Uteuzi wa vingozi wa vyombo nyeti ukamilishwe kupitia bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa vingozi wa vyombo nyeti ukamilishwe kupitia bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fredrick Sanga, May 20, 2012.

 1. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Baada ya kuangalia yanayotoke bungeni na katika vyombo mbalimbali vya serikali, Naona kama kuna Uoga wa utendaji wa vingozi wa vyombo nyeti vya serikali na hivyo kuathiri ufanisi wa utendaji wa serikali kwa ujumla. Viongozi wa vyombo nyeti kama TISS, Waziri Mkuu, Takukuru, Jaji Mkuu, Msajili wa Vyama, Mkurugenzi Tume ya Uchaguzi NK, Wanateuliwa na serikali kupitia Raisi. Nafikiri Raisi angependekeza majina matatu bora na kuyapeleka Bungeni kwa uteuzi, na Raisi asiwe na mamlaka ya kuwaondoa, ila kwa bunge kuridhia.

  Hii itawapa nguvu za kutenda kazi kitaaluma zaidi, na wawe wanariport kwenye kamati za bunge, ili zichambuliwe na kupelekwa kwa raisi kwa ajili ya utekelezaji. Hii itaondoa suala la kulindana. Tatizo letu ni kuiga kila kitu ambacho mkoloni alituachia, hii inaweza kuleta wakoloni weusi. Wateja hivi vyombo ni umma na sio watawala kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni. Kwa mfano Umma una haki ya kujua aina fulani ya taarifa za kiusalama, hasa zile za uhujumu, hata kupitia magazetini, lakini TISS haiwezi kwa sasa kufanya hivyo.

  Riport hizi; kama ya uuzaji wa mlima wa kiwira, vitalu, EPA, Tanesco NK, ni mifano hai ambayo haiitaji kungijea GAG au Kamati za bunge, kulipua mambo. Mifumo yetu inafanya hivi vyombo viwe butu. TAKUKURU, POLISI, MAHAKAMA, TIIS nakadhalika wamekuwa wakiegemea kwa watawala kuliko wananchi. Na mara nyingine hata kuegemea katika chama fulani. Kumbuka leo CCM, Kesho CUF, Keshokutwa TLP au CDM, hawa watachanganyikiwa wasipojengewa mfumo mzuri.

  Hii itafanya viongozi wakuu wa nchi kutafakari mbele ya safari zao za uongozi. Na watawajibika na kupendwa zaidi na wananchi.

  Samahani, haya ni maono ya baadaye, maana nahisi wajukuu watachapa viboko makaburi yetu.
   
 2. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenena lakini kizazi hiki kinachohofia utawala wao kuondoshwa madarakani watakuelewa? Marehemu Baba wa Taifa aliwahi kusema tuna viongozi wa ajabu sana, wanaochukua mambo ya kijinga yaliyofanywa na uongozi uliopita na kuacha yale ya maana.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hayo uliyoyasema ndio yanatakiwa yaingie kwenye katiba mpya. Hii itawapa hao viongozi security of tenure na kuwaondolea uoga wa kujiuliza nikifanya hivi si naweza kugutwa kazi. Wenzetu Kenya wamefika huko sisi ndio kwnza tunaanza mchakato wa Katiba Mpya.
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Suala ni kwamba vyombo vyote vinatakiwa kuutumikia umma kwanza, halafu kuwasaidia viongozi kuutumikia umma. Kwa sasa nahisi kama vinatumikia kikundi fulani teule. Hii ni hatari. Leo unaweza kuwa kwenye kundi teule, lakini kesho usiwepo. Na waswasi sana na stability ya nchi katika hizi structure za kikoloni. Hata ukoloni wenyewe ulishashindwa.
   
 5. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mawazo yako ni mazuri na yanafaa kupelekwa na wewe mwenyewe kwenye tume ya kuandaa katiba mpya inayoongozwa na Sinde Warioba!!
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hawa tume wameweka vipengele vya kufunga watu, na mafaini nisiyoweza kulipa. Sasa wasije wakanigeuka huko. Mimi ni hapa hapa JF pananitosha, mpaka watakapoondoa hivyo vitisho.
   
 7. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  wenzetu wakenya rais akiteua hovyo labda kiburudisho chake,kama hajafanyiwa vetting wabunge wanapiga chini uteuzi huo.wenzetu asasi za kiraia hazijalala,rais akimteua mtu ambae wana mashaka nae,chap chap wanarush kuzuia uteuzi mahakamani.sisi huku tumemuachia jk kila kitu.
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ina maana wakenya wametuzidi sana kama shilingi yao ilivyotuacha?
   
 9. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Suala la ujenzi wa Mfumo ndilo analofanya JK japokuwa sisi wenye akili za kawaida hatulioni hilo. Mwisho wa siku tunaishia kumlalamikia kuwa hafanyi kazi. But the history shall tell us
   
 10. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Suala la ujenzi wa Mfumo ndilo analofanya JK japokuwa sisi wenye akili za kawaida hatulioni hilo. Mwisho wa siku tunaishia kumlalamikia kuwa hafanyi kazi. But the history shall tell us
   
 11. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hilo linaonekana, hata katika kuridhia mchakato wa katiba, sasa sisis wananchi tunatoa mawazo, turekebishane ili tupate muono muafaka.

  Inawezekana.
   
 12. E

  ESAM JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hoja yako imesimama mkuu nashukuru tunazidi kupata masuala muhimu ya kuingiza kwenye Katiba yetu mpya ili matumizi mabaya ya vyombo hivi yakomeshwe. Hongera kwa hoja nzuri
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Labda wakuu JF hebu tujaribu kulist hivi vyombo nyeti, ili tubadilishane mawazo. Nimetoa mifano michache tu.
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hawa watu hawafanyi kazi kwa uhuru bse alyewateu anawaamrisha kama mbwa wa askali wakiwa independent itakuwa jambo la mbolea sana
   
 15. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mbona mimi ninavyomfahamu M Kiti, huwa hawezi kuamrishwa? Sijui lakini.
   
 16. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hawa wabunge wako frustrated
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Unaona mambo yanavyoenda?
   
Loading...