UTEUZI: Wakili wa LULU awa Jaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UTEUZI: Wakili wa LULU awa Jaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mizambwa, Jun 20, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Rais amteua wakili wa Lulu kuwa Jaji.
  June 20, 2012
  Posted in: Habari vyanzo mbalimbali

  Leon Bahati

  RAIS Jakaya Kikwete amemwapisha kuwa Jaji wakili wa kujitegemea, Joaquine De-Mello ambaye alikuwa akimtetea msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba.

  Wakili huyo, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King ya mwaka 2012 na ambaye alikuwa pia alikuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ni miongoni mwa majaji 10 walioapishwa jana na Rais Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  De-Mello ni miongoni mwa mawakili wanne waliojitokeza Aprili mwaka huu kumtetea Lulu katika kesi hiyo ya mauaji inayomtuhumu kumuua usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu.

  Mawakili wengine wanaomtetea Lulu ambaye umri wake umekuwa na utata ni Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Massawe.

  Akizungumza kwenye viwanja vya Ikulu, De-Mello alisema baada ya kuteuliwa kuwa Jaji, sasa atafanya kazi hiyo na moja ya mikakati yake ni kukabiliana na changamoto za wingi wa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Majaji wengine walioapishwa jana na Rais Kikwete ni Francis Mutungi, John Mgeta, Patricia Fikirini, Sam Rumanyika, Salvatory Bongole, Jerald Alex, Mathew Mwaim, Jacob Mwambegele na Latifa Mansook.
  Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alisema amefurahi kuteuliwa kwa majaji hao na anawafahamu kuwa wote ni wazoefu na watatekeleza kazi zao kikamilifu.

  "Wote ni wazoefu. Ukiangalia utaona kuwa sita walikuwa wakifanya kazi mahakamani (Mahakama Kuu na Rufani), wawili mawakili wa kujitegemea na wawili pia mawakili wa Serikali," alisema Jaji Othman.
  Alisema majaji hao wote kabla ya kupangiwa kazi rasmi itabidi waanze kufanya kazi ya kukabiliana na kesi zaidi ya 2,200 zilizopo katika Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi.

  Uteuzi wa majaji hao 10, alisema unaifanya Mahakama Kuu sasa kuwa nao 69 tofauti na wale 16 wanaounda Mahakama ya Rufani.
  Othman alisema pamoja na uteuzi huo wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kulundikana kwa kesi nyingi kuliko uwezo wao.
  "Walioteuliwa watasaidia lakini ukweli ni kwamba bado tunakabiliwa na upungufu wa majaji. Kesi ni nyingi," alisema Othman.

  Hakuweza kueleza mara moja idadi kamili ya majaji inayotakiwa ili kukidhi mahitaji lakini akasema kuwa Serikali imeliona hilo na imekuwa ikilifanyia kazi hatua kwa hatua.

  Licha ya upungufu wa majaji, Jaji Othman alisema wanakabiliwa na tatizo la kutumia teknolojia ya zamani ya kusikiliza na kuandika tofauti na maendeleo ya sasa ambayo yanahitaji kurekodi.
  "Mfumo huu wa kutumia teknolojia ya kisasa pia ungeweza kuharakisha kesi," alisema Jaji Othman lakini akasema Kitengo cha Biashara tayari kimeanza kuifanyia kazi teknolojia ya kisasa.

  Kwa kutumia teknolojia hiyo, alisema mtu anaweza kutumia simu yake ya mkononi kujua siku ya kesi yake na hata kuperuzi kwenye mtandao kupata hukumu pamoja na mwenendo wa kesi yake.
  Alisema wanatarajia kwenda hatua kwa hatua ili kuhakikisha teknolojia hiyo ya kurahisisha kazi za mahakama inaenea idara zote za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.

  Majaji wengine wapya nao walisema kwenye mahojiano na waandishi wa habari kwamba moja ya changamoto ni kufanya kazi katika mazingira magumu na wingi wa kesi zilizolundikana katika mahakama hiyo.
  Jaji Mutungi alisema yeye anaamini kiu kubwa ya Watanzania ni kupatiwa haki na kwamba haki hiyo inapocheleweshwa pia ni tatizo jingine.

  Ili kuhakikisha anawatekelezea Watanzania haki zao, Mutungi alisema atajitahidi kufanya kazi kwa bidii na kumaliza kesi nyingi kwa haraka.

  Kwa upande wake, Jaji Mgeta alisema pamoja na wingi wa kesi kazi kubwa wanayopaswa kuifanya ni kuwa waadilifu na watenda haki.

  Alikiri kwamba Tanzania wako nyuma katika teknolojia ya kuendesha kesi lakini akasema hilo halipaswi kuwa ni jambo ambalo litawafanya warudi nyuma na kutotekeleza wajibu wao kikamilifu.

  Source: Mwananchi
  ====================================================================================================

  MYTAKE: Huyu ni Wakili wa kujitegemea aliyejitolea kumsaidia LULU.
  Je, LULU anaandaliwa hukumu kama ya babu SEYA??  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  haina uhusiano wowote.
  mbona wapo mawakili wengi tu wanakuwa majaji?
  hataweza kupewa hiyo kesi na pia haruhusiwi kijuhusisha na kesi zilizo ktk chamber yake alipotoka
  na hata hivo atapangiwa mikoani na wala sio dar, akibaki dar ni coincidence tu/
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Hongera zake.
   
 4. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Hapa ingekuwa majina ya mashariki mengi Edwin Mtei tungemsikia na wengine humu jamvini pia tungewasikia lakini sasa hivi shaaaari kabisa !

  Hongereni majaji na muwe waadilifu katika kazi zenu! na msubiri MOTO mkali unaowaka KWA KUDHULUMU HAKI NA NAFSI ZA WATU KABLA HAMJARUDI KWA MUUMBA WENU! NA KAMA HAMTAKI HAYA BASI UADILIFU NA HAKI YA BINADAMU WENZENU MUIWEKE KWANZA ...
   
 5. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Unashangaza sana na kupotoka kama wengine, hivi unaujua ukweli wa babu seya au unajisemea tu? Yule mzee alitenda kweli lile kosa na kama hukumbuki jaji aliewekwa kwanza alijitoa kwa kuwa alishindwa kuendesha kesi ile kwa kuwa ilikuwa inamuuma sana kuona watoto wadogo waloambukizwa ukimwi na babu seya kwanini mnapenda kuzusha uongo mara zote, imagine mtoto wako alawitiwe na kuambukizwa ukimwi je wewe utakaa ufurahi na kuona mtuhumiwa wako anaonewa? hebu peleleza kwanza yule jaji wa kwanza mwanamke aliekuwa akiskiliza kesi ya babu seya hakujitowa? babu seya alaaniwe mpaka kifo chake! kwa kutenda udhalimu ule ! tunashukuru kwa dawa za kupunguza makali ya virusi watoto angalau wataishi japo kwa shida !
   
 6. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hongera zake!
   
 7. MKANKULE

  MKANKULE JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 422
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  CCM TUTAWAZIKA NA KUWAAGA KWA NYIMBO NYINGI ZINAZOTUMIKA MSIBANI.
  :wink2:
   
Loading...