za wajasiri haziogopi vikwazo maana wana silaha ya uthubutu. Mpiganaji aendapo vitani huwa ana uhakika wa kushinda tu, kama angejuwa hashindi asingeenda vitani. Mtaji (gharama) wa vita unatisha sana lakini faida yake ni endelevu kwa vizazi na vizazi. Aidha, wapo watu wanaotishwa na umri wao ama mdogo au mkubwa. Katika mchakato wa kutafuta maendeleo hofu ya umri wakati fulani imewafanya watu kujihukumu wenyewe kuingia kifungoni (ama kifungo cha umaskini au cha kutofanikiwa jambo lako fulani) badala ya kuwa huru. Wengi wa Walimwengu waliofanikiwa wamefanikiwa katika umri mkubwa na ni kwa sababu waliamua kwa dhati kabisa kutangaza uadui dhidi ya hofu ya rika. Mojawapo ya kanuni za msingi za kushinda hofu-rika (hofu ya umri) ni kufasiri umri kama ni tarakimu tu hizo na siyo vinginevyo. Walio wengi wana sifa ya ujasiri kinadharia tu, na wanashindwa kuifasiri kwenye matendo halisi. Kushindwa huku kunatokana na kutanguliza uoga wa kuhesabu gharama, na madhara yake ni makubwa kuliko inavyofikiriwa maana uoga unaweka maslahi yako hatarini.

Uadilifu usiohojika
Usafi wa maadili ya mtu unatakiwa kuwa wa mfano kwa jamii yake, na nguvu kubwa ya mtu hutegemea kiwango chake cha uadilifu. Kamwe mwizi hawezi kumkemea mwizi mwenzake maana wote ni watuhumiwa ambao imewapasa hukumu. Unatakiwa kama mpambanaji uthibitike kujikinai na maisha ya kupita kiasi yanayohatarisha hatima na mustakabali wako, siku zote ziada ni hatarishi na kiasi ni salama. Ikiwapo ziada hofu ya haki kuhujumiwa sehemu fulani ili kupata hiyo ziada inadhihiri. Jamii yenye kiasi inaishi kwenye amani, jamii yenye tofauti ya ziada inaishi maisha hatarishi ya amani kupatikana kwa msaada wa mtutu kwa sababu ya migogoro ya maslahi. Kufanikisha maisha-adilifu yenye kiasi kunakugharimu kujinyima na kuwakana marafiki waovu.

Uwezo wa kusimamia utimilifu wa malengo
Binadamu wanatofautiana kwa uwezo wa kuhatamia malengo hadi yadhihirike. Aidha, kuna watu ambao wametabahari kwenye kutengeneza wazo lakini hawana uwezo wa kusimamia wazo hadi utimilifu wake. Halikadhalika, wapo watu waliotabahari kwenye kusimamia mafanikio ya wazo lililotengenezwa na wengine ilhali yeye huyu hana uwezo wa kutengeneza wazo. Unahitaji kutabahari na kuwa na tajiriba ya kutengeneza mawazo mengi ya kipaumbele kwa wakati mmoja, kuratibu utekelezaji wake na kuyafanikisha hatimaye, lakini pia ukisukumwa na ragba ya jamii inayokuzunguka. Hii kati ya sababu zingine, inatokana na ukweli kwamba watu wa aina hii ya uumbaji huwa hawana, kama siyo kutokujuwa, msamiati wa ‘kushindwa’

Nidhamu ya muda, rasilimali na sheria
Uthubutu huchagizwa na: kupitwa na wakati, ari/nia ya kuokoa upotevu wa rasilimali na pia dhamira-chochezi ya kuzidadisi sheria kwa malengo ya kuona km zinahakikisha usalama wa mitaji yako e.g. sheria ya uwekezaji, kodi & leseni. Sheria za nchi zikitumika visivyo inafisha dhana ya uthubutu. Uthubutu huzua maswali mengi kuliko mapendekezo na maoni. Mthubutu akiogopa maswali hatofanikisha uthubutu wake, akiondoa uoga na kukabili maswali kwa ujasiri atatuzwa pongezi na ushindi mwishoni kule.

Uwezo wa kusimamia na kudhibiti watendaji wako
Watumishi wako wana mchango mkubwa na ndiyo mikono na miguu ya kuifanya kampuni yako ifikie ndoto yake. Katika sekta binafsi, ukisimamia vizuri rasilimaliwatu wa kampuni yako, utaokoa muda mwingi wa kutafuta ufumbuzi wa kila shida mahakamani na kuepuka kuchafua jina la kampuni yako kwenye soko & tasnia. Simamia nidhamu ya kazi & uwajibikaji ili kuhakikisha tija. Wakati fulani inawezekana kupandisha tija na kurejesha nidhamu ya kazi hata bila ya kupandisha mishahara kwa sababu hakuna ushahidi wa wazi wa kisayansi kuthibitisha kwamba tija huletwa na kupandishwa mishahara tu. Ni vivyo hivyo hakuna ushahidi wa aina hiyo wa kuthibitisha kwamba kuna matokeo ya moja kwa moja kwa tija kupandishwa na nidhamu mbovu ya kazi. Katika dunia-shindani ya leo ambapo faida inatafutwa kwenye kila kazi, maslahi bora yanaletwa na jasho la kuthibitika kivitendo siyo la kuthibitika kinadharia tu.

Kuwa rafiki wa mabadiliko
Uthubutu hutegemea uwepo wa fursa za mabadiliko ambazo hizi hazionekani kirahisi japo zipo, mthubutu-mzoefu huwa na tabia ya kuwinda fursa ambazo akiziona huzikamata na kutengeneza mikakati ya kuanzisha na kutekeleza mabadiliko. Ni bahati mbaya kuwa walio wengi hawaoni fursa za mabadiliko, wanaona tu ‘kutowezekana’ ambayo hii ikitengeneza usugu ndani yao huwajengea uraibu wa hofu na uoga wa kuthubutu na kujikuta wakiishi kama tera lisiloweza mwendo hadi likokotwe tu, hali hii huwajengea "Stockholm Syndrome" (yaani unaridhika kuwa mateka wa hali inayokusibu hata kama kuna mpenyo wa kuondoka kwenye umateka huo). Watu wa kaliba hii baadhi yao ni waoga wa gharama za makosa (wanaogopa gharama za kufanya makosa ambazo hizi ndizo wanazoziona tu) hawajui kwamba kuna faida za kufanya makosa pia ambazo hizi hudhihiri baada ya kufanya makosa kwanza, hivyo ukiogopa kuthubutu eti ili usifanye makosa basi unapoteza faida ambazo ungezipata baada ya kuthubutu kufanya makosa, kwahiyo makosa ni mtaji pia. “Kumbuka kama hujawahi kufanya kosa basi hujawahi kujaribu jambo lo lote jipya, Albert Einstein.” Mwl anayekwambia usifanye hilo utakosea ni mwovu-mkuu kuliko Mwl anayekusukuma uthubutu kufanya makosa ili baadaye akusahihishe na akikusahihisha basi na wewe unakuwa Mwl kama yeye kwa wenzako. Mwalimu yupo kwa ajili ya makosa ya mwanafunzi na siyo kwa ajili ya mambo sahihi ya mwanafunzi Majwala, H. A. (1983). Kujifunza kwa makosa kwafaa zaidi ya kujifunza kwa usahihi. Uoga wa kufanya makosa ni tabia iliyowafungia wengi nje ya fursa nono, ni tabia iliyowapotezea wengi muda, ujasiri & kujiamini, mojawapo ya hatua za kutoka kwenye umaskini & unyonge ni kujijengea hulka ya uthubutu wenye tabia ya kutoogopa gharama za makosa.

Dunia hii kwa asilimia kubwa imekwamishwa na kundi la watu maskini & wanyonge wenye fikra sahihi za faida kubwa lakini wenye uoga wa kuthubutu kufanya maamuzi yatakayoachilia fikra hizo sahihi zitumike kwa faida; fikra ambazo zinasubiriwa kuokoa mustakabali wa mkwamo wa dunia. Katika kundi hili la maskini & wanyonge hawa wanaishi na utajiri mkubwa kinadharia vichwani mwao (yaani hizo fikra sahihi) kuliko utajiri wa wazi unaoonekana kwa akina Jeff Bezos ($108.9 bl), Bill Gate ($ 91.9 bl), Warren Baffet ($ 90.1 bl), Amancio Ortega ($ 75.8 bl), Mark Zuckerberg ($ 72 bl), Benard Arnault ($ 68.7 bl) na Carlos Slim Helu ($ 67.6 bl). Mungu anahusika na kuweka utajiri kwenye akili zetu, hahusiki na kutupatia utajiri mikononi mwetu.

Hata hao, kama wewe na mimi tulivyo, walikuwa na utajiri huo wote kwenye fikra zao kwanza, ndipo walipojikana na kujikinai na kutengeneza faraka na uadui dhidi ya uoga na kujijengea urafiki na dhana ya uthubutu ambapo walithubutu kuhamisha utajiri huo toka kwenye nadharia vichwani mwao kwenda kwenye uhalisia wa rasilimali zinazoonekana kwa macho. Wakati Zuckerberg amemaliza chuo kikuu na kukosa cha kufanya, aliongoza marafiki zake kuhatamia wazo la kuanzisha jukwaa litakalokutanisha watu wa dunia nzima kuwasiliana wote kwa wakati mmoja, kwa haraka na kwa gharama nafuu, wenzake waliofuzu na kutabahari kwenye taaluma ya TEKNOHAMA walikuwa wa kwanza kuona ‘kutowezekana’ na kuamua kujiondoa kwenye wazo hilo, Zuckerberg akabaki na wenzake wachache sana wakasonga mbele na wazo, baada ya mafanikio kupatikana katika hatua za awali za kutekeleza wazo lile, wale wataalam wa TEKNOHAMA waliojiondoa kwenye wazo wakarudi kubembeleza ajira. Laiti wangekubaliana na uthubutu wa Zuckerberg leo wangekuwa miongoni mwa hao matajiri saba duniani. Kuwa na kitu kunaanza na kutokuwa na kitu. Utajiri (kama siyo wa kurithi) unaanza na umaskini kwanza. Hesabu inaanza na 0 haianzi na 1. Hata 0 nayo ina thamani japo ni 0, ndiyo maana bila 0 hakuna kumi, wala mia, wala elfu, wala laki, wala milioni, wala bilioni, wala trilioni, wala quadrilioni, wala quintilioni, wala sextilioni, wala septilioni, wala octilioni, wala nonilioni, wala decilioni. Kuwa jasiri kama simba anayethubutu kumjaribu hata tembo au simba anayethubutu kumnyang’anya mamba mawindo mdomoni mwake.

Uwezo wa ushawishi
Njia nzuri kuliko zingine ya kufanikiwa katika hili ni kutumia mafanikio yaliyokwishapatikana kama kichocheo na ushahidi wa nia na ari ya kufanikisha yanayotarajiwa pia kama fursa nyingine na ushirikiano vitapatikana tena. Binadamu wamejengeka katika kuamini wanachokiona kwa macho zaidi kuliko wanachotarajia ambacho kiko kwenye nadharia kwanza. Aidha, nguvu ya ushawishi hutegemea pia kiwango cha uadilifu wa mshawishi. Walimwengu wana tabia ya kutangulia kutathmini matendo na mwenendo wa mtu kabla ya kumkubali na hapa wanatumia historia ya mtu, ndiyo maana ni muhimu kwenye maisha kama mtu unatarajia kukubaliwa na watu kwenye malengo yako ukaangalia kutengeneza historia yako vizuri ili usije kukwama (victim of circumstance-mhanga wa mazingira) mbeleni katika mipango na matamanio yako ambayo ili yafanikiwe inategemea mwitikio wa watu unaotarajia wakuvushe kwenda kwenye malengo yako.

Kwa mikono yangu na akili yangu mwenyewe.

Naomba kura yako.
 
Uthubutu hutegemea uwepo wa fursa za mabadiliko ambazo hizi hazionekani kirahisi japo zipo, mthubutu-mzoefu huwa na tabia ya kuwinda fursa ambazo akiziona huzikamata na kutengeneza mikakati ya kuanzisha na kutekeleza mabadiliko. Ni bahati mbaya kuwa walio wengi hawaoni fursa za mabadiliko, wanaona tu ‘kutowezekana’ ambayo hii ikitengeneza usugu ndani yao huwajengea uraibu wa hofu na uoga wa kuthubutu na kujikuta wakiishi kama tera lisiloweza mwendo hadi likokotwe tu. Watu wa kaliba hii baadhi yao ni waoga wa gharama za makosa (wanaogopa gharama za kufanya makosa ambazo hizi ndizo wanazoziona tu) hawajui kwamba kuna faida za kufanya makosa pia ambazo hizi hudhihiri baada ya kufanya makosa kwanza, hivyo ukiogopa kuthubutu eti ili usifanye makosa basi unapoteza faida ambazo ungezipata baada ya kuthubutu kufanya makosa, kwahiyo makosa ni mtaji pia. “Kumbuka kama hujawahi kufanya kosa basi hujawahi kujaribu jambo lo lote jipya, Albert Einstein.” Mwl anayekwambia usifanye hilo utakosea ni mwovu-mkuu kuliko Mwl anayekusukuma uthubutu kufanya makosa ili baadaye akusahihishe na akikusahihisha basi na wewe unakuwa Mwl kama yeye kwa wenzako. Mwalimu yupo kwa ajili ya makosa ya mwanafunzi na siyo kwa ajili ya mambo sahihi ya mwanafunzi Majwala, H. A. (1983). Kujifunza kwa makosa kwafaa zaidi ya kujifunza kwa usahihi. Uoga wa kufanya makosa ni tabia iliyowafungia wengi nje ya fursa nono, ni tabia iliyowapotezea wengi muda, ujasiri & kujiamini, mojawapo ya hatua za kutoka kwenye umaskini & unyonge ni kujijengea hulka ya uthubutu wenye tabia ya kutoogopa gharama za makosa.

Dunia hii kwa asilimia kubwa imekwamishwa na kundi la watu maskini & wanyonge wenye fikra sahihi za faida kubwa lakini wenye uoga wa kuthubutu kufanya maamuzi yatakayoachilia fikra hizo sahihi zitumike kwa faida; fikra ambazo zinasubiriwa kuokoa mustakabali wa mkwamo wa dunia. Katika kundi hili la maskini & wanyonge hawa wanaishi na utajiri mkubwa kinadharia vichwani mwao (yaani hizo fikra sahihi) kuliko utajiri wa wazi unaoonekana kwa akina Jeff Bezos ($108.9 bl), Bill Gate ($ 91.9 bl), Warren Baffet ($ 90.1 bl), Amancio Ortega ($ 75.8 bl), Mark Zuckerberg ($ 72 bl), Benard Arnault ($ 68.7 bl) na Carlos Slim Helu ($ 67.6 bl). Mungu anahusika na kuweka utajiri kwenye akili zetu, hahusiki na kutupatia utajiri mikononi mwetu.

Hata hao, kama wewe na mimi tulivyo, walikuwa na utajiri huo wote kwenye fikra zao kwanza, ndipo walipojikana na kujikinai na kutengeneza faraka na uadui dhidi ya uoga na kujijengea urafiki na dhana ya uthubutu ambapo walithubutu kuhamisha utajiri huo toka kwenye nadharia vichwani mwao kwenda kwenye uhalisia wa rasilimali zinazoonekana kwa macho. Wakati Zuckerberg amemaliza chuo kikuu na kukosa cha kufanya, aliongoza marafiki zake kuhatamia wazo la kuanzisha jukwaa litakalokutanisha watu wa dunia nzima kuwasiliana wote kwa wakati mmoja, kwa haraka na kwa gharama nafuu, wenzake waliofuzu na kutabahari kwenye taaluma ya TEKNOHAMA walikuwa wa kwanza kuona ‘kutowezekana’ na kuamua kujiondoa kwenye wazo hilo, Zuckerberg akabaki na wenzake wachache sana wakasonga mbele na wazo, baada ya mafanikio kupatikana katika hatua za awali za kutekeleza wazo lile, wale wataalam wa TEKNOHAMA waliojiondoa kwenye wazo wakarudi kubembeleza ajira. Laiti wangekubaliana na uthubutu wa Zuckerberg leo wangekuwa miongoni mwa hao matajiri saba duniani. Kuwa na kitu kunaanza na kutokuwa na kitu. Utajiri (kama siyo wa kurithi) unaanza na umaskini kwanza. Hesabu inaanza na 0 haianzi na 1. Hata 0 nayo ina thamani japo ni 0, ndiyo maana bila 0 hakuna kumi, wala mia, wala elfu, wala laki, wala milioni, wala bilioni, wala trilioni, wala quadrilioni, wala quintilioni, wala sextilioni, wala septilioni, wala octilioni, wala nonilioni, wala decilioni. Kuwa jasiri kama simba anayethubutu kumjaribu hata tembo au simba anayethubutu kumnyang’anya mamba mawindo mdomoni mwake.

Uwezo wa ushawishi
Njia nzuri kuliko zingine ya kufanikiwa katika hili ni kutumia mafanikio yaliyokwishapatikana kama kichocheo na ushahidi wa nia na ari ya kufanikisha yanayotarajiwa pia kama fursa nyingine na ushirikiano vitapatikana tena. Binadamu wamejengeka katika kuamini wanachokiona kwa macho zaidi kuliko wanachotarajia ambacho kiko kwenye nadharia kwanza. Aidha, nguvu ya ushawishi hutegemea pia kiwango cha uadilifu wa mshawishi. Walimwengu wana tabia ya kutangulia kutathmini matendo na mwenendo wa mtu kabla ya kumkubali na hapa wanatumia historia ya mtu, ndiyo maana ni muhimu kwenye maisha kama mtu unatarajia kukubaliwa na watu kwenye malengo yako ukaangalia kutengeneza historia yako vizuri ili usije kukwama mbeleni katika mipango na matamanio yako ambayo ili yafanikiwe inategemea mwitikio wa watu unaotarajia wakuvushe kwenda kwenye malengo yako.

Kwa mikono yangu na akili yangu mwenyewe.

Naomba kura yako.
 
Nyanja: Maendeleo ya Jamii

th

Mark Zuckerberg mmiliki wa FB
Taswira kwa hisani ya Google​

Utangulizi
Tabia ya uthubutu haikuumbiwa waoga wala wenye soni bali wajasiri, kuna usemi kuwa wenye visu vikali ndiyo wala nyama. Kule mwituni, simba angekuwa mwoga na mwenye soni njaa ingemwondoa kwenye uso wa dunia. Uthubutu unamfanya simba amjaribu hata tembo, faru na nyati. Sisimizi licha ya udogo wao kimaumbile wanao uwezo wa kumshusha tembo chini kwa sababu wana malengo ambayo lazima yatimie hata kwa kuthubutu (Fortune favours the brave. Bahati hupendelea wajasiri) na kwenye himaya ya sisimizi tembo hakai (hajikuni kwenye mti ambao ni makazi ya sisimizi). Halikadhalika, mbwea wana uthubutu na ushirikiano, wanawinda kama timu kasoro makundi maalum kama watoto na wazee, na wanagawana mawindo kwa usawa, hii ni tofauti na jamii ya simba ambapo dume ni bazazi tu mwenye kazi moja ya kuzalisha na kulinda himaya yake asiporwe majike yake.

Ujasiri wa kutenda
Wengi chini ya jua waliofanikiwa waligundua kuwa kutenda kwa ujasiri hakukwepeki katika utendaji wenye kuona mafanikio mbeleni na kudhamiria kuyapata mafanikio hayo. Macho ya wajasiri kamwe hayaoni kufeli mbele bali yanaona mafanikio tu, na roho za wajasiri haziogopi vikwazo maana wana silaha ya uthubutu. Mpiganaji aendapo vitani huwa ana uhakika wa kushinda tu, kama angejuwa hashindi asingeenda vitani. Mtaji (gharama) wa vita unatisha sana lakini faida yake ni endelevu kwa vizazi na vizazi. Aidha, wapo watu wanaotishwa na umri wao ama mdogo au mkubwa. Katika mchakato wa kutafuta maendeleo hofu ya umri wakati fulani imewafanya watu kujihukumu wenyewe kuingia kifungoni (ama kifungo cha umaskini au cha kutofanikiwa jambo lako fulani) badala ya kuwa huru. Wengi wa Walimwengu waliofanikiwa wamefanikiwa katika umri mkubwa na ni kwa sababu waliamua kwa dhati kabisa kutangaza uadui dhidi ya hofu ya rika. Mojawapo ya kanuni za msingi za kushinda hofu-rika (hofu ya umri) ni kufasiri umri kama ni tarakimu tu hizo na siyo vinginevyo. Walio wengi wana sifa ya ujasiri kinadharia tu, na wanashindwa kuifasiri kwenye matendo halisi. Kushindwa huku kunatokana na kutanguliza uoga wa kuhesabu gharama, na madhara yake ni makubwa kuliko inavyofikiriwa maana uoga unaweka maslahi yako hatarini.

Uadilifu usiohojika
Usafi wa maadili ya mtu unatakiwa kuwa wa mfano kwa jamii yake, na nguvu kubwa ya mtu hutegemea kiwango chake cha uadilifu. Kamwe mwizi hawezi kumkemea mwizi mwenzake maana wote ni watuhumiwa ambao imewapasa hukumu. Unatakiwa kama mpambanaji uthibitike kujikinai na maisha ya kupita kiasi yanayohatarisha hatima na mustakabali wako, siku zote ziada ni hatarishi na kiasi ni salama. Ikiwapo ziada hofu ya haki kuhujumiwa sehemu fulani ili kupata hiyo ziada inadhihiri. Jamii yenye kiasi inaishi kwenye amani, jamii yenye tofauti ya ziada inaishi maisha hatarishi ya amani kupatikana kwa msaada wa mtutu kwa sababu ya migogoro ya maslahi. Kufanikisha maisha-adilifu yenye kiasi kunakugharimu kujinyima na kuwakana marafiki waovu.

Uwezo wa kusimamia utimilifu wa malengo
Binadamu wanatofautiana kwa uwezo wa kuhatamia malengo hadi yadhihirike. Aidha, kuna watu ambao wametabahari kwenye kutengeneza wazo lakini hawana uwezo wa kusimamia wazo hadi utimilifu wake. Halikadhalika, wapo watu waliotabahari kwenye kusimamia mafanikio ya wazo lililotengenezwa na wengine ilhali yeye huyu hana uwezo wa kutengeneza wazo. Unahitaji kutabahari na kuwa na tajiriba ya kutengeneza mawazo mengi ya kipaumbele kwa wakati mmoja, kuratibu utekelezaji wake na kuyafanikisha hatimaye, lakini pia ukisukumwa na ragba ya jamii inayokuzunguka. Hii kati ya sababu zingine, inatokana na ukweli kwamba watu wa aina hii ya uumbaji huwa hawana, kama siyo kutokujuwa, msamiati wa ‘kushindwa’

Nidhamu ya muda, rasilimali na sheria
Uthubutu huchagizwa na: kupitwa na wakati, ari/nia ya kuokoa upotevu wa rasilimali na pia dhamira-chochezi ya kuzidadisi sheria kwa malengo ya kuona km zinahakikisha usalama wa mitaji yako e.g. sheria ya uwekezaji, kodi & leseni. Sheria za nchi zikitumika visivyo inafisha dhana ya uthubutu. Uthubutu huzua maswali mengi kuliko mapendekezo na maoni. Mthubutu akiogopa maswali hatofanikisha uthubutu wake, akiondoa uoga na kukabili maswali kwa ujasiri atatuzwa pongezi na ushindi mwishoni kule.

Uwezo wa kusimamia na kudhibiti watendaji wako
Watumishi wako wana mchango mkubwa na ndiyo mikono na miguu ya kuifanya kampuni yako ifikie ndoto yake. Katika sekta binafsi, ukisimamia vizuri rasilimaliwatu wa kampuni yako, utaokoa muda mwingi wa kutafuta ufumbuzi wa kila shida mahakamani na kuepuka kuchafua jina la kampuni yako kwenye soko & tasnia. Simamia nidhamu ya kazi & uwajibikaji ili kuhakikisha tija. Wakati fulani inawezekana kupandisha tija na kurejesha nidhamu ya kazi hata bila ya kupandisha mishahara kwa sababu hakuna ushahidi wa wazi wa kisayansi kuthibitisha kwamba tija huletwa na kupandishwa mishahara tu. Ni vivyo hivyo hakuna ushahidi wa aina hiyo wa kuthibitisha kwamba kuna matokeo ya moja kwa moja kwa tija kupandishwa na nidhamu mbovu ya kazi. Katika dunia-shindani ya leo ambapo faida inatafutwa kwenye kila kazi, maslahi bora yanaletwa na jasho la kuthibitika kivitendo siyo la kuthibitika kinadharia tu.

Kuwa rafiki wa mabadiliko
Uthubutu hutegemea uwepo wa fursa za mabadiliko ambazo hizi hazionekani kirahisi japo zipo, mthubutu-mzoefu huwa na tabia ya kuwinda fursa ambazo akiziona huzikamata na kutengeneza mikakati ya kuanzisha na kutekeleza mabadiliko. Ni bahati mbaya kuwa walio wengi hawaoni fursa za mabadiliko, wanaona tu ‘kutowezekana’ ambayo hii ikitengeneza usugu ndani yao huwajengea uraibu wa hofu na uoga wa kuthubutu na kujikuta wakiishi kama tera lisiloweza mwendo hadi likokotwe tu, hali hii huwajengea "Stockholm Syndrome" (yaani unaridhika kuwa mateka wa hali inayokusibu hata kama kuna mpenyo wa kuondoka kwenye umateka huo). Watu wa kaliba hii baadhi yao ni waoga wa gharama za makosa (wanaogopa gharama za kufanya makosa ambazo hizi ndizo wanazoziona tu) hawajui kwamba kuna faida za kufanya makosa pia ambazo hizi hudhihiri baada ya kufanya makosa kwanza, hivyo ukiogopa kuthubutu eti ili usifanye makosa basi unapoteza faida ambazo ungezipata baada ya kuthubutu kufanya makosa, kwahiyo makosa ni mtaji pia. “Kumbuka kama hujawahi kufanya kosa basi hujawahi kujaribu jambo lo lote jipya, Albert Einstein.” Mwl anayekwambia usifanye hilo utakosea ni mwovu-mkuu kuliko Mwl anayekusukuma uthubutu kufanya makosa ili baadaye akusahihishe na akikusahihisha basi na wewe unakuwa Mwl kama yeye kwa wenzako. Mwalimu yupo kwa ajili ya makosa ya mwanafunzi na siyo kwa ajili ya mambo sahihi ya mwanafunzi Majwala, H. A. (1983). Kujifunza kwa makosa kwafaa zaidi ya kujifunza kwa usahihi. Uoga wa kufanya makosa ni tabia iliyowafungia wengi nje ya fursa nono, ni tabia iliyowapotezea wengi muda, ujasiri & kujiamini, mojawapo ya hatua za kutoka kwenye umaskini & unyonge ni kujijengea hulka ya uthubutu wenye tabia ya kutoogopa gharama za makosa.

Dunia hii kwa asilimia kubwa imekwamishwa na kundi la watu maskini & wanyonge wenye fikra sahihi za faida kubwa lakini wenye uoga wa kuthubutu kufanya maamuzi yatakayoachilia fikra hizo sahihi zitumike kwa faida; fikra ambazo zinasubiriwa kuokoa mustakabali wa mkwamo wa dunia. Katika kundi hili la maskini & wanyonge hawa wanaishi na utajiri mkubwa kinadharia vichwani mwao (yaani hizo fikra sahihi) kuliko utajiri wa wazi unaoonekana kwa akina Jeff Bezos ($108.9 bl), Bill Gate ($ 91.9 bl), Warren Baffet ($ 90.1 bl), Amancio Ortega ($ 75.8 bl), Mark Zuckerberg ($ 72 bl), Benard Arnault ($ 68.7 bl) na Carlos Slim Helu ($ 67.6 bl). Mungu anahusika na kuweka utajiri kwenye akili zetu, hahusiki na kutupatia utajiri mikononi mwetu.

Hata hao, kama wewe na mimi tulivyo, walikuwa na utajiri huo wote kwenye fikra zao kwanza, ndipo walipojikana na kujikinai na kutengeneza faraka na uadui dhidi ya uoga na kujijengea urafiki na dhana ya uthubutu ambapo walithubutu kuhamisha utajiri huo toka kwenye nadharia vichwani mwao kwenda kwenye uhalisia wa rasilimali zinazoonekana kwa macho. Wakati Zuckerberg amemaliza chuo kikuu na kukosa cha kufanya, aliongoza marafiki zake kuhatamia wazo la kuanzisha jukwaa litakalokutanisha watu wa dunia nzima kuwasiliana wote kwa wakati mmoja, kwa haraka na kwa gharama nafuu, wenzake waliofuzu na kutabahari kwenye taaluma ya TEKNOHAMA walikuwa wa kwanza kuona ‘kutowezekana’ na kuamua kujiondoa kwenye wazo hilo, Zuckerberg akabaki na wenzake wachache sana wakasonga mbele na wazo, baada ya mafanikio kupatikana katika hatua za awali za kutekeleza wazo lile, wale wataalam wa TEKNOHAMA waliojiondoa kwenye wazo wakarudi kubembeleza ajira. Laiti wangekubaliana na uthubutu wa Zuckerberg leo wangekuwa miongoni mwa hao matajiri saba duniani. Kuwa na kitu kunaanza na kutokuwa na kitu. Utajiri (kama siyo wa kurithi) unaanza na umaskini kwanza. Hesabu inaanza na 0 haianzi na 1. Hata 0 nayo ina thamani japo ni 0, ndiyo maana bila 0 hakuna kumi, wala mia, wala elfu, wala laki, wala milioni, wala bilioni, wala trilioni, wala quadrilioni, wala quintilioni, wala sextilioni, wala septilioni, wala octilioni, wala nonilioni, wala decilioni. Kuwa jasiri kama simba anayethubutu kumjaribu hata tembo au simba anayethubutu kumnyang’anya mamba mawindo mdomoni mwake.

Uwezo wa ushawishi
Njia nzuri kuliko zingine ya kufanikiwa katika hili ni kutumia mafanikio yaliyokwishapatikana kama kichocheo na ushahidi wa nia na ari ya kufanikisha yanayotarajiwa pia kama fursa nyingine na ushirikiano vitapatikana tena. Binadamu wamejengeka katika kuamini wanachokiona kwa macho zaidi kuliko wanachotarajia ambacho kiko kwenye nadharia kwanza. Aidha, nguvu ya ushawishi hutegemea pia kiwango cha uadilifu wa mshawishi. Walimwengu wana tabia ya kutangulia kutathmini matendo na mwenendo wa mtu kabla ya kumkubali na hapa wanatumia historia ya mtu, ndiyo maana ni muhimu kwenye maisha kama mtu unatarajia kukubaliwa na watu kwenye malengo yako ukaangalia kutengeneza historia yako vizuri ili usije kukwama (victim of circumstance-mhanga wa mazingira) mbeleni katika mipango na matamanio yako ambayo ili yafanikiwe inategemea mwitikio wa watu unaotarajia wakuvushe kwenda kwenye malengo yako.

Kwa mikono yangu na akili yangu mwenyewe.

Naomba kura yako.
Uliyoaandika ni mema sana, sisi, hapa Abraar Bricks Nyumba kwa wote tna msemo "Dunia haikupi mafanikio, dunia inakupa fursa, vipi utazitumia kujifanyia mafanikio ni juu yako wewe mwenyewe". Kuna fursa nyingi sana tunazitangaza hapa JF kwa miaka sasa, ni wachache wanaothubutu kunyanyua hatua na kuzifatilia. Moja wapo ni hii:

Nimekueelewa mzee baba
 
Back
Top Bottom