Uteuzi wakurugenzi: Rais hakufuata sheria ya utumishi wa umma?

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,440
Uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji, wilaya, manispaa, miji unekuwa na tafrani miongoni mwa wananchi hususan kwenye mitandao kila mtu akieleza lake, kama ni makada, ni watumishi, hawana sifa, kuna upendeleo kuna ubaguzi n.k

Hivyo ni vema tukaliweka wazi kwani hawa wanaoteuliwa ni watumishi wa umma daima watatumikia umma mpaka watakapofika mwisho wa mkataba wao na sio kutenguliwa katka teuzi hizi, malalamiko hayo yanatakiwa kuzingatia yanajibu sheria ya utumishi wa umma ya 2002 na marekebisho yake ya 2009
Na sheria ya masuala ya kiutumishi ya mwaka 2007 kwani tunategemea raisi aliteua hawa MADAS NA WAKURUGENZI kwa kufuata sheria hizo kama sio yeye basi wizara ya utumishi kama walifanya kwa shinikizo bila kufuata sheria tujue.

Kama ni ajira mpya haziwezi kuanza na watu wenye vyeo vikubwa na inavyojulikana hizi sio nafasi za kuomba ni promotion hivyo ni zawadi kwa watumishi watendaji wanaotumikia wananchi kulingana na maadili ya kazi pia wenye weledi wa kutosha na wachocheaji wa maendeleo hivyo daima wanatakiwa kuwa huru kulingana na imani na dini zao.

Naomba sasa tuweke sawa juu ya uteuzi huu je umefuata sheria hizo za utumishi wa umma pia mifano.
 
Kama umeangalia kwa undani mfumo uliopo wa sheria na taratibu unachelewesha kasi ya Rais Magufuli.Alishasema yeye sio mtu wa kungojea michakato. Hivyo wakati mwingine inabidi azipinde sheria.. Suluhisho hapa ni Katiba Mpya tu..
 
Kaka mungo hayo mabadiliko yatalenga mahitaji ya magufuli na si wananchi au?
 
Kikulacho kumbe ki nguoni mwako, rafiki yako ndie adui yako, huu wimbo maupenda sana. Ukiunganisha na ule WA kampeni wa CCM utapata jibu zuri.
 
Kimsingi taratibu ndio hazikufuatwa.
Taratibu zinaelekeza kwamba ili kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa halmashauri ni lazima muhusika awe ameshafanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 12 na pia lazima awe ameshakuwa mtumishi mwandamizi hususani mkuu wa idara pamoja na elimu ya shahada ya uzamili.
Kwa ma days ni lazima awe na uzoefu wa zaidi ya miaka 12 na kuwa mtumishi mwandamizi (afisa utumishi au utawala) wizarani, mkoani ndio wengi walikuwa wanatolewa au kwenye halmashauri.
Nafasi hizo ziliondolewa kujazwa kwa watu kutoka nje ya utumishi wa umma, mabadiliko ya sheria ya utumishi wa umma yalifanyika na kufanya nafasi hizo kuwa za promotion kwa watumishi wa umma wanye utendaji mzuri.
Kitendo cha kuwaibua makada wa ccm ambao hawajawahi kamwe kufanya kazi serikalini ni kosa kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma. Na pia inawashusha mori watumishi wa umma ambao ndio walikuwa na sifa za kupewa nafasi hizo.
Namalizia kwa kusema kilichofanyika ni upuuzi na ushenzi uliopita mipaka.
 
Uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji, wilaya, manispaa, miji unekuwa na tafrani miongoni mwa wananchi hususan kwenye mitandao kila mtu akieleza lake, kama ni makada, ni watumishi, hawana sifa, kuna upendeleo kuna ubaguzi n.k

Hivyo ni vema tukaliweka wazi kwani hawa wanaoteuliwa ni watumishi wa umma daima watatumikia umma mpaka watakapofika mwisho wa mkataba wao na sio kutenguliwa katka teuzi hizi, malalamiko hayo yanatakiwa kuzingatia yanajibu sheria ya utumishi wa umma ya 2002 na marekebisho yake ya 2009
Na sheria ya masuala ya kiutumishi ya mwaka 2007 kwani tunategemea raisi aliteua hawa MADAS NA WAKURUGENZI kwa kufuata sheria hizo kama sio yeye basi wizara ya utumishi kama walifanya kwa shinikizo bila kufuata sheria tujue.

Kama ni ajira mpya haziwezi kuanza na watu wenye vyeo vikubwa na inavyojulikana hizi sio nafasi za kuomba ni promotion hivyo ni zawadi kwa watumishi watendaji wanaotumikia wananchi kulingana na maadili ya kazi pia wenye weledi wa kutosha na wachocheaji wa maendeleo hivyo daima wanatakiwa kuwa huru kulingana na imani na dini zao.

Naomba sasa tuweke sawa juu ya uteuzi huu je umefuata sheria hizo za utumishi wa umma pia mifano.
Bandiko limeshiba busara!! Ameifedhehesha jamii ya wapenda maendeleo! Uteuzi huu umeitia doa Ikulu. Binafsi siamini kama kaufanya JPM! Kahujumiwa
 
Kama umeangalia kwa undani mfumo uliopo wa sheria na taratibu unachelewesha kasi ya Rais Magufuli.Alishasema yeye sio mtu wa kungojea michakato. Hivyo wakati mwingine inabidi azipinde sheria.. Suluhisho hapa ni Katiba Mpya tu..
Wakati mwingine ni bora tuangalie kwa makini tunaposema sheria za utumishi hazikufuatwa tujiulize sheria hizo ziliwekwa na nani na kwa manufaa ya nani.Tumekwisha shuhudia mikataba ya hovyo ambayo haina hata harufu ya uzarendo ndani yake. kama wewe ni mtalamu mambo ya mikataba basi kaangalie baadhi ya ile ya madini. Serikali inalalamika, wananchi wanalalamika kwamba haiinufaishi nchi, nani aliingia mikataba hiyo?

Hata tukiangalia kwa makini sheria za utumishi tujiongeze kidogo na kutafakari kwa kina kwamba iliwekwa na akina nani na kwa manufaa ya nani. Sheria za utumishi za wakati ule wa viongozi wazarendo zilisema mtumishi akituhumiwa kuiba au kufanya kosa lolote kubwa (1) asimamishwe kazi, (2) alipwe nusu ya mshahara wake hadi mahakama itakapotoa hukumu. Akionekana hana hatia (1) alipwe mara moja ile nusu ya mshahara wake iliyobaki ofisini, (2) arejeshwe kazini mara mona na bila masharti. Hapo ni uzarento, hakuna kumuonea mtu wala kuipendelea serikali.

Leo hii kwa makosa yale yale mtumishi anasimamishwa kazi lakini (ati) analipwa mshahara wake wote. Kama mshahara wake ni milioni mbili anaendelea kulipwa wakati akiwa nyumbani kwake au hata kama anafanya shughuli zake nyingine, je huo ni uzarendo. Wakati mwingine mtumishi anafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupokea rushwa lakini cha ajabu anaendelea kuwepo kazini, yuko ofisini, analipwa mshahara wake pamoja na posho zake zote. Hizi ni sheria gani, akija Rais wa awamu ya tano akizipindisha hizi sheria zisizo hata na chembe ya uzarendo analaumiwa. Ah! Jamani. Tunamtegemea mtu atubadirishie hizi sheria zisizo na uzarendo wakati yeye mwenyewe huyo huyo yuko mahakamani kwa tuhuma za kupokea rushwa, yaani aondoe sheria inayomuweka kazini halafu itakuwaje.

Nchi hii zamani ilikuwa na kitu kikiitwa Azimio la Arusha kazi yake ilikuwa moja kubwa kwa viongozi: check and balance. Ukijikweza linakushusha, ukijishusha linakukweza. Liko wapi. Baada ya kuua Azimio ndipo sheria za kizarendo na zenyewe zikafutwa na kutungwa hizo tunazoziuona sasa. Wakati zamani kiongozi wa Umma hakuruhusiwa kufanya biashara alipewa option achague kutumikia Umma au kuendelea na biashara zake, leo kiko wapi mfanya biashara mkubwa ndiye huyo huyo mbunge na wakati mwingine ndiye huyo huyo waziri. Ukimsikiliza kwa makini hoja zake akiwa bungeni unagundua dhahiri kwamba yuko pale kulinda biashara zake, huyo huwezi kumuondoa bungeni maana ana fedha za kutosha. Sheria gani hizi. Serikali ya awamu ya tano iko kwenye mpito wakati mwingine wakikukanyaga kidole kwa bahati mbaya uwe mvumilivu kidogo kinyume cha hapo hapa tulipo hatuwezi kutoka.
 
Back
Top Bottom