Uteuzi wa Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na JKT ni mpango au njama za CCM?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,709
JUMANNE, AGOSTI 24, 2021

MAKALA


Rais Samia tuteulie Waziri wa Ulinzi mwanamama

Na Nkwazi Mhango

KUFUATIA
kifo cha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa, wizara hiyo imebaki na pengo ambalo lazima lizibwe. Kwanza naomba nitumie fursa hii kutoa salamu za rambirambi kwako Rais Samia Suluhu Hassan, familia ya Kwandikwa, majirani zake na Taifa kwa kuondokewa na mwenzetu na kiongozi wetu.

Baada ya salamu za rambirambi, naomba nitoe ushauri kwako Rais Samia wetu mpendwa. Ushauri wenyewe ni kukuomba wakati unajiandaa kufanya uteuzi wa kuziba nafasi iliyoachwa na Kwandikwa, tafadhali Rais naomba tuteulie waziri mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Ulinzi ili kuleta si tu usawa wa kijinsia bali heshima na kubadili mazoea ya mfumo dume ambao umetawala tangu tujitawale takriban miaka 60 iliyopita. Hii maana yake ni kwamba uhuru wetu bado ni mashaka na haujakamilika. Hivyo, unahitaji kukamilishwa kwa kutenda haki kijinsia.

Tangu tupate Uhuru, nchi yetu haijawahi kuwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa mwanamke hata naibu wake. Haijawahi kuwa na mkuu wa majeshi au naibu mwanamke wala IGP au naibu ukiachia mbali Mwanasheria Mkuu. Hatujawahi kuwa na Jaji Mkuu au naibu wake mwanamke. Hatujawahi kuwa na Waziri wa Mambo ya Ndani au naibu wake mwanamke. Kwanini sasa tusifanye mabadiliko hasa kipindi hiki kinacholenga kumkomboa mtoto wa kike kutoka kwenye minyororo ya mfumo dume? Je ina maana tangu tupate uhuru hatujaweza kuwa na kina mama wanaofaa kuhudumu katika nafasi hizo na nyingine? Je tatizo ni wanawake au mfumo? Kwa wanaojua namna tulivyorithi mfumo wa kikoloni, hawatashangaa kuambiwa kuwa mfumo dume hata kama tulikuwa nao kabla ya kutawaliwa, ni mabaki na makandokando ya ukoloni tena mkongwe.

Zifuatazo ni sababu zilizonisukuma kumuomba Rais Samia kama itampendeza atuteulie Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa mwanamke kama njia ya kuliandaa taifa kisaikolojia kuwaweka kwenye nafasi nyingine nyeti ambazo zimekuwa himaya ya wanaume tangu tupate uhuru. Mosi, ni kuwatendea haki kina mama dhidi ya mfumo dume usiotenda haki kijinsia. Ukiachia mbali kutenda haki, kitendo hiki kitawapa mamlaka (empower), kumuinua na kumpa motisha na uzoefu wa kufanya makubwa kama binadamu na raia katika nchi na jamii yake ukiachia mbali kujenga mazingira na mfumo wezeshi kijinsia na kwa usawa. Kama Rais mwana mama umeweza, atashindwa waziri?

Pili, ni kuwapa fursa ya kuonesha uwezo wao ili kuondoa dhana ya ujinsia na madhara ya mfumo dume. Nchi ya jirani ya Kenya ina Waziri wa Ulinzi, Rachel Omamo aliyechukua nafasi kutoka kwa mwanamama mwingine Monica Juma na mambo yanakwenda vizuri. Afrika Kusini wanaye Thandi Modise ambaye aliteuliwa wiki mbili zilizopita akichukua nafasi kutoka kwa mwanamama mwingine Nosiviwe Noluthando Mapisa-Nqakula na mambo yanakwenda vizuri. Kabla ya hawa kina mama wawili alikuwepo Lindiwe Sisulu na mambo yalikwenda uzuri tu. Sudan Kusini wanae Angelina Teny, hivyo kwanini sisi tusifuatie ili kutenda haki kwa wote. Kama kweli tuna nia ya dhati kuleta usawa, kwanini wenzetu watupite wakati tunayo nafasi ya kuondokana na ubaguzi wa kijinsia?

Tatu, tunataka majeshi na idara zetu nyeti zianze kuzoea kusimamiwa na jinsia zote siyo kuleta usawa tu bali pia kujenga mazingira ya kutendeana kwa usawa. Kama mama atakuwa waziri wa wizara hii, hata makamanda hawataona vigumu wala kigugumizi kuwatendea haki wanajeshi walio chini yao bila kujali jinsia iwe kwa kujua au kutojua.

Kwa vile Tanzania imesheheni wanawake wenye uwezo na vipaji vya kuweza kusimamia wizara hii nyeti, wakati wa kuwaibua na kuwapa nafasi hizo umefika ili waoneshe na kutumia vipaji vyao kwa Taifa lao. Kuwateua wanawake kushika nafasi ambazo siku zote zimekuwa za wanaume, kunawajenga Watanzania kisaikolojia kujikubali kwa maumbile yao ambayo hakuna aliyeandika barua kwa Mungu amuumbe alivyo bali kuzaliwa mwanamke au mwanamke ni uamuzi wa muumbaji mwenyewe.

Pia ifahamike kuwa kwa kuwateua wanawake kwenye nafasi ambazo zimekuwa himaya ya wanaume, hakutawapa kujiamini na uzoefu wateuliwa tu bali kutatoa motisha kwa watoto wa kike hata wa kiume kujiona wako sawa na wanaweza kufanya kila kitu bila kuzuiliwa kwa kisingizio cha jinsia zao. Kuna kazi kubwa kama kumtengeneza mtoto na kumbeba ukiachia mbali kumtunza hadi anakuwa mtu mzima? Mbona wote tumetokea kwa hao tunaowaona dhaifu?

Nimalizie kwa kukushukuru Rais wangu Samia kama utasikiliza ushauri huu wa bure ambao nimekuwa nikiutoa kupitia barua ya wazi kama njia mojawapo ya kuchangia kwenye uendeshaji wa Taifa letu.

Kuna kazi kubwa kama kumtengeneza mtoto na kumbeba ukiachia mbali kumtunza hadi anakuwa mtu mzima? Mbona wote tumetokea kwa hao tunaowaona dhaifu?

1631479576826.png
 
Kila lakheri Mh Tax katika wajibu wako muhimu kama Mtanzania aliyeaminiwa katika jukumu nyeti la ulinzi wa mipaka ya nchi yetu. Usiangalie jinsia yako bali angalia majukumu uliyopewa na Taifa.
 
Huyo Tax ataongoza wizara kwa maelekezo kutoka juu!!!Mama ameogopa kumuweka mwanaume hapo hasa wale vihere here wa kutaka kugombea Uraisi by 2025!!!
 
Back
Top Bottom