Uteuzi wa wakurugenzi 187 wazua hofu

MUGASHA THE HERO

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
327
204
Baada ya Rais John Magufuli kuteua wakurugenzi 187 wapya, baadhi ya wanasiasa na wanataaluma wamesema uamuzi wa kuteua makada wa CCM kushika nafasi hizo za ukurugenzi wa wilaya utaathiri Uchaguzi Mkuu ujao. Rais Magufuli, ambaye alikuwa akijielezea kuwa si mwanasiasa, juzi ameteua zaidi ya makada 30 walioshindwa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge mwaka jana, kushika nafasi hizo.

Ni wakurugenzi 65 tu waliobakizwa. Hatua hiyo ya kuteua watendaji wa wilaya kutoka miongoni mwa makada waliowahi kugombea uongozi wa kisiasa, umekuja siku chache baada ya Ofisi ya Rais-Utumishi kutangaza makada wengine kushika nafasi ya makatibu tawala wa wilaya, uteuzi ambao pia ulilalamikiwa kuwa unaingiza siasa kwenye utendaji. “Rais anajenga mfumo wake kwa kuteua watu loyal (watiifu) kwake.

Hivyo anaandaa uchaguzi wa 2020 kwa kuweka returning officers (wasimamizi) wake na bado atabadilisha maeneo mengi zaidi kuelekea huko,” amesema Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo.

Chanzo: Mwananchi
 
Hii wazo nilitaka kulileta hapa JF jana usiku nikitika nionaishe uteuzi huu na uchaguzi mkuu ujao ila nikasita nisijie itwaa mchochezi nashukuru mwananchi wameandika hii habari

Pia, nilitaka kuleta pendekezo sheria ya uchaguzi ibadilishwe kutowatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kama Maofisa wa Tume ya Uchaguzi ambapo sheria hii inawataja kama wasimamizi wa uchaguzi.
 
Hii wazo nilitaka kulileta hapa JF jana usiku nikitika nionaishe uteuzi huu na uchaguzi mkuu ujao ila nikasita nisijie itwaa mchochezi nashukuru mwananchi wameandika hii habari.
ni shida, subiri wazee wa lumumba waje watoe povu hapa
 
Kikwete mrisho Jakaya tutamkumbuka ndio atabaki kuwa rais wangu bora wa karne Tanzania hii sasa hv tutegemee ugumuu wa maisha na mauza mauza mengi ndio tanzania yetu wananchi utafikiri wako kwenye usingizi wa pono huku wanaendelea kuota
 
huu ni mwanzo tu, tutegemee vituko vya karne soon vinakuja.

Mchambuzi hapa huchambui kitu na ni kweli huu ni mwanzo tu kwani ana muda gani wa uongozi?Nae lazima ajiwekee safu ya watu wake mwenyewe watakaomrahisishia uchaguzi ujao 2015.Tena uelewe tarehe 23 mwezi huu Mungu akipenda anaenda kabidhiwa uenyekiti wa chama chao ngazi ya taifa.
 
cc..jingalao,stroke,Yehodaya,motochini,mudawote,Rutashobolwa,na vijana wote wa lumumba buk 7,kujeni huku#
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom