Uteuzi wa mgombea wa CCM Korogwe:Yaliyotokea kama ni ya kweli,2020 CCM wengi wataisoma namba na kuelewa kwanini wapinzani wanalilia demkorasia

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,994
144,329
Kuna clip insambaa mitandaoni ambayo ni muendelezo wa ufafanuzi wa kilichotokea Korogwe katika mchakato wa uteuzi wa mgombea ubunge wa jimbo hilo.

Katika clip hiyo ambayo viongozi wa CHADEMA wameendelea kutoa ufafanuzo wa nini kilichotokea ,viongozi hao wamegusia mpaka kilichofanyika ndani ya CCM katika kumteua mgombea wa chama hicho.

Kwa kifupi, viongozi wa CHADEMA huko Korogwe wamedokeza kuwa, kumbe hata mgombea wa CCM aliepitishwa na chama hicho kugombea ubunge wa jimbo hilo alikuwa ni mshindi wa tatu huku wagombea ambao walikuwa popular ndani ya CCM Korogwe kwa maana ya mshindi wa kwanza na wa pili, waliachwa na kumpitisha aliekuwa DAS Arumeru ambae alikuwa ni mshindi wa tatu.

Clip inapatikana katika akaunti ya twitter ya Halima Mdee.

Somo:Kama madai haya ni ya kweli,basi 2020 wana-CCM mjiandae kwa matukio ya aina hii na wakati huo ukifika, ndio mtaelewa umuhimu na thamani ya demokrasia wanayoililia wapinzani leo hii huku nyinyi mkidhani hayawahusu.

Na mjue tu mkitoswa,safari hii upinzani hauwezi tena kuwapokea maana wenzenu(kina Waitara na wengineo) wameshawaharibia na ole wao na wao woteswe hiyo 2020 sijui watakimbilia wapi.
 
CCM ni magufuli na Magufuli ndio CCM yeye ndio anachagua nani awe mgombea na nani asiwe,hiyo kamati inayokaa kuteua mgombea ni formality tu
 
Back
Top Bottom