magafumukama
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 743
- 198
Sheria ya nini? Sisi tunataka kazi tu. Halo ya sheria ni ya Kwenu. Kwani kuna sheria kubwa kuliko Katiba? Mbona nayo hatuiogopi? Hapa ni kazi tu!
Nivyema nafasi za wakurugenzi wapewe wenye taaluma sio makada wa vyama
Lakini unazijua sheria za utumishi wa Umma na mamlaka ya Rais kwa kila teuzi? Kama hujui utajuaje watakao kwambia kama wana kudanganya au lah?Uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji, wilaya, manispaa, miji unekuwa na tafrani miongoni mwa wananchi hususan kwenye mitandao kila mtu akieleza lake, kama ni makada, ni watumishi, hawana sifa, kuna upendeleo kuna ubaguzi n.k
Hivyo ni vema tukaliweka wazi kwani hawa wanaoteuliwa ni watumishi wa umma daima watatumikia umma mpaka watakapofika mwisho wa mkataba wao na sio kutenguliwa katka teuzi hizi, malalamiko hayo yanatakiwa kuzingatia yanajibu sheria ya utumishi wa umma ya 2002 na marekebisho yake ya 2009
Na sheria ya masuala ya kiutumishi ya mwaka 2007 kwani tunategemea raisi aliteua hawa MADAS NA WAKURUGENZI kwa kufuata sheria hizo kama sio yeye basi wizara ya utumishi kama walifanya kwa shinikizo bila kufuata sheria tujue.
Kama ni ajira mpya haziwezi kuanza na watu wenye vyeo vikubwa na inavyojulikana hizi sio nafasi za kuomba ni promotion hivyo ni zawadi kwa watumishi watendaji wanaotumikia wananchi kulingana na maadili ya kazi pia wenye weledi wa kutosha na wachocheaji wa maendeleo hivyo daima wanatakiwa kuwa huru kulingana na imani na dini zao.
Naomba sasa tuweke sawa juu ya uteuzi huu je umefuata sheria hizo za utumishi wa umma pia mifano.
who cares comment za nyumbu.hajafuata kabisa.anyway who care?ccm haiwezi kamwe kuleta maendeleo katika nchi hii.na Magufuli ndo rais wa ajabu kuwahi tokea tanzania na africa kwa ujumla.subiri tuone
Mbona hii ya sasa imekiukwa hiyo mpya itasalia sasa!Kama umeangalia kwa undani mfumo uliopo wa sheria na taratibu unachelewesha kasi ya Rais Magufuli.Alishasema yeye sio mtu wa kungojea michakato. Hivyo wakati mwingine inabidi azipinde sheria.. Suluhisho hapa ni Katiba Mpya tu..
Kuajiriwa kwa watu wenye sifa hizo je? Kama mtu alikua private sector anazo sifa hatakiwi kuajiriwa?Sheria inaelekeza kwamba nafasi za uongozi katika utumishi wa umma zinatakiwa kujazwa kwa kupandishwa vyeo watumishi wa umma waandamizi wenye utendaji mzuri wa kazi pamoja na elimu inayostahili
akizipindisha wananchi nao wazifanyeje ?Kama umeangalia kwa undani mfumo uliopo wa sheria na taratibu unachelewesha kasi ya Rais Magufuli.Alishasema yeye sio mtu wa kungojea michakato. Hivyo wakati mwingine inabidi azipinde sheria.. Suluhisho hapa ni Katiba Mpya tu..
una mimba ingine tena?who cares comment za nyumbu.
private
Elikuwaga hivyo, sheria ikabadilishwa kwa a sasa nafasi hizo zinatakiwa kujazwa na watumishi wa umma tu, haruhusiwi mtu kutoka nje ya utumishi.Kuajiriwa kwa watu wenye sifa hizo je? Kama mtu alikua private sector anazo sifa hatakiwi kuajiriwa?
Nini umuhimu wa kuwa na sheria.Kama umeangalia kwa undani mfumo uliopo wa sheria na taratibu unachelewesha kasi ya Rais Magufuli.Alishasema yeye sio mtu wa kungojea michakato. Hivyo wakati mwingine inabidi azipinde sheria.. Suluhisho hapa ni Katiba Mpya tu..
Utashi ndiyo suluhisho sio katiba mpya! Kwani katiba ya sasa inaruhusu haya!Kama umeangalia kwa undani mfumo uliopo wa sheria na taratibu unachelewesha kasi ya Rais Magufuli.Alishasema yeye sio mtu wa kungojea michakato. Hivyo wakati mwingine inabidi azipinde sheria.. Suluhisho hapa ni Katiba Mpya tu..
CCM haiwezi kuleta maendeleo ? Nchi hii ilikuwa hivi miaka 30 iliyopita ? Halafu eti nchi hii tuwakabidhi watu wapumbavu kama wewe. Haitatokea hadi dunia hii inakwishahajafuata kabisa.anyway who care?ccm haiwezi kamwe kuleta maendeleo katika nchi hii.na Magufuli ndo rais wa ajabu kuwahi tokea tanzania na africa kwa ujumla.subiri tuone
Huu ni wakati wa kuvunja, kuharibu na kubomoa uozo wote kisha kujenga nchi mpya. Keep it up JPM.Kimsingi taratibu ndio hazikufuatwa.
Taratibu zinaelekeza kwamba ili kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa halmashauri ni lazima muhusika awe ameshafanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 12 na pia lazima awe ameshakuwa mtumishi mwandamizi hususani mkuu wa idara pamoja na elimu ya shahada ya uzamili.
Kwa ma days ni lazima awe na uzoefu wa zaidi ya miaka 12 na kuwa mtumishi mwandamizi (afisa utumishi au utawala) wizarani, mkoani ndio wengi walikuwa wanatolewa au kwenye halmashauri.
Nafasi hizo ziliondolewa kujazwa kwa watu kutoka nje ya utumishi wa umma, mabadiliko ya sheria ya utumishi wa umma yalifanyika na kufanya nafasi hizo kuwa za promotion kwa watumishi wa umma wanye utendaji mzuri.
Kitendo cha kuwaibua makada wa ccm ambao hawajawahi kamwe kufanya kazi serikalini ni kosa kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma. Na pia inawashusha mori watumishi wa umma ambao ndio walikuwa na sifa za kupewa nafasi hizo.
Namalizia kwa kusema kilichofanyika ni upuuzi na ushenzi uliopita mipaka.