Uteuzi wa Wajumbe wa Kamati zote za Bunge (Orodha) - Machi 14, 2013

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
KAMATI za Bunge zimetangazwa , ambapo wajumbe wa kamati mbili zilizowahi kutuhumiwa kwa rushwa, wamesambaratishwa.

Kwa mujibu wa orodha mpya ya wajumbe wa kamati hizo iliyotolewa jana na Ofisi ya Bunge, Kamati ya Hesabu za Serikali na ya Nishati na Madini zilizopata kutuhumiwa kwa rushwa, zimesambaratishwa.

Mbali na hatua hiyo, kwa maana ya wajumbe wake kusambazwa katika kamati zingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, amepangwa kupambana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, John Cheyo.

Kusambaratishwa

Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa na wajumbe 25 ambao baadhi walituhumiwa kupokea rushwa ili kukwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, imebakiwa na wajumbe watatu wa zamani.

Katika Kamati iliyopita, wajumbe walikuwa Selemani Zedi, aliyekuwa Mwenyekiti, Diana Chilolo, Makamu Mwenyekiti na John Mnyika.

Wengine walikuwa Yusuph Haji Khamis, Mariam Kisangi, Catherine Magige, Abia Nyabakari, Charles Mwijage, Yussuph Nassir, Christopher ole Sendeka, Dk Festus Limbu, Shaffin Sumar, Lucy Mayenga na Josephine Chagula.

Wengine ni Mwanamrisho Abama, David Silinde, Suleiman Nchambi Suleiman, Kisyeri Chambiri, Munde Abdallah, Sara Msafiri, Vicky Kamata, Mbarouk Ali, Athuman Mfutakamba na Pamela Palangyo.

Kwa sasa inaundwa na wajumbe wachache kuliko iliyopita akiwamo Victor Mwambalaswa, Saleh Pamba, David Silinde, Martha Mlata, Devotha Likokola, Raya Khamis, Murtaza Mangungu na Juma Njwayo.

Wengine ni Jerome Bwanausi, Richard Ndassa, Anne Kilango, Herbert Mntangi, Shaffin Sumar, Yussuf Haji Khamis na Riziki Lulida na wa zamani Chagula, Charles Mwijage na Mariam Kisangi.


Kamati ya Mrema

Kamati nyingine iliyosambaratishwa ni ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambapo wajumbe walioteuliwa ni Deusderius Mipata, Filikunjombe, Asha Jecha na Lucy Owenya.

Wengine ni Esther Matiko, Cheyo, Zitto, Zainab Vulu, Ally Keissy, Zainab Kawawa, Kheri Ali Khamis, Faida Mohamed Bakari, Ismael Aden Rage, Modestus Kilufi, Abdul Marombwa, Gaudence Kayombo, Kombo Khamis Kombo na Catherine Magige.

Wajumbe wa zamani walikuwa Augustine Mrema, aliyekuwa Mwenyekiti, Iddi Azzan, Makamu Mwenyekiti; Riziki Saidi Lulinda, Zabein Mhita na Godfrey Zambi.

Wengine ni Subira Mgalu, Hasnain Murji, Susan Kiwanga, David Kafulila, Omary Badwel, Abdul Mteketa, Tauhida Nyimbo, Joseph Selasini, Kuruthum Mchuchuli, Maida Abdalah, Dk Cyril Chami.

Kamati hiyo, katika mikutano ya Bunge iliyopita, wajumbe wake walituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa huku mjumbe wake ambaye ni Mbunge wa Bahi, Badwel, akipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kupokea rushwa na kesi yake bado inaendelea.

Aidha, katika orodha hiyo mpya, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto na Makamu wake, Filikunjombe, wameingizwa kwenye Kamati ya Hesabu za Serikali ambayo aliyekuwa Mwenyekiti wake, Cheyo anaendelea kuwa kwenye Kamati.

Kutokana na mabadiliko hayo, katika uchaguzi wa viongozi wa kamati hizo unaotarajiwa kufanyika leo, mchuano mkali utakuwa baina ya Zitto na Cheyo katika nafasi ya uenyekiti kutokana na taratibu zilizopo kuonesha kuwa Kamati hiyo, huongozwa na mbunge kutoka chama cha upinzani.

Aidha, katika orodha hiyo inaonesha kuwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Kilango, ameondolewa kwenye Kamati hiyo na kuingizwa Kamati ya Nishati na Madini ambayo wajumbe wake wa awali 25, takribani wote isipokuwa wanne wamehamishiwa kamati zingine.

Chanzo: HabariLeo | Mwandishi: Halima Mlacha | Machi 15, 2013


ORODHA YA UTEUZI WA WAJUMBE WA KAMATI ZA BUNGE

Kwa Mamlaka aliyopewa Spika na kanuni ya 113 ya Kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007, uteuzi wa wajumbe wa kamati kwa kipindi kilichobaki cha uhai wa Bunge hili sasa umekamilika kama ilivyo kwenye orodha.

Madhumuni ya kuwapanga upya waheshimiwa Wabunge kwenye kamati mbalimbali ni kuwapatia fursa wabunge kadri inavyowezekana kujipatia ujuziu na uzoefu wa shughuli za Kamati tofauti na pia kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kanuni za 113 (5)

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 14 Machi, 2013, na kesho saa sita mchana tarehe 15 Machi, 2003 ni uchaguzi wa Wenyeviti wa kamati hizo katika kumbi mbalimbali zinavyoonyesha .

Imetolewa na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
14 MACHI, 2013

Uk. 2 wa kurasa 18
KAMATI YA KANUNI ZA BUNGE
_____________________
1 Mhe. Anne Semamba Makinda, MB (Spika)
2)Mhe. Job Yustino Ndugai, MB (N/Spika)
3)Mhe. Tundu Antiphas Mughway Lissu, Mb
4)Mhe. Andrew John Chenge, Mb
5) Mhe. Musa Azzan Zungu,Mb
6 Mhe. Dkt.Titus Mtengeya Kamani, Mb
7 Mhe. Jenista Joakim Mhagama, Mb
8 Mhe. William Mganga Ngeleja, Mb.
9 Mhe. Amina Abdallah Amour, Mb
10 Mhe. James Francis Mbatia, Mb
11 Mhe. Hamad Rashid Mohammed, Mb
12 Mhe. Jasson Samson Rweikiza, Mb
13 Mhe. Philapa Godifrey Mturano, Mb
14 Mhe. Anna Margareth Abdallah,Mb
15 Mhe. Christopher Ole-Sendeka, Mb

Uk. 3 wa kurasa 18
KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE
_____________________
1.Mhe. Augustino Lyatonga Mrema, Mb
2.Mhe. Riziki Omar Juma, Mb
3.Mhe. Assumpter Nshunju Mshama, Mb
4.Mhe. Brig. Gen. Hassan Athuman Ngwilizi, Mb
5.Mhe. Agripina Zaituni Buyogera, Mb
6.Mhe. Said Juma Nkumba, Mb
7.Mhe. John Paul Lwanji, Mb
8. Mhe. Mch. Israel Yohana Natse, Mb
9.Mhe. Capt. John Zefania Chiligati, Mb
10.Mhe. Betty Eliezer Machangu, Mb
11.Mhe. Said Amour Arfi, Mb
12.Mhe. Gosbert Begumisa Blandes, Mb
13.Mhe. Augostino Manyanda Masele, Mb
14.Mhe. Dkt. Lucy Sawere Nkya, Mb
15.Mhe. Rashid Ali Abdallah, Mb

Uk. 4 wa kurasa 18
KAMATI YA MASUALA YA UKIMWI
______________________
1 Mhe. Said Suleiman Said,Mb
2 Mhe.Ahmed Ali Salum,Mb
3 Mhe. Maida Hamad Abdallah,Mb
4 Mhe.Lediana Mafuru Mung'ong'o ,Mb
5 Mhe. Maria Ibeshi Hewa, Mb
6 Mhe. Chiku Aflah Abwao, Mb
7 Mhe.Omary Ahmad Badwel, Mb
8 Mhe. Mbarouk Salim Ali, Mb
9 Mhe. Rashid Ali Omar, Mb
10 Mhe. Lameck Okambo Airo, Mb
11Mhe. Lucy Thomas Mayenga, Mb
12 Mhe. AnaMaryStella John Mallac, Mb
13 Mhe. Mch. Luckson Ndaga Mwanjale, Mb
14 Mhe. Mwanamrisho Taratibu Abama, Mb
15 Mhe.Diana Mkumbo Chilolo, Mb
16Mhe. Ignus Aloyce Malocha, Mb
17 Mhe. Saidi Ally Selemani Bungara, Mb
18 Mhe. Iddi Mohamed Azzan, Mb
19Mhe. Neema Mgaya Hamid Mb
20 Mhe. Sara Msafiri Ally, Mb
21 Mhe. Dkt. Engelbert Faustine Ndugulile, Mb
22Mhe. Maulidah Anna Valerian Komu Mb

Uk. 5 wa kurasa 18
KAMATI YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
__________________
1 Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Mb
2 Mhe. Anastazia James Wambura, Mb
3 Mhe.John Magale Shibuda, Mb
4 Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa, Mb
5 Mhe. Muhammad Ibrahimu Sanya, Mb
6 Mhe. Leticia Mageni Nyerere, Mb
7 Mhe.Thuwayba Idrisa Muhamed, Mb
8 Mhe. Susan Anselm Jerome Lymo, Mb
9 Mhe.Faith Mohamed Mitambo,Mb
10 Mhe.Juma Selemani Nkamia, Mb
11 Mhe. Betty Eliezer Machangu, Mb
12 Mhe. Selemani Saidi Jafo,Mb
13 Mhe. Mussa Azzan Zungu,Mb
14 Mhe.Salim Hemed Khamis,Mb
15 Mhe. Eng. Yussuf Hamad Masauni,Mb

Uk. 6 wa kurasa 18
KAMATI YA BAJETI
____________________
1Mhe. Andrew John Chenge, Mb
2Mhe. Christine Mughway Lissu,Mb.
3Mhe. Kidawa Hamid Saleh,Mb
4Mhe. Mansoor Shaniff Hiran, Mb
5Mhe. Saada Mukya Salum, Mb
6Mhe. Amina Abdallah Amour, Mb
7 Mhe. Joseph Roman Selasini, Mb
8Mhe. Josephat Sinkamba Kandege,Mb
9Mhe. Dkt. Cyril August Chami,Mb
10Mhe. Dkt. Bulugu FetusLimbu,Mb
11Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Mb
12Mhe. Assumpter N. Mshama,Mb
13Mhe.James Francis Mbatia, Mb
14Mhe. Beatrice Matumbo Shellukindo, Mb1
5 Mhe. Hamad Rashid Mohamed, Mb

Uk. 7 wa kurasa 18
KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA
____________________________________________
1 Mhe . Abas Zuberi Mtemvu, Mb
2 Mhe. Tundu Antiphas Mughway Lissu, Mb
3 Mhe. Gosbert Bagumisa Blandes
4 Mhe. Pindi Hazara Chana,Mb
5 Mhe. Nimrod Elirehema Mkono,Mb
6 Mhe. Felix Francis Mkosamali,Mb
7 Mhe. Nyambari Chacha Mariba Nyangwine, Mb
8 Mhe. Fakharia Khamis Shomari, Mb
9 Mhe. Rukia Kassim Ahmed, Mb
10 Mhe. Jaku Hashim Ayoub, Mb
11 Mhe. Mustapha Boay Akunaay, Mb
12 Mhe. Ramadhan Haji Saleh, Mb
13 Mhe. Jasson Samson Rweikiza, Mb
14 Mhe. William Mganga Ngeleja,Mb
15 Mhe. Deogratias Aloyce Ntukamazina , Mb
16 Mhe. Ali Khamis Seif, Mb
17 Mhe. Mariam Reuben Kasembe, Mb
18 Mhe. Abdallah Sharia Ameir, Mb
19 Mhe. Halima James Mdee, Mb

Uk. 8 wa kurasa 18
KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA
1 Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa,Mb
2 Mhe. Eng. Habib Juma Mnyaa, Mb
3 Mhe. Margaret Agness Mkanga,Mb
4 Mhe. Haji Khatib Kai,Mb
5 Mhe.Ester Lukago Minza Midimu,Mb
6 Mhe. Hassein Nassor Amar,Mb
7 Mhe. Ahmed Juma Ngwali, Mb
8 Mhe. Luhaga Joelson Mpina Mb
9 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani, Mb
10 Mhe. Joyce John Mukya, Mb1
1 Mhe. David Zakaria Kafulila, Mb
12 Mhe. Shawana Bukhet Hassan,Mb
13 Mhe. Said Mussa Zubeir, Mb
14 Mhe. Vicky Pascal Kamata, Mb
15 Mhe. Naomi Ami Mwakyoma Kaihula,Mb
16 Mhe.Khatibu Said Haji,Mb
17 Mhe. Freeman Aikael Mbowe, Mb
19 Mhe.Amina Mohamed Mwidau,Mb
20 Mhe. Josephine Jonson Genzabuke, Mb
21 Mhe. Dunstun Luka Kitandula,Mb
22 Mhe. Mohamed Hamis Misanga, Mb

Uk. 9 wa kurasa 18
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA
____________________
1 Mhe. Brig.Gen. Hassan Athumani Ngwilizi,Mb
2 Mhe. Anna Margreth Abdallah,Mb
3 Mhe. Dkt. Muhamed Seif Khatib, Mb
4 Mhe. Capt. John Zefania Chiligati, Mb
5 Mhe. Augustino Manyanda Masele, Mb
6 Mhe. Masoud Abdallah Salim, Mb
7 Mhe. Mussa Hassan Mussa, Mb
8 Mhe. Omar Rashid Nundu,Mb
9 Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya, Mb
10 Mhe. Cynthia Hilda Ngoye, Mb
11 Mhe. Henry Daffa Shekiffu, Mb
12 Mhe.Vita Rashid Mfaume Kawawa, Mb
13 Mhe. David Mciwa Mallole,Mb
14 Mhe. Hamad Ali Hamad, Mb
15 Mhe. Rachel Mashishanga Robert, M
b16 Mhe. Dkt. Augustino Lyatonga Mrema, Mb
17 Mhe. Vincent Josephat Nyerere, Mb

Uk. 10 wa kurasa 18
KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII
________________________
1 Mhe.Fatuma Abdallah Mikidadi, Mb
2 Mhe. Ritta Louise Mlaki, Mb
3 Mhe. Riziki Omari Juma, Mb
4 Mhe. Salome Daudi Mwambu, Mb
5 Mhe. Ali Juma Haji, Mb
6 Mhe. Faki Haji Makame, Mb
7 Mhe. Margareth Simwanza Sitta, Mb
8 Mhe. Ezekia Dibogo Wenje, Mb
9 Mhe. Agripina Zaituni Buyogera, Mb
10 Mhe. Juma Sururu Juma, Mb
11 Mhe. Mch. Dkt. Getrude Pangalile Rwakatare, Mb
12 Mhe. Abia Muhama Nyabakari, Mb
13 Mhe. Zabein Mhaji Mhita,Mb
14 Mhe. Mohamed Gulam Dewji, Mb
15 Mhe. Dkt. Anton Gervas Mbasa, Mb
16 Mhe. Steven Hilari Ngonyani,Mb
17 Mhe. Martha Jachi Umbulla, Mb
18 Mhe. Prof. Kulikoyela Kanalwanda Kahigi, Mb
19 Mhe. Asnain Muhamed Murji, Mb
20 Mhe. Cecilia Daniel Paresso, Mb
21 Mhe. Abdulaziz Muhamed Aboud, Mb

Uk. 11 wa kurasa 18
MAENDELEO YA JAMII
________________________
1 Mhe. John Damiano Komba, Mb
2 Mhe. Moza Abedi Saidy,Mb
3 Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi, Mb
4 Mhe. Mohamed Said Mohammed, Mb
5 Mhe. Nasib Suleiman Omar, Mb
6 Mhe. Mustafa Haidi Mkulo,Mb
7 Mhe. Jenista Joakim Mhagama, Mb
8 Mhe. Salum Halfan Barwany,Mb
9 Mhe. Kiumbwa Makame Mbaraka
10 Mhe. Salvatory Naluyaga Machemuli,Mb
11 Mhe. Livingstone Joseph Lusinde, Mb
12 Mhe. Saidi Mohamed Mtanda,Mb
13 Mhe. Agness Elias Hokororo, Mb
14 Mhe. Godbless Jonathan Lema, Mb
15 Mhe.Mary Pius Chatanda, Mb
16 Mhe.Juma Othman Ali, Mb
17 Mhe. Jaddy Simai Jaddy, Mb
18 Mhe. Dkt. Maua Abeid Daftar, Mb
19 Mhe. Albert Obama, Ntabaliba, Mb
20 Mhe.Rose Kamili Sukum, Mb
21 Mhe.Rosemary Kasimbi Kirigini, Mb

Uk. 12 wa kurasa 18
KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI
_________________________________
1.Mhe. Prof. David Homeli Mwakyusa, Mb
2.Mhe. Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mb
3.Mhe. Asaa Othman Hamad, Mb
4.Mhe. Abdulsalaam Selemani Ameir, Mb
5.Mhe. Said Juma Nkumba, Mb
6.Mhe. Abdllah Haji Ali, Mb
7.Mhe. Haji Juma Sereweji,Mb
8.Mhe. Lolensia Masele Bukwimba, Mb
9.Mhe. Mch. Peter Simon Misigwa, Mb
10.Mhe. Prof. Peter Mahmudu Msolla, Mb
11.Mhe. Nameloki Edward Moringe Sokoine, Mb
12.Mhe. Dkt. Lucy Sawere Nkya, Mb
13.Mhe. Sylvestry Francis Koka, Mb
14.Mhe. Kheri Khatib Ameir, Mb
15.Mhe.Meshack Jeremia Opulukwa,Mb
16.Mhe. Philemon Kiwelu Ndesamburo, Mb
17.Mhe. Jitu Vrajlal Soni, Mb
18.Mhe. Sadifa Juma Khamis, Mb
19.Mhe.Donald Kelvin Max, Mb
20.Mhe. Moshi Selemani Kakoso, Mb
21.Mhe. Subira Khamis Mgalu, Mb
22.Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya, Mb

Uk. 13 wa kurasa 18
KAMATI YA MIUNDOMBINU
_____________________
1 Mhe. Peter Joseph Serukamba, Mb
2 Mhe. Maryam Salum Msabaha, Mb
3 Mhe. Clara Diana Mwatuka, Mb
4 Mhe. Zamda Shamte Madabida, Mb
5 Mhe. Innocent Edward Kalogeris, Mb
6 Mhe. Hussein Mussa Mzee, Mb
7 Mhe. Aliko Nikusuma Kibona, Mb
8 Mhe. Said Ramadhani Bwanamdogo, Mb
9 Mhe. Zahra Ali Hamad, Mb

10 Mhe. Ahmed Mabkhut Shabiby,Mb
11 Mhe. Dkt. Pudenciana Wilfred Kikwembe, Mb
12 Mhe.Mussa Haji Kombo, Mb
13 Mhe. Prof. Juma Athuman Kapuya, Mb
14 Mhe. Mtutura Abdallah Mtutura, Mb
15 Mhe. Abdul Rajab Mteketa, Mb
16 Mhe. Suleiman Masoud Nchambi, Mb
17 Mhe. Saidi Amour Arfi, Mb
18 Mhe. Eng. Ramo Matala Makani, Mb
19 Mhe. Rebecca Michael Mngodo, Mb
20 Mhe. Elizabeth Nkunda Batenga, Mb

Uk. 14 wa kurasa 18
KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI
___________________
1 Mhe. Deusiderius John Mipata, Mb
2 Mhe. Deo Haule Filikunjombe, Mb
3 Mhe. Asha Mshimba Jecha, Mb
4 Mhe. Lucy Philemon Owenya, Mb
5 Mhe.Ester Nicholas Matiko, Mb
6 Mhe. John Momose Cheyo, Mb
7 Mhe. Kabwe Zitto Zuberi, Mb
8 Mhe.Zainab Matitu Vulu, Mb
9 Mhe. Ally Keissy Mohamed, Mb
10 Mhe. Zainab Rashid Kawawa, Mb
11 Mhe. Kheri Ali Khamis, Mb
12 Mhe. Faida Mohamed Bakari, Mb
13 Mhe. Ismael Aden Rage,Mb
14 Mhe.Modestus Dickon Kilufi, Mb
15 Mhe. Abdul Jabir Marombwa, Mb
16 Mhe.Gaudence Casssian Kayombo, Mb
17 Mhe. Kombo Khamis Kombo, Mb
18 Mhe. Catherine Valentine Magige, Mb

Uk. 15 wa kurasa 18
KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA
_______________________________________
1 Mhe. Tauhida Cassian Galosi Nyimbo, Mb
2 Mhe. Dunstan Daniel Mkapa, Mb
3 Mhe. Azza Hillal Hamad, Mb
4 Mhe. Yahya Kassim Issa, Mb
5 Mhe. Menrad Lutengano Kigola,Mb
6 Mhe. Bahati Ali Abeid, Mb
7 Mhe. Kulthum Jumanne Mchuchuli, Mb
8 Mhe. Rajab Mbarouk Mohammed,Mb
9 Mhe. Yusuph Abdallah Nassir, Mb
10 Mhe. Philipa Geofrey Mturano, Mb
11 Mhe. Eustas Osler Katagira, Mb
12 Mhe. Muhonga Said Ruhwanywa, Mb
13 Mhe. Munde Tambwe Abdallah, Mb
14 Mhe. Ezekiel Magolyo Maige,Mb
15 Mhe. Mch. Israel Yohana Natse, Mb
16 Mhe. Alfaxard Kange Lugola, Mb
17 Mhe. Felista Aloyce Bura, Mb
18 Mhe.Suleiman Jumanne Zedi, Mb


Uk. 16 wa kurasa 18
KAMATI YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
_________________________
1 Mhe. John Paul Lwanji,Mb
2 Mhe. Hamis Andrea Kigwangalla,Mb
3Mhe.Godfrey Weston Zambi, Mb
4 Mhe. Highness Samson Kiwia, Mb
5 Mhe. Benardetha Kasabago Mushashu, Mb
6 Mhe. Asha Mohamed Omari, Mb
7 Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, Mb
8 Mhe. Rosweeter Faustine Kasikila, Mb
9 Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka, Mb
10 Mhe. Eugen Elishininga Mwaiposa, Mb
11 Mhe. Rashid Ali Abdallah, Mb
12 Mhe. Eng. Athuman Rashid Mfutakamba, Mb
13 Mhe.Pauline Gekul,Mb
14 Mhe. Sabreena Hamza Sungura,Mb
15 Mhe. Mkiwa Adam Kimwanga, Mb
16 Mhe.Mariam Salum Mfaki, Mb
17 Mhe. Moses Joseph Machali, Mb
18 Mhe. Sylvester Masele Mabumba,Mb

Uk. 17 wa kurasa 18
KAMATI YA NISHATI NA MADINI
__________________________
1 Mhe. Victor Kilasile Mwambalaswa, Mb
2 Mhe. Saleh Ahmed Pamba, Mb
3 Mhe. Josephine Tabitha Chagulla Mb
4 Mhe. David Ernest Silinde, Mb
5 Mhe. Martha Moses Mlata, Mb
6 Mhe. Devotha Mkuwa Likokola, Mb
7 Mhe. Raya Ibrahim Khamis, Mb
8 Mhe. Mariam Nassor Kisangi, Mb
9 Mhe.Murtaza Ally Mangungu, Mb
10 Mhe. Juma Abdallah Njwayo, Mb
11 Mhe. Jerome Dismas Bwanausi, Mb
12 Mhe. Richard Mganga Ndassa Mb
13 Mhe. Anne Kilango Malecela , Mb
14 Mhe. Charles John Paul Mwijage, Mb
15 Mhe. Herbert James Mntangi, Mb
16 Mhe. Shaffin Ahmedali Sumar, Mb
17 Mhe. Yussuf Haji Khamis, Mb
18 Mhe. Riziki Saidi Lulida, Mb

Uk. 18 wa kurasa 18
KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA
_________________________________
1. Mhe. James Daud Lembeli, Mb
2. Mhe. Abdulkarim Esmail Hassan Shah, Mb
3. Mhe. Sylvester Mhoja Kasulumbayi,Mb
4. Mhe. Zakia Hamdani Meghji,Mb
5. Mhe. Susan Limbweni Aloyce Kiwanga,Mb
6. Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa, Mb
7. Mhe. Muhamad Amour Chomboh, Mb
8. Mhe. Waride Bakar Jabu, Mb
9. Mhe. Kaika Saning'o Telele, Mb
10. Mhe. Amina Andrew Clement,Mb
11. Mhe. Ester Amos Bulaya, Mb
12. Mhe. John John Mnyika, Mb
13. Mhe. Michael Lekule Laizer, Mb
14. Mhe. Mwanakhamis Khasim Said, Mb
15. Mhe. Salim Hemed Khamis, Mb
16. Mhe. Al-Shymaa Kwegyr, Mb
17. Mhe. Grace Sindato Kiwelu, Mb
18. Mhe. Salim Abdullah Turky, Mb
19. Mhe. Abuu Hamoud Juma, Mb
20. Mhe. Kisyeri Werema Chambiri, Mb

Angalizo:
Let's the conspiracy begin
 
Kamati ya nishati na madini ni muhimu sana ila imepewa watu ambao wengi hawaendani na umuhim huo.

Kamati ya serikali za mitaa na tawala za mikoa nayo wajumbe wake sioni mantiki yake

Kamati ya haki ,kinga na madaraka ya bunge , inapaswa kuwa balanced na sio kujaza wabunge wengi wa CCM na wakati huo hii ni kama mahakama ya nidham za wabunge, sasa kutokana na ushindani wa kisiasa uliopo hawatawatendea haki wabunge wa vyama vinine kutokana na ukweli kuwa maamuzi yake yanafanywa kwa kura , sasa haki itatokea wa
Hapo?

Hivi Joshua Nassari yuko kamati gani, Ndesamburo yuko kamati gani ........aliyeona majina yao tafadhali.

Hivi ile kamati ya Afriika mashariki mbona sijaiona tena humu au Supika alitudanganya watanzania?
 
Hivi kutangaza kamati leo na kesho kufanyika uchaguzi , wale walioko JKT hawatapata fursa za kushiriki kwenye kugombea ama kuchagua wenyeviti wa kamati hizo? ...........Zitto kawekwa na Cheyo ....what does this mean? .....
 
Chadema inaitesa sana ccm, dawa ni kuwazibiti!

Sizani kama watafanikiwa..
Moto wa cdm ni hatari kwa ccm! Mpaka wanatafuta kila mbinu ya kuwazibiti!
Mungu yupo tutafanikiwa hata wakiwadhibiti sisi hatuko tayari tena kuipenda ccm kwa maovu yao..
 
Hivi kutangaza kamati leo na kesho kufanyika uchaguzi , wale walioko JKT hawatapata fursa za kushiriki kwenye kugombea ama kuchagua wenyeviti wa kamati hizo? ...........Zitto kawekwa na Cheyo ....what does this mean? .....

wasipige kampeni mbaya, leo mchana wabunge wa CCM wamekaa kupitisha nani wamchague hasa kwenye zile kamati zinazotakiwa kuongozwa na upinzani, kwa ile ya hesabu za serikali watapitisha jina la CHEYO lakini wabunge wataasi na kumchagua zitto.
 
Huyu spika yupo bias kwenye kupanga hizi kamati iweje Waziri kivuli anaehusika na NISHATI NA MADINI(JOHN MNYIKA)asiwekwe kwenye Kamati ambayo inamuhusu na anayoifanyia kazi!!Kiukweli MNYIKA anamnyima usingizi huyu Mama ndomana anakuwa na kinyongo nae.
 
wasipige kampeni mbaya, leo mchana wabunge wa CCM wamekaa kupitisha nani wamchague hasa kwenye zile kamati zinazotakiwa kuongozwa na upinzani, kwa ile ya hesabu za serikali watapitisha jina la CHEYO lakini wabunge wataasi na kumchagua zitto.

Ukipitia majina ya wajumbe wa hiyo kamati ninayeona mwenye kuweza kuasi kwa upande wa CCM ni mmoja tuu Deo , ila wengine ni wale wa kuamrishwa tuu na sio vinginevyo.....lets wait and see......
 
Tanzania tuna bahati mbaya sana. Ukiangalia muundo wa hizi kamati unaona kabisa huu ni utani, na kama si utani umbumbumbu, na kama si umbumbumbu basi hawa wakubwa wamekusudia kuona hii nchi inaenda kuzimu!

1.Utangulizi wa huu uteuzi unasema hivi, "Madhumuni ya kuwapanga upya waheshimiwa Wabunge kwenye kamati mbalimbali ni kuwapatia fursa wabunge kadri inavyowezekana kujipatia ujuziu na uzoefu wa shughuli za Kamati tofauti na pia kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na kanuni za 113 (5)"

Nijuavyo mimi, hakuna mbunge asiye na taaluma au ujuzi katika nyanja fulani. Hakuna. Wapo wachumi, madktari wa binadamu na mifugo, wauguzi (nurses), waalim, wanasheria, wafanyabiashara (hata wa maji), wanamuziki (including bongo flava - wapo), n.k.

Huu uzoefu na ujuzi anaosema Spika ni wa kitu gani? Bunge ni miaka 5, lakini huu si muda mrefu kwa mtu kujifunza na kutenda. Bunge limegeuzwa chuo? Walifuata nini bungeni kama hawana ujuzi? Na kwanza ni ujuzi gani maana bungeni wanajadili sekta ambazo ndizo walizokuwa wanatumikia uraiani?

2. Kama sikosei kuna wabunge zaidi ya 320. Ukiondoa mawaziri, Spika na Naibu wake, bado utakuwa na wabunge walau 280. Hivi kuna sababu gani ya kumeweka mbunge kwenye kamati mbili (2) tofauti wakati? Kwanini wasipunguze idadi ya wabunge kwenye kamati ili kuhakikisha mbunge anakuwa na kazi ya kuisamamia serikali kwenye sekta moja tu?

Mfano: Kuna kamati zina wajumbe 22, nyingine 19! Kwanini wasiunde kamati za wajumbe kumi kumi ili kuhakikisha mbunge anakuwa anajikita kwenye sekta moja? Busara ya kawaida kabisa inasema ukiwa na kundi la watu wachache ni rahisi kusikilizana na kila mtu atapata muda wa kutoa michango yake.

3. Lakini la muhimu, ambalo nadhani bunge na hasa Spika anaonekana kutoleta 'new thinking' ni huu mtindo wa kupachika watu kwenye mambo ambayo hawana taaluma nayo. Tumeona serikalini watu jinsi kulivyo na mis-match. Na bunge wanaonekana ku-copy & paste huu mfumo (mbaya).

Kama nilivyosema awali, wabunge wote wana taaluma zao. Spika na washauri wake wameshindwa kuona umuhimu wa kutumia TAALUMA za wabunge kwa kuwaweka kwenye sekta ambazo wana ujuzi nazo? Kwa mfano, unampa uenyekiti wa bajeti Andrew Chenge - Mwanasheria, lakini unamuweka Dr Ciril Chami - Economist with PhD- mjumbe? Wakati huo huo unamuweka mtu kama Abas Mtemvu kuwa mwenyekiti wa kamati ya sheria na katiba na kuacha wanasheria waliobobea! Hivi huku ndiko ku-utulise resources tulizonazo ndani ya bunge?

Bunge la majaribio na utalii? Hawako serious kabisa hawa waheshimiwa. Inaudhi.

NB:
1 Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa,Mb, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA. Ningetaka kujua ana uhusiano wowote na Dr Mgimwa, Waziri wa Fedha? Na ana ujuzi gani kwenye mambo ya uchumi, viwanda na biashara?
 
Mnyika"wame mpaisha zaidi"!Kumuweka kamati inayohusu ardhi ni kumpa meno zaidi maana kwenye idara hiyo ndiyo madudu ya kutia uchungu yapo!

Mnyika nenda kam-bane Mama Tibaijuka!
 
Watabadili formation zote lakini hawatawaweza Chadema, Chadema sio CUF a.k.a bibi kizee cha Torino. Sasa hv hata hawasikiki tena.
 
Kamati ya nishati na madini ni muhimu sana ila imepewa watu ambao wengi hawaendani na umuhim huo.

Kamati ya serikali za mitaa na tawala za mikoa nayo wajumbe wake sioni mantiki yake

Kamati ya haki ,kinga na madaraka ya bunge , inapaswa kuwa balanced na sio kujaza wabunge wengi wa CCM na wakati huo hii ni kama mahakama ya nidham za wabunge, sasa kutokana na ushindani wa kisiasa uliopo hawatawatendea haki wabunge wa vyama vinine kutokana na ukweli kuwa maamuzi yake yanafanywa kwa kura , sasa haki itatokea wa
Hapo?

Hivi Joshua Nassari yuko kamati gani, Ndesamburo yuko kamati gani ........aliyeona majina yao tafadhali.

Hivi ile kamati ya Afriika mashariki mbona sijaiona tena humu au Supika alitudanganya watanzania?

Mkuu mbona unalalamika sana. Spika hawezi tu kujaza nafasi bila mbunge kuwa angalau na uwezo katika area ya mambo hayo (qualification). Wewe unashauri ingekuwaje.

Mzee Ndesamburo yuko kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.
 
Wapange wanavyojua wao makamanda tumewatuma kufanya kazi na wataifanya tu.
Hatuwaachi tutakufa nao mwaka huu mpaka kieleweke.
Pipooooz
 
Tanzania tuna bahati mbaya sana. Ukiangalia muundo wa hizi kamati unaona kabisa huu ni utani, na kama si utani umbumbumbu, na kama si umbumbumbu basi hawa wakubwa wamekusudia kuona hii nchi inaenda kuzimu!

Kama nilivyosema awali, wabunge wote wana taaluma zao. Spika na washauri wake wameshindwa kuona umuhimu wa kutumia TAALUMA za wabunge kwa kuwaweka kwenye sekta ambazo wana ujuzi nazo? Kwa mfano, unampa uenyekiti wa bajeti Andrew Chenge - Mwanasheria, lakini unamuweka Dr Ciril Chami - Economist with PhD- mjumbe? Wakati huo huo unamuweka mtu kama Abas Mtemvu kuwa mwenyekiti wa kamati ya sheria na katiba na kuacha wanasheria waliobobea! Hivi huku ndiko ku-utulise resources tulizonazo ndani ya bunge?

Bunge la majaribio na utalii? Hawako serious kabisa hawa waheshimiwa. Inaudhi.

NB:
1 Mhe. Mahmoud Hassan Mgimwa,Mb, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA. Ningetaka kujua ana uhusiano wowote na Dr Mgimwa, Waziri wa Fedha? Na ana ujuzi gani kwenye mambo ya uchumi, viwanda na biashara?

Mbona watanzania tunapenda sana kulalamika lalamika tu?.

Mkuu siyo kuanza kulalamika tu bila hata kuzisoma kanuni za bunge na kuzielewa.

Nani kakwambia spika wa bunge anateuwa wenyeviti wa kamati za bunge?. Fanya kwanza homework kabla ya kulalamika.

Spika hachagui wenyeviti wa kamati za bunge bali wao miongoni mwao ndiyo watajichagua kama kanuni inavyoanisha hapa,

(10) Wajumbe wa kila Kamati watawachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwao ambao kwa muda wote watakaokuwa Wabunge, wataendelea kushika nafasi hizo mpaka mwisho wa kipindi kilichotajwa katika fasili ya (7) ya Kanuni hii, lakini wanaweza kuchaguliwa tena.
 
Huu mpangilio/upangaji wa kamati za bunge sijaupenda kabisa. Kuna baadhi ya kamati zimewekewa wabunge vilaza kabisa.
Kamati kama za madini, hesabu za serikali, serikali za mitaa hazina watu makini.
 
WAJAMENI,
Nawaombeni msifanye hii kitu ya REPLY WITH QUOTE kwa vile mtawamaliza wale wanaotumia visimu vya mchina kuingia JF.

JUST REPLY ONLY WITHOUT QUOTE AND GO.
 
chadema inawanyima usingizi ma ccm kila kukicha wanabuni namna yakuizoofisha..
 
Mbona watanzania tunapenda sana kulalamika lalamika tu?.

Mkuu siyo kuanza kulalamika tu bila hata kuzisoma kanuni za bunge na kuzielewa.

Nani kakwambia spika wa bunge anateuwa wenyeviti wa kamati za bunge?. Fanya kwanza homework kabla ya kulalamika.

Spika hachagui wenyeviti wa kamati za bunge bali wao miongoni mwao ndiyo watajichagua kama kanuni inavyoanisha hapa,

(10) Wajumbe wa kila Kamati watawachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kutoka miongoni mwao ambao kwa muda wote watakaokuwa Wabunge, wataendelea kushika nafasi hizo mpaka mwisho wa kipindi kilichotajwa katika fasili ya (7) ya Kanuni hii, lakini wanaweza kuchaguliwa tena.


Lusinde maendeleo ya jamii, lahaulah
 
Loudly n Clear Serikali ya CCM haitaki bughudha kwenye sekta ya NISHATI NA MADINI...Mikataba ya Gesi, Mafuta, Dhahabu, Uranium, Makaa ya Mawe, Almasi, Tanzanite, Rubby, AGRECO, IPTL, SONGAS, PAN AFRICAN, SYMBION vitaendelea kuwa siri kwakuwa vinatuingizia fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao... "Umoja ni Ushindi"!!!!
 
Back
Top Bottom