Uteuzi wa Job Masima kuwa Balozi Israel ni ishara ya Rais Magufuli kuinoa na kuiimarisha TISS

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
15,502
22,354
Balozi Job Masima ameanza kazi rasmi ya kuiwakilisha Tanzania nchini Israel akiwa balozi wa kwanza nchini humo tangu Tanzania (wakati huo ikiitwa Tanganyika) ivunje uhusiano wake na taIfa hilo teule yapata miaka 43 ilopita.

Ni mmoja wa mabalozi waloapishwa jana Ikulu kabla ya kwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Ujerumani, Israel na Oman.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mahusiano kati ya nchi hizo mwezi October mwaka 2015 aliekuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete alimkaribisha balozi wa Israel bwana Yahel Vilan alipokwenda kukabidhi hati za utambulisho tayari kuridhia mahusiano ya kimataifa kwa nchi hizi mbili.

Baada ya raisi John Magufuli kuingia madarakani mwezi January mwaka jana Balozi Vilan alimtembelea raisi Magufuli na kumhakikishia uhusiano huo kwamba upo na kusisitiza kwamba Israel itafungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania.

Raisi John Magufuli nae akamhakikishia balozi Vilan kwamba Tanzania ilikuwa mbioni kuhakikisha inakuwa na ubalozi mjini Tel Aviv.

Baada ya Tanzania kupata uhuru wake December 1 mwaka 1961, Tanzania ilifungua ubalozi wake nchini Israel lakini makazi yakiwa nchini Misri.

Mwaka 1973 umoja wa nchi za kiafrika uliamua kujitenga na Israel baada ya nchi hiyo kuwa inaitawala Palestina kwa kuwa na sera za kibaguzi na za kuitenga Palestina na kuizuia kuvuka ukanda wa Gaza.

Lakini pia sababu ingine ilikuwa ni khasa baada ya vita ya Yom Kippor ambapo mataifa sita ya kiarabu yakiongozwa na Misri na Syria yalikuwa yakipigana vita na Israel katika milima ya Golan na Sinai.

Kusudio ya vita hiyo ilikuwa ni kuyakomboa maeneo hayo kutoka kwa Israel ambayo iliyateka baada ya vita ilojulikana kama "six days war" ya mwaka 1967 na pia raisi wa Misri Anwar Sadat alikuwa na mpango wa kufungua mfereji wa Suez.

Pamoja na hayo uhusiano wa nchi hizi haukuwa umezimwa moja kwa moja na ilipofikia mwaka 1995 mahusiano kati ya nchi hizi yalirudishwa na Tanzania ikarejesha ubalozi wa Tanzania Israel lakini makazi yakiwa nchini Misri na Israel ikawa na ofisi ya ubalozi mjini Nairobi nchini Kenya.

Tanzania na Israel walikuwa wakishirikina katika miradi mbalimbali na mmojawapo ni mradi mkubwa wa Bugando nchini Mwanza na miradi mingine.

Mwezi Julai mwaka jana Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alihudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika Mashariki ulofanyika nchini Uganda na akakabidhiwa barua rasmi na waziri wa mambo ya nje ya ushirikiano wa kimataifa na kikanda Dr Augustine Mahiga, kutoka kwa raisi John Magufuli.

Katika barua hiyo raisi Magufuli alimweleza waziri mkuu Netanyahu kwamba Tanzania ilikuwa imeamua kufungua rasmi ofisi ya ubalozi nchini Israel.


Dr Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri mkuu wa Israel mjini Entebbe mwezi julai mwaka 2016. (Picha na Kobi Gideon wa GPO)

Israel inajulikana duniani kwa kuwa wataalam kwenye maeneo ya kilimo na umwagiliaji, Israel ina kiwanda kikubwa cha plastiki kijulikanacho kama Plazit Polygal Group ambacho kina wafanyakazi wapatao 500 na kinapata faida ya mauzio kiasi cha doka milioni 250 kwa mwaka.

Pia Israel inajulikana duniani kwa utengenezaji bidhaa mbalimbali za kiteknolojia zikiwemo satellite, silaha za kivita kama makombora na ndege zijiendeshazo zenyewe au Drones.

Lakini kikubwa zaidi ni kuhusu jeshi la Israel ambalo mpaka kufikia mwaka 2015 matumizi ya jeshi la Israel yaani "military expenditure" nchi hiyo ni ya 15 duniani huku ikiwa ni nchi ya 8 kwa uuzaji wa silaha duniani.

Asilimia 20 ya bajeti ya ulinzi ya nchi hiyo inatolewa na Marekani sawa na dola bilioni 3.8 kwa mwaka baada ya kutiliana saini mkataba utakaokuwa ni wa mwaka 2018 hadi 2028.

Uteuzi wa balozi Job Masima hauwezi kupita bila kuangaliwa kwa jicho la tatu kwani unaelekeza wadadisi kuona kwamba ni uteuzi wa kimkakati zaidi.

Kabla ya uteuzi wa balozi Masima, alikuwa ni katibu mkuu wizara ya Ulinzi na jeshi la kujeng taifa nafasi ambayo aliichukua mwaka 2011 alopoteuliwa na aliekuwa raisi wa serikali ya awamu ya nne Jakaya Kikwete.

Lakini balozi Job Masima ni mmoja wa watu muhimu sana katika kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania, akiwa tayari amekaa sehemu mbalimbali za ulinzi na usalama, raisi Magufuli ameamua kumpa majukumu ya kuimarisha uhusiano wake na Israel lakini kukiwa na malengo maalum.

Raisi John Magufuli ametambua haja ya kuimarisha idara ya ujasusi Tanzania TISS na amekusudia kuiimarisha kiutawala na kiutendaji ambapo vijana wengi sasa wanapata nafasi za kujiendeleza zaidi na kijifunza mbinu mpya za ulinzi wa taifa khasa katika ulimwengu wa leo ambao umejaa mikikimikii ya kila aina.

Hapo ndipo unapokuja kuwaamini Israel katika masuala ya ulinzi na usalama kwani wana msemo wao ambao unasema kwa kiingereza kwamba "Security is a subject that can be taught theoretically, but nothing is a substitute for a real hands-on experience and we've got lots of it."- yaani wakimaanisha kwamba usalama ni somo ambalo laweza kufundishwa kinadharia, lakini hakuna mbadala wa mikono halisi yenye uzoefu ambayo tunayo mingi tu.

Ni dhahiri kuwa yanayojiri leo hii ni pamoja na nafasi pana ya mawasiliano kati ya maofisa, muunganiko yaani "coordination" kati ya idara na idara na uimarishaji wa "kitengo" ambacho ndicho kiko katika ngazi ya juu kabisa ya uangalizi wa taifa hili.

Bila shaka Israel inatusaidia katika nyanza mbalimbali za ulinzi na usalama, uchumi na maendeleo mengine kwa ujumla, lakini Amani na utulivu na ustawi wa watanzania unahitaji ulinzi na usalama imara.

Ulinzi na usalama imara ndiyo nguzo ambayo inahitaji kuboreshwa kwa gharama yoyote ile na hiyo ni moja ya mipango ya serikali ya awamu ya tano.

Waweza kupata mwanga wa nini nimekusudia katika Makala hii ndogo kwa kujikumbusha Makala hizo hapo chini, lakini wenzangu wadadisi wa masuala ya ujasusi kama mkulu Yeriko Nyerere naomba michango yenu kwa kuongezea nyama kwenye hili.

Je, raisi John Magufuli anajimaarisha kiusalama zaidi au anaisuka zaidi TISS?

Je, balozi Job Masima ana cheo gani kijeshi?

Ujasusi wa Kiuchumi na Kiteknolojia unakuwa kwa kasi, Je Tanzania iko tayari

Wazee Mwang'onda na Hassy Kitine waasisi wa TISS imara Tanzania

https://www.jamiiforums.com/threads/hili-ni-jaribio-jingine-kwa-system-state-au-kitengo.896405/
 
Mkuu umeleta uzi mzuri sana, Mkuu ana nia ya dhati kabisa ya kuumarisha taasisi yetu hii ya Usalama ambayo kiuhalisia imekuwa iko operate locally sana na haitakii kubadilika kwa mwavuli tu wa kuwa utendaji wao ni secret Mheshimiwa JPM alianza kuonesha nia ya ya dhati pale tu alipo mteua Modestus kipilimbi kama GD wa idara Kumuweka tu mtu ambae ni professional wa Computer science basi kutamfanya aipelekee idara Kisasa kabisa , Mbinu za Intelligence karibia katika agency zote ni Moja tunachozidiana Ni technology leo ukiangalia M15 ya uk au FBI utaona wanapopishana ni Tech tu, Uteuzi huo wa Job masima kama Balozi utaleta matokeo chanya katika kujifunza na kupata mapya juu ya usalama Huko.
 
Mbona Trainers wao wengi huwa wanatokea huko huko Israel na mara nyingi Wajanja huwa tunagongana nao sana pale JNIA wakiwa wanakuja kuwafunza Vijana katika Vyuo vyao? Sasa unaposema kuwa Ubalozi umeanzishwa ili kuiimarisha hiyo idara unataka kutuambia nini labda ambacho hatukijui?

Nakumbuka mwaka juzi Trainer mmoja ( najua Vijana wa Idara mliokuwa zamu pale JNIA ) mtakumbuka baada ya huyu Trainer wa Kiyahudi kutoka Mossad alipokuwa anaingia aliambiwa akaguliwe vitu vyake lakini akakataa kata kata na Jamaa walipozidi kumlazimisha akatishia kugeuza na kurudi Kwao ndipo ikapigwa Simu Magogoni kwa Mkwere na Chuoni baada ya hapo ikatoka tu amri kuwa aruhusiwe kupita na asikaguliwe Jamaa akaingia nchini kweli na kutufundishia Vijana kwa wiki mbili tu lakini waliofunzwa wanasema mafunzo yake utadhani ni ya mwaka na baadae akaondoka zake.
 
Mbona Trainers wao wengi huwa wanatokea huko huko Israel na mara nyingi Wajanja huwa tunagongana nao sana pale JNIA wakiwa wanakuja kuwafunza Vijana katika Vyuo vyao? Sasa unaposema kuwa Ubalozi umeanzishwa ili kuiimarisha hiyo idara unataka kutuambia nini labda ambacho hatukijui?

Nakumbuka mwaka juzi Trainer mmoja ( najua Vijana wa Idara mliokuwa zamu pale JNIA ) mtakumbuka baada ya huyu Trainer wa Kiyahudi kutoka Mossad alipokuwa anaingia aliambiwa akaguliwe vitu vyake lakini akakataa kata kata na Jamaa walipozidi kumlazimisha akatishia kugeuza na kurudi Kwao ndipo ikapigwa Simu Magogoni kwa Mkwere na Chuoni baada ya hapo ikatoka tu amri kuwa aruhusiwe kupita na asikaguliwe Jamaa akaingia nchini kweli na kutufundishia Vijana kwa wiki mbili tu lakini waliofunzwa wanasema mafunzo yake utadhani ni ya mwaka na baadae akaondoka zake.
Simu ikapigwa magogoni na nani?
 
Mbona Trainers wao wengi huwa wanatokea huko huko Israel na mara nyingi Wajanja huwa tunagongana nao sana pale JNIA wakiwa wanakuja kuwafunza Vijana katika Vyuo vyao? Sasa unaposema kuwa Ubalozi umeanzishwa ili kuiimarisha hiyo idara unataka kutuambia nini labda ambacho hatukijui?

Nakumbuka mwaka juzi Trainer mmoja ( najua Vijana wa Idara mliokuwa zamu pale JNIA ) mtakumbuka baada ya huyu Trainer wa Kiyahudi kutoka Mossad alipokuwa anaingia aliambiwa akaguliwe vitu vyake lakini akakataa kata kata na Jamaa walipozidi kumlazimisha akatishia kugeuza na kurudi Kwao ndipo ikapigwa Simu Magogoni kwa Mkwere na Chuoni baada ya hapo ikatoka tu amri kuwa aruhusiwe kupita na asikaguliwe Jamaa akaingia nchini kweli na kutufundishia Vijana kwa wiki mbili tu lakini waliofunzwa wanasema mafunzo yake utadhani ni ya mwaka na baadae akaondoka zake.

Mkiwa na ofisi Tel Aviv itakuwa ikiratibu shughuli zote ambazo hapo awali zilikuwa zinaleta utata khasa kwenye clearance ya hao trainers kuja Dar.

Nafikiri umeeleza kuhusu huyo myahudi wa mwaka juzi, ambapo kama kila kitu kingekuwa kimemalizwa mjini Tel Aviv basi angetua na kupita tu hapo JNIA bila mizengwe.

Pili, kwa ajili ya kuwa na faragha kati ya mipango yetu na Israel si jambo jema kuwa na ofisi mjini Nairobi hivyo kuweka ofisi yao Dar-es-Salaam na sisi Tel Aviv basi hata wakenya hawataweza kudukua ni masuala gani ya maslahi na usalama wa taifa yanajadiliwa kati ya Tanzania na Israel.
 
Umeandika vyema sana.

Japo, nimesikitika sana kuona ama kusoma.kuwa pana mtu alikuja akapata shida ya kuingia japo JNIA yaani, sielewi kabisa sisi hapo Tanzania, unawezaje ukamuita mkufunzi toka nchi nyingine halafu ushindwe kumpokea hadi Simu ipigwe kutoka feri na chuoni?

Hii ni aibu kubwa na pia ni uratibu na ukaribisha wa wageni kuto nje ya nchi kuja huko Tanzania wa kiwango cha zero brains kabisa.

Intelligence services, wanashindwaje kumpokea mtu kwa ajili yao?

Ni aibu kama hayo ni kweli , wanahiitaji kufanyiwa msasa na PR and Protocol unity iwepo.

Ila, nimuulize mwandishi wa thread hii, kwa nini wewe unaona ulinzi na usalama kwa Tanzania kushirikiana na Israel na siyo nyanja zingine za maendeleo maana naona ndiyo sekta umeipatia kipaumbele? Ni kwa nini?
Ahsante.
 
Umeandika vyema sana.

Japo, nimesikitika sana kuona ama kusoma.kuwa pana mtu alikuja akapata shida ya kuingia japo JNIA yaani, sielewi kabisa sisi hapo Tanzania, unawezaje ukamuita mkufunzi toka nchi nyingine halafu ushindwe kumpokea hadi Simu ipigwe kutoka feri na chuoni?

Hii ni aibu kubwa na pia ni uratibu wa wageni wa kiwango cha zero brains kabisa.

Intelligence services, wanashindwaje kumpokea mtu kwa ajili yao?

Ni aibu kama hayo ni kweli , wanahiitaji kufanyiwa msasa.

Ila, nimuulize mwansishi wa thread hii, kwa nini wewe unaona ulinzi na usalama kwa Tanzania kushirikiana na Israel na siyo nyanja zingine za maendeleo maana naona ndiyo sekta umeipatia kipaumbele? Ni kwa nini?
Ahsante.

Ni kweli kuna nyanja mbalimbali za ushirikiano kati ya Tanzania na Israel kama nilivyooanisha hapo juu japo ni kidogo.

Lakini Israel ni watu wenye uwezo mkubwa sana katika masuala ya kiteknolojia, sayansi, kijeshi na kiusalama.

Kama unakumbuka kampuni ya Apple ilipoingia kwenye mgogoro na FBI kuhusu simu ya IPhone ya yule muuaji wa California Syed Farook kwamba isingetoa siri ya namna ya kuifungua simu hiyo kwa ajili ya uchunguzi, baadae kampuni ya Israel ndiyo ilikuja kufungua simu hiyo.

Nimeeleza kuhusu kampuni hii ya Cellebrite katika moja ya Makala zangu kwenye jukwaa hili na wanavyofanya kazi.

Kampuni ya Cellebrite ni kampuni kubwa sana ya teknolojia duniani na ina matawi sehemu kadhaa kiasi cha kufikiria kutafuta masoko Zaidi katika nchi za Afrika Tanzania ikiwa ni mojawapo.

Israel pia ni wataalam na wana teknolojia ya juu katika masuala ya "surveillance" na hivyo watapata nafasi na soko la kuuza bidhaa zao zinazohusiana na eneo hili.

Pia ukitaka kujua namna ulinzi wa viwanja vya ndege vya Israel ulivyopewa kipaumbele nchini Israel basi unapaswa kwenda Israel na ukifika nchini humo utajifunza mengi, kwani hapa sitaelezea mengi kutokana na sababu mbalimbali.

Mwisho wayahudi wana misemo miwili muhimu kabisa kuhusiana na ulinzi na usalama wa Israel, kwanza wanasema "what can I do for Israel" na mwingine wanasema "what can I do to help brothers ans sisters in Israel".

Ni lazima unaelewa njia za kuilinda nchi yako na hata unapokuwa vitani unatakiwa kukumbuka vitu vitatu, jina lako, namba inayokutambua yaani code na royalty uzalendo.

Nafikiri umenielewa ndugu.
 
mh, mimi sina cha kuongezea lakini, tukiamka tukikiponya hiki kikundi cha Tiss mikononi mwa ficiem naamini nchi itanufaishwa sana na TISS wanafaida sana hawa lakini wapo chini ya mwalimu wa ufisadi naamini nao watamlinda mwalimu wao tu badala ya kutulinda wanafunzi

Mkuu, kwanini unadhani tiss ni kikundi cha fisiem?
 
Back
Top Bottom