Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali 2010

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,196
13,186
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji Frederick Mwita Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia leo, Jumamosi, Novemba 6, 2010.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Phillemon Luhanjo inasema kuwa Jaji Werema ataapishwa saa 11 jioni leo katika shughuli itakayofanyika Ikulu.

Kabla ya uteuzi wake, Jaji Werema alikuwa anashikilia nafasi hiyo hiyo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hivyo, anaendelea na wadhifa huo.

Rais Kikwete amefanya uteuzi huo saa chache baada ya kuwa ameapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha miaka mitano katika sherehe iliyofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Saalam.

Imetolewa na
:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM
.

06 Novemba, 2010
 
Ok, happy to him. He has to be fair and protect out Constitution in no ones benefit but the PUBLIC...
 
Serikali yaanza kuundwa sasa, tunasubiri mawaziri. Hivi watatoka wapi? Let wait and see
 
majaji kama MAKAMAE wAMEPOTEZA CREDIDIBILTY YAO TULIYOWAPA HADI UZEE HUU KWA KUWANYIMA RAIA HAKI ZAO ZA KUCHAGUA WAMPENDAO
 
Hehe hivi rais anapomaliza urais wake anakuwa pia ana-afect ajira za wateule wake wote? I mean wakuu wa wilaya, mikoa, AG na kadhalika?

Au werema aliapishwa kwa mkataba mfupi? Ina maana na jaji mkuu mpya ataapishwa punde?
 
jibu ni ukweli anaunda serikali mpya mwanasheria mpya,waziri mkuu mpya....anashirikiana na waziri mkuu kuteua mawaziri wapya na wakuu wa mikoa wapya mwisho kabisa anamalizia na wakuu wa wilaya!si ajabu kukutana na sura mpya nyingi kuliko zile za kale
 
mambo fasta fasta,JK hana jipya

Mama 5J's;

Ni issue ya Katiba: Mtu wa kwanza kabisa kuteuliwa na Rais kabla ya wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali... nadhani ni ili aweze kumsaidia Rais asijevunja katiba.... especially kwa kuwa sio lazima Rais kuwa mwanasheria by professional a.k.a ueledi.
 
ngoja tusubirie mawaziri

nina hamu ya mapya lakini hisia zangu zinashindwa kukwepa hawa... Kawambwa, vita, ngeleja, nchimbi, kombani, mwakyusa, mwinyi, makamba, pinda, lowassa, labda na wawili watatu wapya... Mawaziri kama stini, na washikaji vyeo kama laki
 
fredericwere.jpg

Rais Jakaya Kiwete amemteua rasmi jaji frederick mwita werema kuwa mwanasheria mkuu wa serikali muda mfupi baada ya kuapishwa kwake leo katika uwanja wa uhuru jijini dar.Jaji werema anapata nafasi hiyo kwa mara nyingine kuendelea na wadhifa huo ambao alikuwa nao hapo awali.

KUNA MTU ANAJUA CV YA HUYU MTU ?
 
This is not news... guys... sio kila kitu kujadiliwa Jaji Werema piga mzigo twende mbele!
 
fredericwere.jpg

Rais Jakaya Kiwete amemteua rasmi jaji frederick mwita werema kuwa mwanasheria mkuu wa serikali muda mfupi baada ya kuapishwa kwake leo katika uwanja wa uhuru jijini dar.Jaji werema anapata nafasi hiyo kwa mara nyingine kuendelea na wadhifa huo ambao alikuwa nao hapo awali.

KUNA MTU ANAJUA CV YA HUYU MTU ?

Poa tu, lakini ajitahidi sana maana bunge la safari hii lina Tundu. Asije akafanya kazi kwa mazoea kama katika kipindi kilichopita ambapo alikuwa anasaidiwa na Andrew Chenge kujibu maswali. Isije ikawa ujaji wake nao ni wa kuchakachuliwa
 
state attorney, mkurugenzi wa katiba na haki za binadamu ofisi ya mwanasheria mkuu, jaji wa mahakama kuu na mwanasheria mkuu wa serikali.
 
Hehe hivi rais anapomaliza urais wake anakuwa pia ana-afect ajira za wateule wake wote? I mean wakuu wa wilaya, mikoa, AG na kadhalika?

Au werema aliapishwa kwa mkataba mfupi? Ina maana na jaji mkuu mpya ataapishwa punde?
KAATIBA:tape:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom