Uteuzi wa Kamishna Sianga Ishara kuwa Makonda Kaharibu Vita

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,314
72,740
Jana mheshimiwa Rais kamteua Kamishna mpya wa Tume ya uthibiti wa madawa ya kulevya, Kamishna Sianga.
Kitendo hicho kufanyika wiki moja tuu baada ya Makonda kuanzisha anayoita vita ya madawa na kutokea kwa malalamiko kuwa njia anazotumia ni ishara kuwa Makosa makubwa yameonekana katika namna Makonda na Sirro wanavyo fanya kazi hiyo?
Serikali ilipotunga sheria maalumu za kupambana na madawa na kuunda chombo rasmi ilielewa ugumu wa uchunguzi na uendeshaji wa kesi za madawa sio Tanzania tuu Bali duniani pote. Sasa kwa nini washauri wa Rais hawakumshauri kabla ya kutoka hadharani kumuunga mkono Makonda kuwa njia anaxotumia sizo na anaharibu uchunguzi kwa kutokujua au makusudi?
Nadhani baada ya Kamishna Sianga kuteuliwa sasa Makonda aamtishwe kunyamaza aache wenye kazi yao wafanye kwa weledi vinginevyo mgongano utaendelea. Na kwa vile hata yeye katajwa kuwa na mahusiano ya mashaka na watu washukiwa acha naye achunguzwe
 
Kosa kubwa analofanya mtu ni kudhani ukiwa na madaraka basi unaweza fanya kila kitu kwa amri yako na kufikiri kila unachosema wewe ni sahihi
Unataka tueleweje? Umesahau kuwa madaraka ndio yanakupa mamlaka na nguvu ya kufanya jambo?

Yaani uwe na madaraka halafu ukae umetulia nayo? Sasa hayo madaraka umepewa ya nini? Bora ubaki kwako ulime bamia
 
Jana mheshimiwa Rais kamteua Kamishna mpya wa Tume ya uthibiti wa madawa ya kulevya, Kamishna Sianga.
Kitendo hicho kufanyika wiki moja tuu baada ya Makonda kuanzisha anayoita vita ya madawa na kutokea kwa malalamiko kuwa njia anazotumia ni ishara kuwa Makosa makubwa yameonekana katika namna Makonda na Sirro wanavyo fanya kazi hiyo?
Serikali ilipotunga sheria maalumu za kupambana na madawa na kuunda chombo rasmi ilielewa ugumu wa uchunguzi na uendeshaji wa kesi za madawa sio Tanzania tuu Bali duniani pote. Sasa kwa nini washauri wa Rais hawakumshauri kabla ya kutoka hadharani kumuunga mkono Makonda kuwa njia anaxotumia sizo na anaharibu uchunguzi kwa kutokujua au makusudi?
Nadhani baada ya Kamishna Sianga kuteuliwa sasa Makonda aamtishwe kunyamaza aache wenye kazi yao wafanye kwa weledi vinginevyo mgongano utaendelea. Na kwa vile hata yeye katajwa kuwa na mahusiano ya mashaka na watu washukiwa acha naye achunguzwe
Hiyo nzuri maana sasa kazi itafanyika katika kanuni na taratibu zinazofa
 
Kwa nini udhani Makonda kaharibu badala ya kudhani kuwa kwa uteuzi huu mh Rais amezidi kuongeza nguvu katika hii vita na jitihada Makonda zimeongezewa nguvu zaidi?
Ukisoma sheria inayotoa mamlaka kwa Tume ya udhibiti wa madawa ya kulevya, RC hawezi tena kuwa kiranja wa vita hii kama anavyoji nasibu. Na ni kweli kama Kamishna huyo ni makini kazi hiyo inaweza kufanyika kwa ufanisi zaidi kisheria
 
Jamani hivi mmemsikiliza Makonda vizuri au mnaandika tu?Mheshimiwa Makonda amesema yeye anashughulikia madawa ya kulevya kwenye mkoa wake Daresalaam tu.Kamishna ni nchi nzima,Mhe.waziri wa mambo ya ndani ni nchi nzima.Kwa sisi tuliosoma hesabu mkoa wa Daresalaam ni component ya nchi nzima yaani Dar+Mwanza+Mbeya+.........=Nchi nzima(Mhe.Waziri) kwa maneno mengine Dar ikishinda vita ya dawa za kulevya bila kudhibiti mikoa yote naweza kusema dawa zitakuwa hazijjadhibitiwa.Of course ukifanikiwa kudhibiti Madawa DARESALAAM ni kama umedhitibiti madawa nchi nzima.
 
Watu tunachanganya,Makonda hajasema ni kiranja wa nchi nzima.Amesema wazi kabisa havuki mipaka ya mkoa wake.
 
Ukisoma sheria inayotoa mamlaka kwa Tume ya udhibiti wa madawa ya kulevya, RC hawezi tena kuwa kiranja wa vita hii kama anavyoji nasibu. Na ni kweli kama Kamishna huyo ni makini kazi hiyo inaweza kufanyika kwa ufanisi zaidi kisheria
Nakupata, ufahamu wangu ni kuwa Makonda kama RC ameliona tatizo katika eneo lake la kazi, hatua ambayo naamini mkuu wa mkoa mwingine au DC yoyote ama mwenyekiti wa mtaa anaweza anaweza kuchukua hatua kwa ajili ya kuokoa hali. Kuwepo kwa tume ya kudhibiti madawa kulevya hakuwezi kuzuia vyombo vingine na mamlaka zingine zisichukue hatua hasa linapokuja suala la kupigana na tatizo la madawa ya kulevya.
 
Jamani hivi mmemsikiliza Makonda vizuri au mnaandika tu?Mheshimiwa Makonda amesema yeye anashughulikia madawa ya kulevya kwenye mkoa wake Daresalaam tu.Kamishna ni nchi nzima,Mhe.waziri wa mambo ya ndani ni nchi nzima.Kwa sisi tuliosoma hesabu mkoa wa Daresalaam ni component ya nchi nzima yaani Dar+Mwanza+Mbeya+.........=Nchi nzima(Mhe.Waziri) kwa maneno mengine Dar ikishinda vita ya dawa za kulevya bila kudhibiti mikoa yote naweza kusema dawa zitakuwa hazijjadhibitiwa.Of course ukifanikiwa kudhibiti Madawa DARESALAAM ni kama umedhitibiti madawa nchi nzima.
Rizi mbona anaishi mikocheni kwa Mwl nyerere na anamkwepa kumtaja?
 
Nakupata, ufahamu wangu ni kuwa Makonda kama RC ameliona tatizo katika eneo lake la kazi, hatua ambayo naamini mkuu wa mkoa mwingine au DC yoyote ama mwenyekiti wa mtaa anaweza anaweza kuchukua hatua kwa ajili ya kuokoa hali. Kuwepo kwa tume ya kudhibiti madawa kulevya hakuwezi kuzuia vyombo vingine na mamlaka zingine zisichukue hatua hasa linapokuja suala la kupigana na tatizo la madawa ya kulevya.
Nadhani bado tupo pamoja. Utendaji wa Tume hii ni kama Tume ya Uchaguzi tuu kwamba yenyewe iko Dar lakini mpaka mawilayani kazi zinafanywa na maafisa mbalimbali but under directives za Tume. Hivyo hata hilo la madawa bado ma RC, RPC, DC na Polisi kwa ujumla bado watafata directives za tume.
Na lengo la kudhibiti halo hiyo ni kuwa ukiacha jambo lisimamiwe na RC kisiasa linaweza kuharibika kiuchunguzi na kisheria na kesi kushindwa. Vilevile biashara hii ni mitandao ya kimataifa hivyo ni Tume pekee yenye uwezo na mamlaka kuwasiliana hata na vyombo vya nje vinavyohusika na vita hii katika kutengeneza kesi
 
Back
Top Bottom