Mati Mkenda
Senior Member
- Mar 4, 2018
- 171
- 211
Siku ya Jana CCM ilitangaza majina ya Watu watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya ubunge kwenye majimbo yote, Bara na Visiwani, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu. Uteuzi huo unaweza kutazamwa kwa sura mbili, yaani sura ya kwanza kuwa ni tishio na ile pili kuwa ni funzo kubwa kwa vyama vya upinzani hapa nchini.
Tishio: Vyama vya upinzani almost vyote, tayari vilikuwa vimeshatangaza majina ya watu ambao watapeperusha bendera za vyama vyao katika baadhi ya majimbo. Walifanya “Professional Guess” zao za kukadiria uwezo wa wapinzani wao, hasa kutoka chama tawala, wakaja na majina ya wale walioona kuwa wana uwezo wa kushindana na washindani wao hao. Kitendo cha CCM kuja na sura nyingi mpya kinaweza kuwa ni tishio kubwa sana kwa upinzani kwani kuna wagombea wapya wengi ambao hata upinzani hawakutajia kama wangepitishwa na chama hicho.
Hivyo hata kama watarudi kwenye “Drawing Board” na kuanza kujadili sura mpya hizo haitasaidia kwani kuwaondoa wagombea wao waliopitishwa ambao wanaweza kuwa na udhaifu fulani kiasi cha kutoa nafasi kwa CCM kushinda, kunaweza kuleta mpasuko mkubwa ndani ya vyama vyao. Hivyo upo uwezekano CCM wakawa wamecheza na loophole hiyo, kwa kuwaleta wagombea wenye ushawishi mkubwa kuzidi ule wa wapinzani wao.
Funzo: CCM imeteua wagombea kwenye majimbo yote, kitendo ambacho hakijawezekana kwa vyama vya upinzani. Hii inaonyesha kuwa CCM ina hazina kubwa ya wanachama waliojengeka kiuongozi. Kitendo cha sura tulizozizoea ndani ya CCM kuwekwa pembeni tunaweza sema chama kimefanya kitu kinachoitwa “Breaking the status quo”, hali ambayo hata wapinzani hawakutegemea kama ingetokea.
Hali hiyo imetoa funzo kuwa bila fulani na fulani, bado chama kinaweza kusimama na kusonga mbele. Ni wakati sasa wa upinzani kuiga mfano huo mzuri wa CCM kwa kuandaa hazina ya viongozi, ili kuweza kuwa na uwezo wa kusimamisha wagombea katika majimbo yote, ambao wana uwezo mkubwa wa kushawishi na si mar azote kuwaleta watu wale wale ambao kila kukicha wanadidimiza maendeleo ya vyama hivyo. Lazima vyama vihame kutoka kumilikiwa na watu wachache hadi kumilikiwa na umma.