Uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi walaumiwe UKAWA

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,250
Kama UKAWA wangetumia busara wakati ule wa mchakato wa Katiba mpya hasa kwenye eneo la bunge la Katiba ambamo ndimo ilizaliwa UKAWA na kutosusia moja kwa moja vikao na hatimae Katiba iliyopitishwa na kina marehemu mzee Sitta leo Rais Magufuli asingekua na mamlaka kikatiba ya kuteua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na pengine asingekua rais maana hata malalamiko ya Lowassa kuibiwa ushindi badala ya kuyapeleka kwa watu kama nabii Joshua na wazungu mbalimbali wangekua na nafasi kikatiba ya kwenda mahakamani kuhoji ushindi.

Kama ukiisoma ile Katiba pendekeza iliyopitishwa na Bunge la Katiba bila UKAWA kuwemo mle kuna mengi mazuri japo siyo yote, lakini si haba kwa kuanzia hasa kwa wakati ule ambapo nchi ilikua inaelekea kwenye uchaguzi mkuu, waswahili wana msemo nanukuu "toa kwanza mwiba ulikuchoma kalioni upate kukaa chini uweze kuutoa mwiba ulikuchoma mguuni" mwisho wa kunukuu.

Hicho ndio kilipaswa kufanyika, kukubali kwanza kupokea kitu ambacho kilikua kikililiwa siku nyingi na wana demokrasia (tume huru ya uchaguzi), then mambo mengine wangeendelea kuyadai kwenye serikali inayofuata ambayo pengine ingekua ni yao! Kwenye katiba ile pendekezwa kulikua na mengi yakiwemo haya ya muhimu kwa wapenda demokrasia na wanasiasa wa upinzani:

1 Tume huru ya uchaguzi

2: Matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani

3: Wagombea binafsi..

4: Rais lazima ashinde kwa 50%

Kwa haya machache tu utaona ya kwamba katiba hii ingekua bora kuliko hii tulio nayo ambayo Rais Magufuli leo anajifaragua anavyotaka kwenye teuzi n.k. kwa mujibu wa Katiba.
 

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,250
Nafasi ilikua ile ,sidhani kama itatokea tena maana magufuli kishasema katiba mpya sio kipaumbele kwa serikali yake
 

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,000
Mleta mada ina maana waliobaki hawakuona umuhim wa hayo? Katiba pendekezwa hipo tayari sasa sijui nikwa jinsigani UKAWA wamezuia hiyo katiba isipigiwe kura...Nifungue mawazo mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom