Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,137
Nimeshangazwa sana na hatua ya Rais Magufuli kuteua mawaziri wawili pekee na kudai kuwa uteuzi wa wizara nyingine utafuata baadaye.
Tulishuhudia katika kipindi chake cha awamu ya kwanza, akimaliza karibu miezi miwili bila kuteua waziri yeyote!
Sasa nimekuwa nikijiuliza, kulikoni safari hii ateue mawaziri wawili "faster" ndani ya wiki moja, tokea Tume ya Taifa ya uchaguzi imtangaze kuwa ndiye aliyeshinda nafasi ya urais baada ya uchaguzi mkuu, ambao umelalamikiwa sana na vyama vya upinzani kuwa ulivurugwa?
Nimgependa kujua nini mantiki ya Rais Magufuli kuwateua mawaziri wawili pekee, wakati wizara nyingine pia zikihitaji sana huduma ya mawaziri?
Ndipo hapo ninapojiuliza hivi kuna shguhuli gani za dharura zinazohitaji kuwa ni lazima waziri wa mambo ya nchi za nje, kuwa ni lazima ateuliwe sasa?
Ndiyo maana katika "ramli" yangu nimeona kuna uwezekano mkubwa ameteuliwa waziri wa mambo ya nje, ili akajitahidi kwenda izima kesi iliyofungiliwa huko ICC na chama cha ACT Wazalendo na mwanaharakati Maria Sarungi, ambapo nchi yetu imeshtakiwa kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, nyakati za uchaguzi mkuu, ambao hadi imepelekea kuuliwa kwa wananchi kadhaa wasio na hatia.