Naima Naimani
Member
- Aug 23, 2014
- 39
- 147
Majaliwa hakuwa na umaarufu wowote wala hakuna aliyedhani kama angeweza kuibuka yeye.... endelea
UTEUZI WA MBOWE KWA MASHINJI NI SAWA TU NA ULE WA MAGUFULI KWA MAJALIWA.
Na Lumola Steven Kahumbi.
Tar. 12 March 2016. Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo lilikaa huko jijini Mwanza. Pamoja na mambo mengine pia Baraza hilo lilithibitisha jina la Katibu Mkuu wa chama, Dkt. Vicent Mashinji.
Uteuzi huo ni baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu awali Dr. Slaa. Takribani miezi 6 iliyopita Slaa alijiuzulu kutokana na sekeseke la Uchaguzi Mkuu wa JMT 2015.
Mara baada ya Uchaguzi Mkuu. Wafuasi wa CHADEMA nikiwemo na mimi kwa vipindi tofauti tofauti tulijadili sana juu ya Katibu Mkuu mapya ajaye. Na kila mmoja kwa namna yake alikuwa na maoni tofauti, ingawa yapo yaliyofanana. Magazeti nayo hayakuwa nyuma na kwa ajabu kabisa hata Makada wa CCM walijadili sana juu ya nani atakuja kuwa.
Uteuzi wa Dkt. Mashinji hakuna aliyeweza kutabiri ni sawa sawa tu na ilivyokuwa uteuzi wa Mhe. Majaliwa. Hakuna MTU aliyewahi hata kuhisi tu kama Rais kama Magufuli angeweza kumteua Majaliwa kuwa Waziri Mkuu. Inafanana tu nakusema hakuna aliyewahi kuota kwamba Chama kama CHADEMA kitakuja kuwa na Katibu Mkuu kama Mashinji.
Majaliwa hakuwa na umaarufu wowote wa kuwatishia Magwiji wa CCM tuliowazoea kuwaona Majukwaani, kwenye Luninga au wale wa mikakati ya ndani. Hivyo hivyo Mashinji kwa CHADEMA hakuwa na umaarufu kupita Makamanda tuliozoea kuwaona kwenye maandamano, majukwaani au kwenye Luninga.
Majaliwa alijulikana kama Waziri Mpole kuliko wote kwenye Serikali ya Mshua. Kadhalika na Mashinji kwa CHADEMA.
Lakini Mhe. Magufuli alijua ya ziada aliyonayo Mhe. Majaliwa akaamua kumteua. Kama alivyofanya Kamanda Mbowe kwa Mashinji.
Wengi hawakumuelewa Magufuli kwa kuamua kumteua Majaliwa kama ambavyo leo wengi bado hawajamuelewa Mbowe kwa kumteua Mashinji. Lakini miezi mi3 baada ya Majaliwa kuapa wengi sana wamemuelewa Magufuli na wanaamini hakukosea. Tumpe muda Mashinji nina amini tutayashangaa ya Mashinji baada ya miezi mi3 kama ambavyo leo tunayashangaa ya Majaliwa.
Ushauri wangu kwa Makamanda.
Kila MTU atimize wajibu wake. Na tumpe ushirikiano chanya Dkt. Mashinji.
Tukitoa ushirikiano wa Dhati kwa Mashinji. Basi Mashinji kwa CHADEMA atakuwa ni zaidi ya Majaliwa kwa JMT.
Under signature:
14 March 2016
Lumola Steven Kahumbi.