Uteuzi wa viongozi wa NEC urudishwe mikononi mwa wananchi kupitia Bunge

Relief

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
254
47
Ndugu zangu katika Taifa hili la mwenye nacho kuongezewa na asie nacho kunyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho, nawasalimuni nyote.

Naomba tuungane kuazimia hili la uteuzi wa viongozi wa NEC pamoja na baraza lake lote kurudishwa mikononi mwa wananchi kupitia kwa wawakilishi wetu bungeni. Ni kwa namna hii tutapata Uchaguzi ulio huru na wa haki na usio fungamana na upande wowote, ili tuweze kupata viongozi sahihi na waadilifu.

Kwa namna ilivyo sasa UCHAGUZI umekosa haki, umekuwa ni wa kubebana sana ili kulinda vibarua kwa manufaa ya watu binafsi na sio manufaa ya Taifa zima.

Wana jamii tuungane kufanikisha hili sasa kwa demokrasia ya kweli na ya kuaminika

I urge you brothers and sisters, Its about time we call a spade a spade.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Well said Relief, haya mambo ya kila mtu anateuliwa na Rais imekuwa too much sasa.....tena kwa tume nyeti kama hii ilibidi moja kwa moja iteuliwe na BUNGE la JMT; hapo ndo kutakuwa na free and fair election. Kwa akilli ya haraka haraka tu na ya kitoto, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa NEC wanareport kwa rais (ndo boss wao na yeye ndo amewapa kazi), na rais huyo huyo ndo mgombea Urais; hivi kweli watammwaga mheshimiwa boss wao.......

If you guys know the elect MPs personally its about time tuwatumie wapeleke hii mada Bungeni with strong reasons. NEC inabidi iriport kwa BUNGE na sio rais..........otherwise CCM hawatakubali kung'olewa na kila mwaka itakuwa hivi hivi tu.
 
Nadhani itakuwa bora mkurugenzi wa uchaguzi achaguliwe na wananchi kwa kupigiwa kura badala ya kuteuliwa na raisi
 
Good topic, good start!

Maada kama hizi ndio zinahitaji hasa attention kwa wapenda mageuzi na mabadiliko! lakini wapenda siasa za udaku huwaoni huku
 
Wananchi tuungane??
Tuanzie wapi? hapo ndipo pagumu.

Kupitia forum mbalimbali, tasisi za kijamii kama TGNP, TAMWA, Vyombo Vya habari na kwa wabunge wa upinzani. Wimbo wetu sasa UWE NI MABADILIKO YA KATIBA YA JAMHURI YA MUNGANNO WA TANZANIA. Kila kitu kitaainishwa kwenye Katiba, ikiwa ni pamoja na muundo wa tume na uteuzi wake, madaraka ya rais.nk.
 
Good topic, good start!

Maada kama hizi ndio zinahitaji hasa attention kwa wapenda mageuzi na mabadiliko! lakini wapenda siasa za udaku huwaoni huku

I CANT AGREE WITH YOU MORE, siasa za fitina ndo zimetawala na chuki lakini utakapozungumzia jambo la msingi kwa kweli wafitini hutowaona ng'o! why? kwa sababu wanaona jambo hilo lina manufaa kwa Taifa na si kwao na wao wangependa iwe the opposite, this is a problem na hawa watu watatoka tuu in no time
 
I CANT AGREE WITH YOU MORE, siasa za fitina ndo zimetawala na chuki lakini utakapozungumzia jambo la msingi kwa kweli wafitini hutowaona ng'o! why? kwa sababu wanaona jambo hilo lina manufaa kwa Taifa na si kwao na wao wangependa iwe the opposite, this is a problem na hawa watu watatoka tuu in no time

surely!
 
Back
Top Bottom