Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya waingiliwa na wana mtandao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya waingiliwa na wana mtandao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 2, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,213
  Trophy Points: 280
  Na Saed Kubenea

  Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa Mbele


  UTEUZI wa wakuu wapya wa wilaya, uhamisho wa baadhi na kustaafishwa kwa wengine, vinadaiwa kuingiliwa na mtandao wa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, MwanaHALISI limeelezwa.

  Taarifa zinasema kati ya wakuu wa wilaya 15 walioteuliwa wengi wao ni wale wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa karibu wa kundi la Lowassa, huku wakuu wa wilaya watano walioachwa wakiwa miongoni mwa wale waliowahi kugombana naye.

  Aidha, taarifa ambazo hazikuthibitishwa zinadai kuwa inawezekana orodha ya wakuu wa wilaya iliyotangazwa ni tofauti na ile ya awali.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya wakuu wa wilaya waliotangazwa hawakuwamo katika orodha hiyo,huku wengine wakipelekwa wilaya tofauti na zile walizoarifiwa mapema kuwa watahamishiwa.

  Angalau mmoja ambaye ametajwa kupelekwa ambako alikuwa hakuandaliwa awali, ni mkuu mpya wa wilaya ya Bahi, Dodoma, Betty Mkwassa. Awali alipangwa Makete, Iringa.

  Gazeti lilipowasiliana na Betty kujua kilichotokea hadi akakwepa kwenda Makete alisema, "Kwanza, sijui kama nilikuwa nimepangiwa kwenda Maketa. Pili, sijui kilichotokea. Waulizeni wanaopanga."

  MwanaHALISI limethibitishiwa kwamba Betty alijulishwa kuwa anahamishiwa Makete, na kwamba hata Betty mwenyewe aliwahi kulalamika kwa watu kadhaa juu ya hatua hiyo.


  Walioteuliwa ambao wanatajwa kuwa wafuasi wakubwa wa Lowassa, ni pamoja na Norman Sigalla (Hai) Francis Isaac (Mbulu), Erasto Sima (Korogwe) na Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba).

  Isaac anatajwa kuwa ni mfuasi wa karibu wa kundi la mtandao maslahi, akihusishwa zaidi na mwenyekiti wa zamani wa UV-CCM Emmanuel Nchimbi.

  Isaac akiwa Katibu Mkuu wa UV-CCM, Nchimbi alikuwa mwenyekiti wa umoja huo, huku Lowassa akiwa mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini.

  Wakati mkataba wa UV-CCM na mbia wake kampuni ya M.M. Integrated Steel Mills Limited., unasainiwa, "Isaac alikuwa mtu muhimu akishika nafasi ya Mkuu wa Idara ya Fedha na Uchumi ya UV-CCM.

  Ilikuwa ni vigumu kwa kambi ya Lowassa kumuacha nje Isaac, hasa baaada ya kupoteza ukatibu mkuu," taarifa zinasema.


  Kabla ya kutangazwa kuwa mkuu wa wilaya, Isaac tayari alikuwa anachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kumiliki mali nyingi kinyume na kipato chake.

  Kangoye alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Tarime mkoani Mara. Anatajwa kuwa ni mfuasi wa karibu wa Lowassa ingawa hakuna maelezo zaidi juu ya mahusiano yao.

  Mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema uteuzi huu umeaibisha serikali.

  Alisema, "Huwezi kuteua mtu ambaye anakabiliwa na tuhuma lukuki kama hizi za matumizi mabaya ya madaraka. Basi hakukuwa hata na sababu ya kumuondoa Mnali."


  Albert Mnali alikuwa mkuu wa wilaya ya Misenyi. Aliondolewa baada ya kumuamuru askari kupiga walimu viboko.

  Kwa upande wa waliostaafishwa, wanaotajwa kuwa walikwaruzana na Lowassa, iwe hadharani au kwa siri, ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Kanali mstaafu, Peter Madaha, mkuu wa wilaya ya Muleba, Deusdedit Mtambalike na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kyera, Mashimba Mashimba.

  Kanali Madaha alikuwa mtendaji wa kwanza kumkosoa Lowassa hadharani. Akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Nyamagana mapema mwaka 2007, Kanali Madaha alimrushia kumbora Lowassa, "Usinifundishe kazi. Nimefanya kazi hii kwa zaidi ya miaka 15."


  Kuna taarifa kwamba Lowassa alizozana na Mtambalike kiasi cha kumsainisha "hati ya kumfukuza kazi." Kwa mujibu wa taarifa, Mtambalike alilazimishwa na Lowassa kusaini hati isemayo, "Kama itatokea ukafanya kosa la pili utakuwa umefutwa kazi."

  Haijafahamika Mtambalike amefanya kosa gani la pili hadi kuondolewa ukuu wa wilaya.

  Kwa upande wake, Mashimba alikosana na kundi la Lowassa baada ya kumtetea Nape Nnauye aliyepinga mkataba wa UV-CCM wa kupangisha jengo na ujenzi wa mradi katika Kiwanja Na. 108/2 barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam, kati ya UV-CCM na mbia wake unaomhusisha moja kwa moja Lowassa.

  Miongoni mwa waliobakishwa na ambao haikutegemewa wabakizwe ni Kanali Edmund Mjengwa ambaye wakati huo aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga.

  Kanali Mjengwa anatuhumiwa kuiba fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Mbarali. Wananchi wa Mbarali walifungua kesi Mahakama Kuu baada ya serikali kukataa kufanya hivyo.

  Hata hivyo, kesi hiyo ilichukuliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) lakini baadaye akaifuta.

  Mwingine ni Thomas ole Sabaya. Huyu ana tuhuma za kuandaa na kushiriki katika ukandamizaji wa haki za wananchi wa Serengeti.

  Miongoni mwa tuhuma zinazomkabili ni kuamrisha kuchoma moto nyumba za wananchi na kuhamisha zaidi ya familia 135 katika kijiji cha Nyamuma Iliyobaki, wilayani Serengeti.

  Katika uchunguzi wake, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ilibaini kuwa aliongoza kunyang'anya wananchi ardhi yao. Tume iliagiza serikali kumchukulia hatua za kisheria.

  Kutokana na hali hiyo, haikutarajiwa kuwa Rais Kikwete angembakiza katika utumishi wa umma.

  Mwingine ni Pascal Mabiti, aliyehamisha kutoka Manyoni kwenda Singida Vijijini. Mabiti akiwa mkuu wa wilaya ya Tarime, mkoani Mara, anatuhumiwa kuvunja haki za binadamu katika mahusiano yake na wananchi, hasa kuhusiana na wamiliki wa migodi ya Nyamongo wilayani Tarime.

  Ni Mabiti aliyekamata na kuweka chini ya ulinzi waandishi wa habari waliokwenda kuchimbua taarifa kuhusu unyanyasaji katika migodi hiyo.

  Tundu Lissu, wakili mahiri aliyefuatilia kwa karibu matatizo ya Migodi ya Nyamongo alipata kusema, "Tokea mwaka 2003 tuhuma za Mabiti ziko wazi. Rais alipaswa kumwambia, ‘Una tuhuma. Pengine si za kweli, lakini pengine ni za kweli. Sikutaki, utaniharibia katika serikali yangu mpya.' "

  Katika orodha hiyo, wamo Hawa Mchopa, James Yamungu na Philemon Shelutete. Wote hawa wanadaiwa kuwa wamebaki kutoka na kile kinachoitwa, "wanamtandao kuingilia kati."


  Kuna madai kwamba kati ya wakuu wa wilaya wapya 17 walioteuliwa na Kikwete mwaka 2006, saba (7) walitoka mkoa wa Arusha.

  Lakini wapo wanaodai kwamba wakuu wengi wa wilaya wakati ule, waliteuliwa au kubakishwa katika nafasi zao kutokana na shinikizo la aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa.
   
 2. n

  nzala Member

  #2
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  hakika wanamtandao ni kiboko!!!!!!!
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sasa Pinda anafanya nini?

  Ni kama Mashimba anasema hajawahi kukosana na Lowassa wala Mwakipesile. Haamini kuondolewa kwake kumetokana na hao wakuu wawili.

  Hata yeye ni kitendawili juu ya nini kimetokea mpaka akaondolewa kuwa DC. Inasemekana jina lake liliondolewa kule ofisi ya waziri mkuu. Nani aliliondoa na kwasababu zipi, mimi sijui.

  Huenda ile kufumaniwa na mwanamke kumechangia maana lile suala lilifika mbali sana mpaka tume ya maadili.

  Inaelekea Watanzania wa sasa kila utakayemteua kuna madhambi kibao nyuma yake.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Duuu,
  Naona KIHINDI-HINDI ahhhh, Kizungu-zungu.
  Na mwingine alipewa U-DC kwa sababu Mtandao ulimchukulia Mkewe.....
  Bado na Mtoto wa Kiislaam Mange Kimambi apewe u-dc kwa kupigwa na ......
   
 5. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Unajua sijui hadi sasa nashindwa kuelewa ni kwanini mambo yanaenda kienyeji tuuuuu;kama vile serikali ni mali ya mtu binafsi tena anaiendesha bila kufata taaluma na maadili ya shughuli husika?
  Hapa ndipo tunaposema serikali ya TZ ni kichwa cha mwendawazimu;ikiwezekana tubinafsishe hiki kitengo cha maadili ya viongozi na kinachoshughulika na kupanga na kupangua vyeo!!
  Tukiona inafaa tuipitishe.
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  yesu na maria ISSACK FRANCIS TENA
  KWELI JAKAYA FATAKI
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watu hawa ni hatari na watamtesa sana JK kwa kuwa wanamfahamu,kinatakina atumie njia ya Rais wa Malawi kuachana na mafisadi.
   
 8. A

  AbbyBonge Member

  #8
  Apr 2, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini jamani mbona wana mtandao wanakosoa sana kuliko kushauri au kueleza mema ambayo yamefanywa na serikali, hivi inawezekana hii serikali iwe inakosea siku zote au kila inachokifanya kipo chini ya mbinu za wana mtandao?
  ninapoisoma hiyo makala ya Mwanahalisi kwa mfano sielewi mwandishi alikuwa anataka kututahadharisha na nini?
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama 2010 mafisadi hawa watatumia mbinu hizi hizi na bila wananchi kung'amua ni bora nchi itawaliwe na DJ kama Madagasca,tumechoka na usanii uliojificha nyuma ya amani ya kimaskini.
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani Serikali inaendelea kukosea sana tu Mkuu. Inakosea zaidi inaporuhusu kuingiliwa na hao wanamtandao.

  Kuhusiana na mafunzo ya makala ya MwanaHalisi, ninachoona ni kwamba, inawezekana tunae PM anaewakilisha PM mwingine. Maana yake ni kwamba, inawezekana tukadhani kuwa Mhe. Pinda ndie PM kumbe bado EL ni PM (kwa kuwa ndie anaeendelea kufanya kazi za PM).

  Ila kubwa zaidi ni kwamba, wanamtandao wanaelekea kuwa bado wapo, na wana nguvu nyingi sana ndani ya serikali (bado wanaimiliki). Mipango hiyo ya ma-DC ni katika harakati tu za kuweka mtandao wao sawa ili uchaguzi ujao uwe wa huru na wa haki kwao kuliko kwa wengine. Kazi ipo, timu inapangwa. Piga ua matokeo ni yale yale ya 2005.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  Recta,

  ..JK ni mwanamtandao. tena alikiri mwenyewe kwamba alijipanga kwa takribani miaka 10 yeye na wanamtandao wenzake kuchukua hatamu za uongozi wa taifa letu.

  ..nadhani wanamtandao wameona kwamba kundi lao limekosa umaarufu. wameamua kulikana wenyewe kundi lao.

  ..wananchi tuwe macho, tusidanganywe na hizi propaganda za kitoto.

  ..NYOKA NI NYOKA TU, HATA AJIVUE NGOZI YAKE NA KUWA NA NGOZI MPYA.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145


  Uteuzi wake unamaanisha kuwa ameshaonekana kuwa ni safi?​
   
 13. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  wakuu wa wilaya huchaguliwa na waziri mkuu <<I THINK>>(kipindi hicho EL) then hupelekwa majina kwa prezidaa na yeye anawatangaza rasmi. So in a way haishangazi sana kuona kwa nn JK anabadiri wakuu wa wilaya, na hii sio mara yake ya kwanza! Kumbuka kwamba kama ww na JK haziivi ukuu wa wilaya anytime from now unavuliwa, na kama wewe ni mjumbe wa halmashauri kuu NEC, usishangae ukaona unapewa ubalozi sehemu fulani na uchaguzi unaitishwa chap chap na mzee makamba akasema sehemu ipo wazi kugombewa na mwanaccm yoyote lakini wao wana mtu wao in place already!
  Mabadiriko jamani ndo tunayaona leo ? Mbona yalishaanza tokea kipindi kile EL alipojiuzuru ?

  anachofanya sasa hivi JK, ni safishasafisha NEC, na safishasafisha wakuu wa wilaya(wa EL)! The dude (JK) is not smart, sema sisi tu tumekuwa somehow slow kurealize anachofanya!
   
Loading...