Uteuzi wa Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mstahiki, Jun 25, 2009.

 1. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara kama ifuatavyo kwa lengo la kujaza nafasi zilizokuwa wazi pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi kwenye Wizara kama ifuatavyo:-

  1. Bwana ELIAKIM CHACHA MASWI - ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) atakayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kabla ya uteuzi huo, Bwana Maswi alikuwa Kamishna Msaidizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha na Uchumi.

  2. Bwana JUMANNE ABDALLAH SAGINI – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI atakayeshughulikia Elimu ya Msingi na Sekondari. Kabla ya uteuzi huu Bwana Sagini alikuwa Mratibu wa Mradi wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

  3. Dr. SHAABAN RAMADHANI MWINJAKA – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko. Kabla ya uteuzi huu Dr. Mwinjaka alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Makamu wa Rais.

  4. Bi. ELIZABETH JOKTAN NYAMBIBO – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu Bi. Nyambibo alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.

  5. Bwana ULEDI ABBAS MUSSA – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Bwana Mussa alikuwa Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji kwenye Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  6. Dr. PATRICK S. J. J. MAKUNGU – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kabla ya uteuzi huu Dr. Makungu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa ‘Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology’, Arusha.

  Uteuzi huu unaanza tarehe 13 Juni, 2009.

  (Phillemon L. Luhanjo)
  KATIBU MKUU KIONGOZI

  IKULU,
  DAR ES SALAAM
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Dr. PATRICK S. J. J. MAKUNGU, Jamaa down to earth na hard worker aliisha kuwa mkuu wa idara ya kilimo uhandisi SUA...kabla ya kwenda CARMATEC, aliisha tengeneza tractor rahisi la kusukuma kwa mkono...alikosa pesa za kuliendeleza....Kila laheri Msukuma wa Mkolani, Mwanza...
   
 3. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Mkuu hakika unamtambua Prof Makungu ni kweli kabisa kwa uliyoyasema. Tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya
   
 4. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Naona Ma Dr naibu katibu wakuu. Je mabosi wao nao Ma Dr?s
   
 5. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Miganiko,
  Ina maana sasa CARMATEC ndo kwisha habari yake? Maana hata eneo lao serikali imewapa Mandela Institute of Science and Technology, Chuo ambacho kitakuwa na matawi sehemu mbalimbali barani Africa ikiwemo Nigeria, Africa ya Kusini, Tanzania etc. Sehemu ya Tanzania itakuwa na mambo ya biotechnology.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Labda kama atapatikana mtu mwingine dedicated kama Dr Makungu, naamini kuna watanzania vichwa ukiacha kujuana na usanii....Otherwise CARMATEC tusubiri kuisomea arobaini yake!
   
 7. a

  angolile Member

  #7
  Jun 25, 2009
  Joined: Nov 14, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Samahani mjomba halikuwa trector la kusukuma kwa mkono, ila lilikuwa na uwezo wa kutumika kwa kazi mbalimbali kama vile kukoboa mahindi na kusaga nafaka za aina mbalimbali. Naungana na wengine waliompongeza Makungu (Prof.), na hii ni dalili njema ya utumishi wake bora na umakini. Honengera ila usijisahau kwamba utumishi wako ni wa watanzania na si watu wachache. Endeleza umakini wako uliotoka nao SUA. it''scold/cheers
   
 8. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  miganiko,
  Kule kwa Dr. mwere Malecela ni wewe umesifia sana na huyu Dr makungu ni wewe tena umekuja chapchap kumwaga sifa kwa hiyo unawajua karibu wote wanaoteuliwa? mmh!!
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Sasa kama anawafahamu na anafahamu utendaji wao asiwasifie?kwani we unaumizwa na nini?kama una other side of the story zungumza sio kuanza kuhoji vitu visivyo na msingi.
   
 10. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #10
  Jun 25, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hope unaibu wake ni kwa ajili ya sayansi na technologia, sio upande wa ICT, maana wizara hii ina idara kubwa mbili...

  Kama atashughulika na ICT, samahani natafuta asprin nimeze, maana matrekta na mkongo wa fibre wapi na wapi?
   
 11. F

  Felister JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hongereni Drs. R.S Mwinjaka na P.S Makungu. Uyakinifu na uchapakazi ni sifa zenu. Mungu awatangulie na awawezeshe katika kusaidia kubadili sura ya maendeleo ya watu wa Tanzania kupitia wizara zenu.
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  No wonder watu wana fake U Dr kumbe unalipa eeh
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Yego hujachelewa tafuta form za Pacific University ama open University mwaka mmoja unakuwa Dr Masatu!
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wats wrong with dat!
   
 15. s

  skasuku Senior Member

  #15
  Jun 25, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  inakuaje serekalini kumejaa ma Dr. Prof. ... etc na hali ya Mtanzania inazidi kua mbaya. Do we really need these Dr. or Prof. in management?

  Binafsi nafikiri hawa Dr's and Prof's waendelee na shughuli zao zakiutafiti n.k. na tutafute wasimamizi / watekelezaji ambao wanaujuzi wakuongoza.

  No wonder hatuoni matunda yakua na namba kubwa ya wasomi wa aina hii.

  Just thinking out aloud....
   
 16. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Hongera mama Nyambibo..Nakumbuka wakati ule wa wizara ya ushirika na masoko kule Dodoma ukiwa DAP kama ulivyokuwa huko viwanda.
   
 17. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #17
  Jun 25, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Mkuu CARMATEC imepewa kiwanja maeneo ya njiro opposite na kiwanda cha General Tyre kilichokuwa kiwanda cha kiko zamani.Ukarabati wa majengo pamoja na mengine mapya unafanyika nadhani kabla ya mwaka huu CARMATEC itaamia makao yake mapya.

  Naomba kuwasilisha.
   
 18. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  sina tatizo na teuzi zao lakini unaposema down to earth ina maana hutaki watu waseme chochote tena maana from the sky hakuna mwingine hapo katikati,na hata kama una hakika hakuna wengine tuache basi tuwachambue hao hao kwa nini ufunge?kule kwa mama Mwere ndo kabisa umetangaza hali ya hatari kwenye hiyo thread yako loh! Hata hivyo nawapongeza sana japo mwingine jina bado lipo njiani.
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,665
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  mmmhhh....halfu Belly isije ikawa tulikuwa idara moja.....naanza kuogopa wengine mabosi wetu kumbe wako hapa!?:confused:
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bambo Kijiba cha roho mbaya kitamuumiza sana!
   
Loading...