SoC01 Uthubutu na Dhana ya Mafanikio

Stories of Change - 2021 Competition

Karanga Lawfirm

Senior Member
Feb 10, 2021
161
165
Nijambo lisilopingika kuwa mwanadamu anahitaji mafanikio. Ili kusema mtu anamafanikio lazima kuwepo kwa mabaliko chanya kwa mtu husika katika nyanja zake zote za kimaisha kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ya juu zaidi. Kumekuwa na shahuku kubwa hasa kwa vijana kutaka kufikia maisha mazuri kwa namna yoyote ile.

Mafanikio hayawezikuja bila kufanya kazi na kujaribu shughuli tofauti tofauti. Moja ya mambo yanayofanya vijana wengi kushindwa kufikia hadhima zao nipamoja na kushindwa kuthubutu kufanya shughuli mbali mbali zinazoweza kuwavusha kutoka katika hatua moja kwenda hatua nyingine. Hivi sasa kumekuwa na malalamiko mengi kwa vijana kuhusu swala la ukosefu wa ajila na ukosefu wa mitaji kwajili ya kuanzisha biashara.

Hakuna mafanikio yoyote yanaweza kutokea kwa mtu yoyote pasipo yeye mwenyewe kufungua milango ya kuanza kufanya kazi.

Mwaka 2012 kijana mmoja aliyehitimu kidato cha nne na kushindwa kufaulu masomo yake jambo lilomkwamisha kuendelea na safari yake ya kielimu. Aliamua kuanza kujifunza shughuli za utengenezaji samani ambapo aliomba kujifunza kwa fundi mkongwe wa samani kwa ada wa shilingi elfu kumi tu. Kijana alijifunza kwa bidii na baadae kujua namna ya kutengeneza samani mbali mbali. Baadae aliomba kujitegemea ili aweze kutengeneza samani zake mwenyewe pasipo usimamizi wa mtu.

Kijana alifanikiwa na kutengeneza samani mbali mbali swala ambalo lilimuwezesha kupata wateja wengi na kuuza bidhaa zake na kupata kipato chakutosha. Kijana hakuishia hapo alitanua wigo wake wa biashara kwa kujihusisha na ununuzi wa mazao mbali mbali za nafaka kama mahindi mpunga na maharage. Hili lilimfanya kijana huyo kupata pesa nyingi na zakutosha kuendesha maisha yake.

Historia ya kijana huyo kujiajili kwa kuthubutu kuanza inaonyesha ni kwanma gani mafanikio hawapo katika dhana ya maneno tu bali udhubutu wa kuamua kufanya. Hakuna mafanikio bila uthubutu.
 
Back
Top Bottom