Uteuzi Wa Viongozi Wazee

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Feb 16, 2007
989
51
Nimekuwa nikipata shida kutokana na mfumo wa uongozi hapa tanzania ktk serikali na kwenye sekta za umma.Tumekuwa na viongozi wale wale kwenye madaraka kiasi kwamba damu mpya(vijana)hatupewi nafasi kutoa michangoyetu ktk jamii.Sasa hivi wanatuambia tunapomaliza masomo tujiajiri wenyewe wakati hatuna mitaji,hatuna uzoefi wa kazi,hatuna contact na washikadau wengine.Lakini hawa viongozi wetu wanauzoefu na contact mbalimbali na washikadau mbalimbali,mitaji mikubwa,kwa nini woa wasijiweke pembeni iliwatengeneze ajira kwa kutumia ujuzi wao walioupata ktk kulitumikia taifa kuliko kungangania kufia katika ofisi za serikali au za umma.
 
Yaani nakuambia,

damu mpya hakuna anayewahitaji sasa hivi! inabidi mwende congo au Rwanda kupigana vile maana hiyo ndiyo ajira pekee imebakia
 
katibu-tarafa,
hapo umeshindilia msumari kwenye kichwa!! kwenye nchi za wenzetu wataalamu kwanza hupata uzoefu ktk taasisi za serikali na baada ya hapo huenda kwenye sekta binafsi na KUJIAJIRI.

Mimi nawashangaa sana viongozi wetu wanapowaambia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wajiajiri. hivi hata kama ni mhandisi anaomba kazi, zaidi ya vyeti vyake, ana kitu gani cha kuonyesha kwamba anauwezo wa kitaalamu?
 
Damu mpya mbona ipo? ila lazima iwe na uhusiano wa damu na damu ya zamani.. to some extent anyway! Na mimi nataka nibadili jina, sijui nijiite nani? ...

Petro F. Sumaye
Henry Joseph D. Mwakawago
Hassan M. R. Kawawa
Amir A.S. Mkwawa
Raymond W.B. Mkapa
 
Hii ndio sababu ya kutokuwa na jipya Tanzania, bado mambo ni yale yale ya mwaka 47! Uongozi unazunguka miongoni mwa wateule wachache miaka nenda miaka rudi.
 
Damu mpya mbona ipo? ila lazima iwe na uhusiano wa damu na damu ya zamani.. to some extent anyway! Na mimi nataka nibadili jina, sijui nijiite nani? ...

Petro F. Sumaye
Henry Joseph D. Mwakawago
Hassan M. R. Kawawa
Amir A.S. Mkwawa
Raymond W.B. Mkapa

Mkjj,

kwi kwi kwi,

inabidi ubadili jina ujiite;

mtoto wa mlalahoi anayetaka kutumia jina la mkubwa bin Kikwete
 
..Nyerere alikuwa mtoto wa Chifu.
..Malecele mtoto wa mtumishi wa Kanisa.
..Mkapa mtoto wa mtumishi wa Kanisa.
..Kikwete mtoto wa DC.
..Kawawa mtoto wa game warden.

I can go on and on...

Tanzania tatizo letu Uchumi wetu uko very slow na hau-create ajiri mpya. Kila mtu akiwa shule anawaza kufanya kazi BOT,TBL,PPF,Sigara.

kwenye nchi za wenzetu ukiingia kwenye siasa au serikali frm private sector you are taking a HUGE PAY CUT.
 
Nafikiri tufike mahala watu wafanyekazi kwa mkataba wa miaka kumi au kuminatano na baada ya hapo waingie katika sekta binafsi ilikupeana nafasi ktk kulitumikia taifa,kwani ni letu sote.Tukifanya hivyo tutaongeza uwajibikaji ktk serikali pamoja na sekta za umma.
 
Nakubaliana na wachangiaji wengi hapa, Kwnye ile topiki ya uchaguzi wa Msekwa nimesema hivi:

Mimi nashangaa ati Msekwa ni chaguo bora, pls give me a break, na sisi tutajapata hayo madaraka lini? kama waioko juu hawastaafu?

Tangia nikiwa naaza darasa la kwanza yeye alikuwa sijui mkuu wa nini, (sijui katibu mkuu wa tanu, mkuu wa mkoa, VC mlimani, etc.) leo hii nafikiria mambo ya pensheni yangu, yeye bado yupo huko juu, je hakuna vijana?, au angalau watu wa miaka ya 50 au sitini! Iweje leo hii karne ya 21, kati ya watanzania milioni 35 bado tung'ang'ane na watu wenye zaidi ya miaka 70 na ushee? For me its a joke, big joke! Au Msekwa ndo baadhi ya watu wachache wanaojiona wameteuliwa na Muumba kama akina Mugabe, Banda, Castro, Nujoma na vizee vingine ambavyo havitaki kukubali umri wao na kuachia ngazi? WAZEE NYIE hamna aibu?
 
Ulimwengu ameongelea leo kwenye BBC swahili, kwamba hakuna jipya watu ni wale wale
 
Nafikiri tufike mahala watu wafanyekazi kwa mkataba wa miaka kumi au kuminatano na baada ya hapo waingie katika sekta binafsi ilikupeana nafasi ktk kulitumikia taifa,kwani ni letu sote.Tukifanya hivyo tutaongeza uwajibikaji ktk serikali pamoja na sekta za umma.

Wajanja hawa, mikataba ipo na ina mwisho wake, wana renew na kusema oooh, huyu bado tunamuhitaji, sijui vitu gani, yaani kero tupu. Akina 'anonymous' sisi tutaishia kuwa wamachinga na digrii zetu.
 
Wazee waliokuwa wachovu kuongoza safari, mnaweza kabisa msifike huko mnakoenda kutokana na uchovu wao.

Wazee ni muhimu katika uongozi wowote ule, kama huamini anza kuwakataa baba na mama yako, then uone kama utapiga hatua.
Nadhani hii si issue ya kukomalia, kinachohitajika ni wezo wa mtu kuweza kufanya kazi na ku-deliver.

Pia kimbikeni kwamba uchagizi wa CCM ni kwa manufaa ya wanachama wa CCM wenyewe na chama chao, wewe kama ni mwanachama wa CCM na unataka kuhoji humu kwenye JF kwani nini wanawachagua wazee, ina maana hukijui chama chako kwani kinautaratibu maalum wa kufikisha hayo unayotaka kuhoji. Otherwise Mambo ya nani kapewa kiti CCM kwa mtazamo wangu siyo issue ya JF.
 
Wazee ni muhimu katika uongozi wowote ule, kama huamini anza kuwakataa baba na mama yako, then uone kama utapiga hatua........

Mhhh,

Yani kukataa wazee kuongoza siasa ni kama kumkataa baba na mama? Ama kweli JF kutakuwa na mengi sana hapa nitasoma mwaka huu.

Katika maisha haya ambayo wazazi wangu wanafanya chini ya asilimia tano katika maisha yangu ya sasa, ninashauriwa hapa kuwa niwaruhusu wazazi waendeshe asilimia tisini na tano ya maisha yangu?

Haya mwaya, wanasisiemu fundisho hilo munapewa kuwa wazee ndio hivyo tena wako hapo to stay. Young blood inabidi muwe back up singers wa Komba or samthin...
 
Wa-Tanzania sasa hivi wanalia machozi na haya haya maneno ya kuwapa madaraka vijana, si tumewapa na matokeo yake ndio hayo tumeyaona, kina Karamagi wanavyotufanya wajinga,

Ndio maana huko Dodoma, Vijana kina Muungwana, wamekubali kuwa hawawezi, ndo maana wao wenyewe wamekubali kumpa Msekwa, kwenye hili la vijana na wazee, Tanzania hatuwezi kulisema tena maana tumeshajionea wenyewe,

Mkapa kila siku analia ni private, the matter of fact kuna theory kubwa among viongozi wa juu na hasa familia yake Mkapa, kuwa to this day haelewi aliwapitishaje Mtandao, maana alikuwa amemuapia mke wake kuwa haitakuja kutokea, mtoto wake alipomuona akimpitisha Muungwana, aliipiga mateke TV,

Anyways, kwenye hili la wazee na vijana, Tanzania tufikie mahali tunyamaze tu, maan limetushinda kabisaaa!
 
mhhh,

MKuu FMES, kama Kikwete na Karamagi ni vijana, basi inabidi nirudi shuleni kusoma upya tafsiri mpya ya neno ujana!
 
wsdau sasa tunageuza mada inakwenda ndivyo sivyo,hapa tunataka hawa wazee ambao wamelitumikia taifa hili kwa muda mrefu na kupata uzoefu wakutosha ni wakati wao sasa kuingia ktk sekta binafsi ilikutumia ujuzi na mtaji walionao ktk kukuza uchumi na sio kuzeekea kwenye madaraka ambayo wamekuwa nayo miakanenda rudi.Na sio kunisukuma mimi ambaye ninacheti tu bila ujuzi wala mtaji.hilisio suala la uccm wa nanihiiiii
 
Mhhh,

Yani kukataa wazee kuongoza siasa ni kama kumkataa baba na mama? Ama kweli JF kutakuwa na mengi sana hapa nitasoma mwaka huu.

Katika maisha haya ambayo wazazi wangu wanafanya chini ya asilimia tano katika maisha yangu ya sasa, ninashauriwa hapa kuwa niwaruhusu wazazi waendeshe asilimia tisini na tano ya maisha yangu?

Haya mwaya, wanasisiemu fundisho hilo munapewa kuwa wazee ndio hivyo tena wako hapo to stay. Young blood inabidi muwe back up singers wa Komba or samthin...

Sidhani kama kweli wazazi wako wanafanya 5% katika maisha yako ya sasa unless you quantify. Kama ndivyo hivyo basi kuna tatizo katika maisha yako.
Nikirudi katika suala la uongozi, I meant kwamba huwezi ukawa na viongozi watokanao na tabaka moja tu, especially kwa chama kama CCM ambapo kuwepo kwake kunatokana na mikakati mbalimbali wanayojiwekea kila kukicha. Hiki kinajionyesha ni chama cha umoja zaidi (wanachama na viongozi wake hukukubali:kupata na kupoteza) na hii ndiyo silaha kubwa na nguvu ya CCM.
CCM ina matabaka mbalimbali ya wanachama (Wanawake, Wazazi, Vijana, wazee, wasomi, wafanyabiashara, wakulima etc). Kwa hiyo at certain time kubalance nguvu ya chama ni muhimu sana (kwa wanasiasa wanalielewa hili) vinginevyo itakuwa kazi kubwa kuendesha shughuli za chama not only chama hata kama ingekuwa ni klabu ya mpira.
 
Back
Top Bottom