Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 697
Baada ya kuangalia yanayotoke bungeni na katika vyombo mbalimbali vya serikali, Naona kama kuna Uoga wa utendaji wa vingozi wa vyombo nyeti vya serikali na hivyo kuathiri ufanisi wa utendaji wa serikali kwa ujumla. Viongozi wa vyombo nyeti kama TISS, Waziri Mkuu, Takukuru, Jaji Mkuu, Msajili wa Vyama, Mkurugenzi Tume ya Uchaguzi NK, Wanateuliwa na serikali kupitia Raisi. Nafikiri Raisi angependekeza majina matatu bora na kuyapeleka Bungeni kwa uteuzi, na Raisi asiwe na mamlaka ya kuwaondoa, ila kwa bunge kuridhia.
Hii itawapa nguvu za kutenda kazi kitaaluma zaidi, na wawe wanariport kwenye kamati za bunge, ili zichambuliwe na kupelekwa kwa raisi kwa ajili ya utekelezaji. Hii itaondoa suala la kulindana. Tatizo letu ni kuiga kila kitu ambacho mkoloni alituachia, hii inaweza kuleta wakoloni weusi. Wateja hivi vyombo ni umma na sio watawala kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni. Kwa mfano Umma una haki ya kujua aina fulani ya taarifa za kiusalama, hasa zile za uhujumu, hata kupitia magazetini, lakini TISS haiwezi kwa sasa kufanya hivyo.
Riport hizi; kama ya uuzaji wa mlima wa kiwira, vitalu, EPA, Tanesco NK, ni mifano hai ambayo haiitaji kungijea GAG au Kamati za bunge, kulipua mambo. Mifumo yetu inafanya hivi vyombo viwe butu. TAKUKURU, POLISI, MAHAKAMA, TIIS nakadhalika wamekuwa wakiegemea kwa watawala kuliko wananchi. Na mara nyingine hata kuegemea katika chama fulani. Kumbuka leo CCM, Kesho CUF, Keshokutwa TLP au CDM, hawa watachanganyikiwa wasipojengewa mfumo mzuri.
Hii itafanya viongozi wakuu wa nchi kutafakari mbele ya safari zao za uongozi. Na watawajibika na kupendwa zaidi na wananchi.
Samahani, haya ni maono ya baadaye, maana nahisi wajukuu watachapa viboko makaburi yetu.